Saturday, October 17, 2015

YANGA NA AZAM ZATOKA SULUHU YA BAO MOJA KWA MOJAWachezaji wa Yanga wakishangilia  goli lilifungwa na mshambuliaji wao hatari, Donald Ngoma

Beki wa Yanga,Kelvin Yondani akiwania mpira na beki wa Azam,Pascal Wawa (kulia) na kipa Aishi Manula katika mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

. Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma (kushoto) akimtoka beki wa Azam,Pascal Wawa (katikati) na Agrey Morris  katika mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa

Mshambuliaji wa Yanga,Donald Ngoma (kulia) akifunga goli katika mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam,kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ea Salaam jana, kushoto ni kipa wa Azam Aishi Manula na beki wake Agrey Morris

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KUAGA MWILI WA DEO FILIKUNJOMBE LUGALO

 SPIKA W ABUNGE NA MH KAFULILA
 WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKITOA POLE KWA SPIKA WA BUNGE ANA MAKINDA
 MGOMBEA URAIS WA CCM DK JOHN POMBE MAGUFULI AKIMFARIJI MKE WA MAEREHEMU DEO FIIKUNJOMBE
 WAOMBOLEZAJI

 RAIS JAKAYA  KIKWETE  AKIAGA MIILI YA MAREHEMU AKIWEMO ALIYEKUW AMBUNGE WA RUDEWA DEO FILIKUNJOMBE

KIONGOZI WA ACT ZITTO KABWE AKIAGA MIILI YA MAREHEMU

DIMOND AWASILISHA TUZO KWA MASHABIKI

 Msanii Nassib Abdul Diamond (katikati), Meneja wa Tigo music Hamza Balla (kushoto) na Mtaalam wa mitandao ya kijamii toka Tigo Samira Baamar wakiwa kwenye picha ya pamoja kuwaonyesha mashabiki tuzo alizonyakua za Afrimma.
 Msanii Diamond Platnum akiongea na waandishi wa habari na mashabiki waliojitokeza kumpokea  mara baada ya kuwasili kutoka nchini Marekani alikopokea Tuzo za Afrimma. Wengine kushoto kwake Meneja wake Babu Tale, Meneja wa Tigo music Hamza Balla, na Mtaalam wa mitandao ya kijamii toka Tigo Samira Baamar.
Meneja wa Tigo music, Hamza Balla akiongea na waandishi wa habari na mashabiki waliojitokeza kwa wingi kumpokea msanii wa kizazi kipya Nassib Abdul Diamond (kushoto)mara baada ya kuwasili kutoka nchini Marekani alikopokea Tuzo za Afrimma. Pembeni kulia Mtaalam wa mitandao ya kijamii toka Tigo Samira Baamar.

Wednesday, October 14, 2015

MWAMUNYANGE KUWASILI LEO NCHINI


UBUNGO YATIA FORA KWA BENDERA ZA VYAMA VYA SIASA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

 Sehemu ya makutano ya barabara ya Morogororoad na Samunijoma eneo la ubungo likiwa limepambwa na bendera za vyama vya Siasa

MAMA MARIA NYERERE AFANYA IBADA YA KUMKUMBUKA MWALIMU NYERERE

MJANE wa Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,mama Maria Nyerere,ameshiriki misa ya shukrani katika kumbukumbu ya miaka 16 ya kifo cha muasisi wa taifa la Tanzania katika Kanisa Katoriki Parokia ya Butiama huku suala amani kuelekea uchaguzi mkuu likizungumzwa na viongozi wa dini.

Akitoa neno wakati wa misa hiyo,Padri wa Jimbo la Musoma na Katibu wa Askofu wa Jimbo la Mara,William Bahitwa,alisema wakati watanzania wakiwa wanafanya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere wanapaswa kutafakari na kuyafanyia kazi mazuri yote aliyoyafanya na kutanguliza amani hasa katika wakati huu wa uchaguzi.

Alisema Mwalimu Nyerere amelifanyia taifa la Tanzania mambo mengi ambayo yanapaswa kukumbukwa na kila mmoja na kudai iwapo yale yote ambayo amekuwa akipingana nayo na watu wakiamua kufanya watakuwa awamuenzi kwa dhati.

Bahitwa alisema suala la amani limekuwa likihubiliwa na Mwalimu Nyerere kwa kujua iwapo amani itakosekana na kuwa na mtafaraku mambo mengi yatashindwa kufanyika ikiwepo shughuli za kiuchumi katika kujiletea maendeleo kwenye familia na taifa.

Alisema ni jambo la kumshukuru Mungu kumleta Mwalimu Nyerere katika taifa la Tanzania na ikiwa inahadhimishwa miaka 16 baada ya kifo chake bado ataendelea kukumbukwa na maneno yake bado yanapatikana kwenye vitabu na hotuba zake alizoziacha.

Kiongozi huyo wa dini alisema,Kanisa Katoriki kutokana na mchango wa mwalimu Nyerere katika masuala mbalimbali na imani aliyokuwa nayo,limeamua kuanzisha mchakato wa kumtangaza mtakatifu na kwa sasa tayari ameshatangazwa kama mtumishi wa Mungu Mwalmu Julius Kambarage Nyerere.

“Kanisa limeanza mchakato wa kumtangaza kama mtakatifu,na mchakato una hatua ambazo unapitia na kwa sasa mwalimu anatambulika kama mtumishi wa Mungu na michakato inaendelea ili aitwe mtakatifu.

“Naomba tunapoenda kwenye uchaguzi tuzingatie suala la amani na kila mwana siasa awe tayari kukubaliana na matokeo katika uchaguzi kwani wakati kama huu katika mataifa mengine ndio tumekuwa tukishuhudia uvunjifu wa amani.”alisema Padri Bahitwa.

Akizungumza na Mtanzania kuelekea uchaguzi mkuu,kiongozi wa ukoo wa Mwalimu Nyerere,Chief Japhet Wanzagi,alisema baba wa taifa alikuwa mtu ambaye alikuwa akisisitiza suala la amani wakati wote na kuwaomba watanzania wakati wakielekea kwenye uchaguzi kulipa kipaumbele suala hilo.

Alisema wito wake kwa watanzania ni kujitokeza kupiga kura kwa wagombea wanao wahitaji baada ya kusikiliza mikutano ya kampeni na hakuna sababu ya kufanya matendo ambayo yanaweza kutoa viashilio vya uvunjifu wa amani.

BUTIKU AWATAKA WATANZANIA KUMCHAGUA MGOMBEA AMBAYE SIO MLA RUSHWAMKURUGENZI  Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, amesema katika muda huu wa kuelekea uchaguzi mkuu ni vema watanzania watazamane nani ni nani na alifanya nini katika nchi hii.
Aliyasema hayo jana katika mkutano wa amani ulioandaliwa na taasisi hiyo na kufanyika katika ukumbi wa Blue Pearl jijini Dar es Salaam ambapo ulihudhuriwa na wananchi mbalimbali wakiongozwa na watoa mada ambao ni pamoja na Butiku, mjumbe wa bodi ya wadhamini wa taasisi hiyo, Getrude Mongela na Humphrey Polepole ambaye ni mjumbe.
Akitolea mfano wa kashfa iliyotokea kwenye serikali inayomaliza muda wake Butiku alisema watu wamekuwa wakijadili kuhusu uwajibikaji na kusema kuwa mtu fulani (hakumtaja jina) aliwajibika ili kumwokoa rais wake na serikali yake lakini bado watu hawafahamu ukweli.
Hata hivyo alisema “ubishi” huo ulitakiwa kuanza mapema na si wakati huu wa uchaguzi ambapo kila mtu anafanya jambo ili aweze kupata madaraka.
“Ubishi huu ulistahili kujitokeza mapema na si sasa hivi” alisema Butiku na kuongeza kuwa uwajibikaji umekuwa si wa viongozi bali ni wa taasisi suala ambalo alipingana nalo kwa kusema viongozi ndio wanaotakiwa kuwajibika.
“Sasa hivi watu wamekuwa wakizungumzia taasisi utasikia CCM (Chama cha Mapinduzi), Chadema (Chama cha Demokrasia na Maendeleo), NCCR Mageuzi, CUF na vingine lakini viongozi ndio wakuwajibika na hawana namana ya kukwepa ukweli huu.
Alisema viongozi wasikwepe wajibu wao kwasababu wao ndio hukabidhiwa dhamana ya kushughulikia umaskini, rushwa na ufisadi, viongozi wanaochaguliwa katika chaguzi zote zilizopita na huu unaokuja ndio ambao awali waliwahi kukabidhiwa dhamana ya uongozi na baadhi yao ndio leo wanaoomba nafasi za uongozi ili wasaidiane na wananchi kusimamia mambo yote ya wananchi.
“Kukubali kuwajibika ndio badiliko la msingi linalotakiwa sasa, kujaribu kukwepa uwajibikaji ama wa kiongozi binafsi au wa uongozi wa pamoja hasa katika ngazi ya taifa ndiyo dalilili ya uhakika ya kukataa mabadiliko. Falsafa ya uongozi inasema kuongoza ni kuonyesha njia na ili kuongoza ni lazima kuwa mbele na kuonyesha mfano na kiongozi mzuri ni yule anayeonyesha njia. Tujifunze kujua wananchi wanataka nini ili iwe rahisi kuwaongoza,” alisem Butiku.
Alisema mapungufu yaliyopita na yaliyopo katikka kuwahudumia watanzania yanatokana na mapungufu ya viongozi mmoja mmoja na katika umoja wao ambapo aliongeza kuwa uwajibikaji katika mapunguufu hayo ni wa viongozi na si wa chama au serikali.
Aidha aliwataka wananchi kutowaamini watu wanaoomba ridhaa ya kuongoza na wanafanya kila jitihada kukwepa wajibu wao binafsi au wa kundi lao la uongozi wa pamoja na kusema kuwa viongozi wa ain ahiyo hawafai.
Alisema viongozi wengi wamejenga tabia na hulka ya kuwahutubia wananchi badala ya kuwapatia utaalam, zana za kisasa za kilimo, kuwapa ardhi na kuwapimia, kuweka mipango ya kilimo cha umwagiliaji, ufagaji n auvuvi wa kisasa, kujenga viwanda vikubwa na vidogo na hasa vile vya kusindikia mazao ya wakulima ili kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo.
“Hili ni tatizo la uwajibikaji na kukubali ukweli wote kuhusu uwajibikaji. Viongozi waliopita na waliopo kwa miaka yote 54 ya uhuru wa nchi yetu ukiondoa vijana wa miaka 18 iliyopita walikuwepo,” alisema Butiku na kuhoji nani amlaumu nani ikiwa viongozi hao waliokuwepo na waliotoka ndani ya chama hicho wapo?
Aidha alisema hakuna wakumnyooshea kidole mwenzake kwasababu wote walishiriki katika uamuzi na utekelezaji na kwamba hakuna aliyewahi kuwajibika.
“Rushwa na ufisadi umekuwepo kwa miaka mingi kadhalika matatizo ya ardhi, elimu, afya, maji na ajira. Naniu aliwahi kujiuzulu wadhifa wake kwa kutoridhika na utekelezaji ndani ya chama au serikali?” alihoji Butiku.
MONGELA
Kwa upande wake Mongela alianza kutoa mada yake kwa kusema anawashangaa watu wanaosema hawawezi kuongozwa na wazee kama yeye lakini bado kuna wazee wanagombea nafasi ya urais.
Aidha alisisistiza kuwa mabadiliko lazima yaletwe na vijana na si wazee waliochoka midhili yake.
“Kama mnatafuta watu wakuongoza mabadiliko tafuteni vijana, wazee kama sisi tumeshachoka na muda wetu umekwisha,” alisema Mongela.
Akizungumzia suala la amani alisema Tanzania ilikuwa maskini na sasa ni maskini lakini amani bado ipo na kuhoji kama ni sahihi kuwa maskini ambao hawana amani.
“Tulikotoka tulikuwa masikini na tulikuwa na amani, tukaendelea na umasikini haujaisha lakini tupo na amani. Je mnataka hata amani tuipoteze?” alihoji Mongella na kutolea mfano taifa la Misri ambapo alisem awaliandamana na kumtoa kiongozi wao kwa fujo na sasa wanapinduana kwasababu walifanya mabadiliko bila kufikiria.
Kuhusu uchaguzi alisema ndiyo sehemu sahihi ya kufanya mabadiliko lakini akataatharisha kutofanya mabadiliko ya hasira na yasiyo na amani.
“Tunaenda katika uchaguzi na uchaguzi kuna uchungu na wasiwasi wa kutochaguliwa na watu wenye wasiwasi hawana amani na mtu wa namna hiyo hawezi kuwa na heshima. Lazima tuwe na utii wa sheria na kila mtu akitekeleza wajibu wake tutakuwa na uchaguzi wa amani,” alisema Mongella.
TASLIMA
Akichangia mjadala katika mdahalo huo Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Twaha Taslima, alitoa ujumbe wan chi za afrika mashariki na kusema wanaiombea amani Tanzania kwasababu ndiyo nchi iliyopakana nan chi zote za Afrika.
Aidha aliitaka Tume tya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutenda haki kwenye uchaguzi ujao kwani kinyume na kufanya hivyo amni iliyopo inaweza kutoweka japo hakun aanyetaka iwe hivyo.
Aidha aliishauri tume kuairisha uchaguzi pale ambapo itaona mambo hayaendi vizuri ili kuinusuru amani iliyopo.
“Nimekuja hapa kuleta ujumbe wa nchi za Afrika Mashariki, wanatuombea amani kwasababu tumezungukwa nan chi zote za Afrika Mashariki n atumekuwa na mchango mkubwa katika kurudisha amni kwenye nchi zao, tunaomba NEC isaidie kuhakikisha amani hii inakuwepo kwa kutenda haki na pale inapoona mambo hayaendi vizuri ni bora wakahairisha uchaguzi sisi tupo tayari,” alisema Taslima.
Kwa upande wake Humphrey Pole pole ambaye ni miongoni mwa washiriki wa taasisi hiyo, alisema kushindwa kuwajibika na kuwambana na ukweli mwisho wake uwendea  uongo na kudai kwamba kufanya hivyo heshima haitakuwapo.
“Ustahimilivu wetu haupo tena, siku hizi ukisema kitu ambacho mwingine hataki kusikiliza na matokeo yake utatolewa lugha chafu tabia ambayo hipo kwenye mitandao ya kijamii,”alisema Pole pole.
Alimnukuu Mwalimu Nyerere kwa kusema kwamba aliubiri siasa safi na uongozi bora na kutolea mfano wa baadhi ya wanachama wa vyama mbalimbali nchini kwa tabia ya kuzomea wengine barabarani na kudai kwamba kwa kufanya hivyo ni kuwanyima uhuru wa maamuzi huku viongozi wakikaa kimya bila ya kukemea jambo hilo.
Alisema hafurahishwi na anayoyaona leo katika maisha yake tabia ya viongozi kumungunya maneno huku wakiendelea kuhubili uongo kwa kudai kwamba haelewi utokea kwa lengo gani.
“Uongo ni adui yetu mkubwa, tulipokuwa tuki yasema hayo hapo awali wenzetu walitutukana tukiwa na mzee  wetu Butiku kuwaeleza kwamba tunamatatizo na kujaribu kuwa uma sikio juu ya hilo.
Alisema kwamba aliwahi kusema kwamba endapo CCM wangemchagua  fisadi angezunguka nchi nzima kupinga jambo hilo na kujaribu kutolea  muktadha wa Mwalimu Nyerere wa mwaka 1995 kwa kudai kwamba kwa wakati huo wananchi walichoka na rushwa na kuongezea kuwa uongozi si utajiri, ukabila, udini na kuwataka wapiga kura kuwatathimini wagombea wao.
“Tuwanze kwa kusema kijiko ni kijiko na bereshi si kijiko kikubwa, nikiona mtu  ndani ya CCM ameyazuia maoni ya wananchi niko lazi kupambana nae.
“Televisheni tatu wamesema Polepole nisiende  kwenye mijadala yao, leo hii kuna magazeti hazitoi makala zangu,”alisema na kuongezea kwamba kushindwa kwa vyama vya upinzani kutekeleza ajenda ya ufisadi ambayo ndio ajenda ya taifa na CCM kujitutumua kwa kufungua mahakama ya ufisadi ndio mabadiliko ambayo kwa upande wa vitabu vya dini tukio hilo linahashiria kuwa ni siku ya mwisho umewadia.
Pia alikemea kauli za kichochezi kwa vyama vyote ambapo alitolea mfano kauli ya ‘Bao la Mkono’ iliyotolewa na Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye, kwenye mkutano wa kampeni Mtwara na ile ya UKAWA, Tanganyika Packers kuwa si nzuri.
“Baada ya kauli ile nilimkanya Nape lakini sikumuona kiongozi aliyejitokeza na kukemea ile kauli ya ikiwa kama uchaguzi utakuwa uhuru na haki CCM ijiandae kukabidhi Ikulu na kama wakikataa watatumia nguvu ya umma kwenda Ikulu
“Kwenda kudai Ikulu kwa nguvu ya umma kwenye sheria ni kitu gani kitatokea?,”alisema Polepole.
Akihitimisha mdahalo huo Butiku aliwatahadharisha vijana kuwaepuka wazee wanaowachonganisha badala ya kuwaeleza ukweli na kudai kuwa wazee wanaohama miji saa za mwisho wanamatatizo.
“Ukiona baba au babu anahangaika saa za mwisho na kuhama mji ujue huyo ana matatizo, wazee si watu wakuchonganisha bali ni watu wakupatanisha sasa wazee wamekuwa wachonganishi badala ya kuwaeleza ukweli,” alisema Butiku.
Alisema vijana wanaweza kuvaa mashati ya vyama lakini watafute ukweli na baada ya kujua ukweli wakafanye uamuzi kwa kuangalia dhamira zao.
“Vaeni mashati ya vyama lakini tafuteni ukweli wa mambo na mkishaujua ukweli mkafanye uamuzi kwa kuangalia dhamira zenu…mtu ukifanya uamuzi bila kuangalia dhamira yako kesho yake usimlaumu mtu,” alisema Butiku.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...