Friday, October 30, 2015

KASSIM MGANGA AINANGA TIP-TOP CONECTIONMSANII wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Kassim Mganga, amedai kwamba alipokuwa kwenye kundi la Tip Top Connection alikuwa kama mtoto wa kambo kutokana na kutokushirikishwa kwenye mambo mbalimbali ya kundi hilo.
Akihojiwa katika kipindi cha Mkasi, alisema alipokuwa kwenye kundi hilo alikuwa akiwekwa kando na hakujua sababu ilikuwa nini.
“Babu Talle hakuwa baba bora kwangu, naweza kusema hivyo kwani alinifanya nijisikie kama mtoto wa kambo, hakuwa akinishirikisha chochote,” alisema.
Alisema kutokana na kutokuridhishwa na hali hiyo, aliamua kujitoa na kuamua kufanya kazi zake mwenyewe ambapo kwa sasa anajivunia kwa kazi zake kukubalika.

MATOKEO YA UBUNGE MBAGALA YAPINGWA NA UKAWAWAGOMBEA  wa vyama tofauti waliokuwa wanagombea ubunge   Mbagala wameungana kupinga matokeo yaliyobandikwa katika Kituo cha Shule ya Msingi Majimatitu ambayo yamempa ushindi mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Issa Mangungu.
Wagombea hao wanaotoka katika chama Cha Wananchi (CUF), ACT- Wazalendo, AFP, NCCR-Mageuzi, wanayapinga matokeo hayo wakidai si ya halali.
Matokeo yaliyobandikwa katika kituo hicho na kugongwa muhuri wa Mkurugenzi yanaonyesha mgombea wa CCM, Mangungu ameshinda kwa kura 87,249 akifuatiwa na wa CUF , Kondo Bungo aliyepata kura 77,043.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za chama hicho, Temeke  Dar es Salaam, Bungo alisema matokeo hayo yamepikwa na ni kinyume na sheria.
"Tunayakataa kwa sababu katika.makubalino yetu.juzi na.mkurugenzi wa Temeke, Photidas Kagimbo, tulikubaliana uchaguzi umeharibika na ilikuwa jana atoe tamko lakini hata uhakiki bado haujafanyika.
“Juzi tulibaini kasoro nyingi ikiwamo kasoro ambayo Kata ya Kijichi ilionyesha nimepata kata moja wakati karatasi za wakala zinaonyesha nimepata kura 78  na kuna kata ilikuwa na vituo 94 lakini walileta matokeo ya vituo 80 na mkurugenzi alikiri kasoro hizo...tunashangaa jana wamebandika na yana muhuri wa mkurugenzi,” alisema Kondo.
Alisema wameamua kufanya mazungumzo na wanasheria wao  kuweza kutoa uamuzi wa pamoja kuhusiana na matokeo hayo.
Kondo alisema anachoweza kusema ni kuwa wananchi wa Mbagala wafahamu haki yao imepokwa na wao binafsi kila mmoja atajua jinsi ya kudai haki yake.
“Wananchi watafakari kila.mmoja dhuluma hii na kila.mtu atajua hatua za kuchukua,” alisema Kondo.
Vyama vingine vilivyogombea ni   TADEA kilichopata kura 607, AFP 739, CHAUSTA 362, Demokrasia Makini  264, NRA 238  na NCCR Mageuzi 2,156.
Waandishi wa gazeti hili walitembelea  kituo hicho cha shule ya Majimatitu na kukuta ulinzi ukiwa umeimarishwa na baadhi ya maduka yakiwa yamefunguliwa.
MTANZANIA ilifanya jitihada za kumtafuta mkurugenzi Magimbo   kupata ufafanuzi zaidi wa matokeo hayo lakini  simu yake ilikuwa haipatikani na pia hakuwapo ofisini.

LOWASA APINGA MATOKEO NA KUDAI ANAONEWAALIYEKUWA mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa amepinga matokeo ya urais na kusisitiza kuwa yeye ndiye mshindi halali.
Kutokana na hali hiyo, Lowassa anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutengua matokeo hayo na kumtangaza yeye kuwa mshindi wa nafasi hiyo.
Lowassa aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuwa ushindi wake umepatikana baada ya kukusanya matokeo kutoka katika vituo vya kupigia kura nchi nzima.
“Leo (jana) Oktoba 29, 2015, kupitia mgombea mwenza wangu, Juma Duni Haji nimewasilisha rasmi malalamiko yetu kuhusu mwenendo mzima wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
“Tumeainisha katika malalamiko yetu, kutokuridhishwa kwetu na mwenendo na matukio mbalimbali, hususani, utangazaji wa matokeo batili, yasiyo akisi matokeo halisi yaliyopatikana katika vituo vya kupiga kura.
“Kama tulivyoeleza jana (juzi), takwimu zetu sisi zilionesha nilikua naongoza, tumejiridhisha baada ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu za matokeo nchi nzima.
“Kwa hali hii, ninaitaka NEC initangaze mara moja, mimi Edward Ngoyai Lowassa kuwa mshindi wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” alisema Lowassa.
Hata hivyo Lowassa, aliwashukuru wananchi kwa imani waliyoionyesha kwake kwa kumchagua na kuwaamini yeye na viongozi wenzake.
“Mimi pamoja na viongozi wenzangu, tunaamini kuchezea demokrasia ni kuvunja amani,sote tunatambua, nyie Watanzania ndio mnaoporwa haki yenu ya kupata mabadiliko na viongozi mnaowahitaji…nitaendelea kuwa pamoja na Watanzania wote kudai haki yenu kwa nguvu zote”alisema Lowassa.
Wakati Lowassa akitangaza hatua hiyo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alimtangaza mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk. John Magufuli kuwa mshindi wa nafasi ya urais, baada ya kupata kura 8,882,938 sawa na asilimia 58.46, wakati Lowassa akipata kura 6,072,848 sawa na asilimia  39.97
Mwisho.  

MAGUFULI AKABIDHIWA HATI YA URAIS NA KUWASHUKURU WAKAZI WA DAR

 Rais mteule Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia wakazi wa Dar es Salaam alipokuwa akitoka katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Picha na zote na Humphrey Shao
 Msafara wa Rais Mteule John Pombe Magufuli kuelkea Lumumba katika ofisi ndogo za CCM Mkoa  wa Dar es Salaam
 Rais Jakaya Kikwete akisalaimiana na Rais Mteule John Pombe Magufuli
 Rais Kikwete akihutubia mamia ya wakazi wa jijini Dar es Salaam waliofurika kwa Magufuli
 wanachama wa CCM wakiwa wamekaa barabarani
 Rais Mteule John Pombe Magufuli akihutubia wana CCM katika ofisi ndogo za mkoa wa Dar es Salaam
 Spika wa Bunge Anna Makinda akiwa na Seif Khatibu wakifurahia jambo
 Rais Mteule Dkt JohnMagufuli
 Dkt John Magufuli akiwa na Makamu mteule Samia Suluhu wakionyesha cheti ch
 Asha Baraka
 Mwigulu Nchemba akiteta na Waziri mkuu
 wanachama wakiwa na mabango barabarani

WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WATAKIWA KUWA WAADILIFU

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,Amina Khamis Shaban amesema hakuna sababu yoyote ya T...