Thursday, December 17, 2015

WACHEZAJI WENYE ITC RUKSA TFF


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya marekebisho ya kanuni za usajili ambapo sasa mchezaji ambaye usajili wake utakuwa umepita kwenye mfumo wa mtandao wa Transfer Matching System (TMS) atapewa leseni na kuitumikia moja kwa moja timu yake mpya.


TFF itatoa leseni ya usajili wa mchezaji ambaye amethibitishwa kupitia mtandao wa TMS baada ya kuwepo nyaraka zote; mkataba uliomalizika, barua ya kuvunja mkataba, barua ya kuachwa (release letter), mkataba mpya na uthibitisho wa makubaliano kati ya klabu zinazohusika.


Licha ya mchezaji kupata leseni, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji bado itakuwa na mamlaka ya kushughulia upungufu, malalamiko ya kiusajili, pingamizi na uhalali wa kimkataba kati ya pande mbili (mchezaji na klabu).


Wachezaji wote wa kigeni waliosajiliwa kwa ajili ya kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) wanapaswa kulipiwa dola za kimarekani U$ 2,000 kwa kila mmoja kabla ya kupatiwa leseni na kuanza kuzitumikia klabu zao katika michuano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho.


Pia TFF kupitia kamati ya sheria na hadhi za wachezaji inaweza kumruhusu kwa kipindi maalum mchezaji mwenye dosari acheze kwa leseni ya muda (provisional license) hadi dosari hizo kati ya klabu na klabu zitakapomalizwa. Iwapo dosari hizo hazitakuwa zimemalizwa, mchezaji anaweza kuzuiwa kucheza na klabu husika kuadhibiwa.


Timu zote za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili zinatakiwa kufuatilia TFF kujua wachezaji ambao hawana pingamizi na leseni za wachezaji waliopitishwa wanaweza kuanza kutumika kuanzia kesho tarehe 18/12/2015 na kwenye michezo ya kombe la Shirikisho (FA Cup) kama hawakuwa wamecheza raundi ya kwanza kwenye vilabu vya zamani.


 


 

MOURINHO ATUPIWA VIRAGO RASMI CHELSEAMourinho atupiwa virago Chelsea
LONDON England
CHELSEA hatimaye imefikia uamuzi mgumu kabisa wa kumtimua kocha wao kipenzi, Jose Mourinho ikiwa ni miezi saba tu tangu kocha huyo aimbiwe wimbo wa kishujaa baada ya kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa England.
Uamuzi wa Bodi ya Chelsea umetangazwa jana jioni na umeelezwa kuchangiwa na matokeo mabaya ya timu hiyo katika Ligi Kuu ya England (EPL) msimu huu, ambapo timu hiyo inashika nafasi ya 16 ikiwa na pointi 15 kutokana na michezo 16 iliyocheza.
Kufungwa na vinara wa ligi hiyo Leicester City mabao 2-1 na kuwafanya wawe nyuma kwa pointi 20 nyuma ya timu hiyo, kulimfanya mmiliki wa  Chelsea, Roman Abromovic kuitisha kikao cha bodi ambacho kwa pamoja kilifikia uamuzi mgumu licha ya malalamiko ya kocha huyo aliyoyatoa kwamba anahujumiwa na wachezaji wake.
 

JB AANZA KUUZA FILAMU ZAKE MWENYEWE

 Msanii wa filamu hpa nchini ambaye kazi zake zinapendwa na watu wengi Jacob Stephen (JB) ameamua kuuza filamu zake mwenye licha ya kuwa na mkataba na kampuni ya Steps Entertiemnet .
JB ameanza utaratibu huo kwa kuwashirikisha vijana wa mtaani maharufu kama machinga hili waweze kujikwamuakimaisha na  kutokana hali ngumu kwa sasa.

aliongeza kuwa licha ya filamu zake kuuzwa na Steps bado yeye anuza mkononi na popote pale alipo kwenye gari yake mtu anweza kujipatia filamu hiyo inayokwenda kwa jina la Chungu cha tatu

The top five luxurious hotels in TanzaniaManta Resort, Pemba

At this hotel you will find a paradise. The underwater room is 13 feet under the Indian Ocean; this is the first of its kind in Tanzania and even east Africa. It is the perfect spot to enjoy the underwater paradise of Tanzania, surrounded by the tropical marine environment.


Essque Zalu, Zanzibar

Essque Zalu, is located on the north eastern coast of Indian Ocean, the hotel has the attractive villas and executive suites. It is built with local traditional material on the roof, exquisite gardens and outdoors furniture. The hotel located in Nungwi where Tanzania’s most beautiful beaches are found.Singita sasakwa Lodge, Serengeti
Occupying more than 300,000 acres, the exquisite hotel rooms overlooks the Serengeti national park plains. The lodge was built with incorporated stone walls and verandas. What a perfect moment to enjoy the wildlife!

Park Hyatt, Zanzibar

It’s a perfect way to enjoy the Zanzibar architecture; the hotel gives room for travelers to experience the culture and spectacular views of the oceanfront in the heart of stone town.


Hyatt Regency, Dar es Salaam.
This is the biggest luxurious five star hotels in Tanzania; it provides its guests with views of the Indian Ocean. The hotel featuring 180 spacious and comfortably appointed rooms and suites with authentic hospitality, deluxe amenities and extensive business facilities to meet the needs of all travelers

About Jovago
Jovago.com is an online hotel booking service with offices in Lagos (Nigeria), Nairobi (Kenya), Dakar (Senegal) and Dar es Salaam (Tanzania) founded by Africa Internet Group and has MTN and Millicom as its investors. Jovago.com, Africa’s No.1 booking portal, facilitates the booking process for its users to provide them with the best hotel booking experience with fast, transparent and easy-to-use services. Jovago.com has over 25,000 local hotel listings across Africa and over 200,000 hotels around the world.
BOMOA BOMOA KATIKA BONDE LA KINONDONI MKWAJUNI

 KATAPILA LIKIBOMOA NYUMBA ZA WAKAZI WALIJENGA MABONDENI


WAKAZI WA ENEO HILO WAKIJARIBU KUOKOA VITU VYAO

Tuesday, December 15, 2015

Eng Manyanya Akunwa na Kazi za COSTECH

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Ufundi Eng Stela Manyanya akizungumza na wafanyakazi wa COSTECH
 Dr Mshinda akitoa brief kwa Naibu Waziri
Naibu Waziri wa Elimu akifatilia Presantation kwa maikini

Naibu Waziri Eng Stela Manyanya Aiagaiza bodi ya Mikopo kutoa mikopo yote kwa wanfuzni walioomba

 Mmoja wa Wanfunzi kutoka Chuo cha UDSM Akitoa hoja kwa Waziri
 Binti kutoka Udsm akimueleza namna wanavyonyanyasa kwa kukosa mikopo
 Naibu waziri wa Elimu Sayansi Tekinollojia na  Ufundi Eng Stela Manyanya akizungumza na wanavyuo katika ofisi ya Bodi ya Mikopo

WADAU WA MITINDO NA UREMBO WAALIKWA KUSHIRIKI MAONESHO UCHINA

Makamu wa Rais wa Maonyesho ya Wachina Maharufu kama China International Beauty Expo African Hall,Rex Chan akizungumza na Waanddishi w...