Friday, January 1, 2016

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU.Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence S.Milanzi akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Naibu wakatibu wakuu iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria,Amon Mpanju akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na  Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam


: Makatibu wakuu na Naibu Katibu wakiapa kabla ya kusaini Hati ya Maadili ya Umma mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju wakishuhudia Makatibu wakuu na Naibu Katibu wakiapa kabla ya kusaini Hati ya Maadili ya Umma mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016

Hekalu la Mchungaji Rwakatare Kuvunjwa Jan 5*Wizara ya Maliasili na Utalii yaliwekea alama X

*Hoteli za kitalii nazo zakumbwa bomoabomoa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAZI ya uwekaji alama za X kwenye nyumba zilizojengwa kwenye maeneo yasiyo rasmi imeshika kasi, huku rungu la maofisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii likitua pia katika nyumba inayomilikuwa na Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto la Mikocheni B, Getrude Lwakatare.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuendelea na ubomoaji wa nyumba hizo kuanzia Januari 5, mwaka huu.
Maofisa hao wa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), jana walitua katika nyumba ya Mchungaji Lwakatare na kuweka alama ya X  baada ya kuelezwa kuwa ipo katika eneo la hifadhi ya bahari.
Timu hiyo ilikuwa ikiongozwa na Ofisa Misitu Msaidizi wa Manispaa ya Kinondoni, Issa Juma ambaye aliambatana na watu wanaoweka alama hizo pamoja na askari wa Jeshi la Polisi waliokuwa na mitutu ya bunduki.
Juma alisema nyumba hiyo ya Mchungaji Lwakatare imejengwa kinyume cha sheria kwenye eneo lililokuwa na miti ya mikoko, mita 60 kutoka bahari ya Hindi.
Alisema nyumba hiyo ilijengwa kimakosa ikizingatiwa kuwa eneo hilo kuna kibao kinachoashiria kuwa ni hifadhi ya maliasili na hairuhusiwi kujengwa nyumba ya makazi wala jengo la biashara na mtu au taasisi yoyote.
“Sheria ya misitu namba 14 ya mwaka 2014 inaahinisha wazi kuwa wananchi hawaruhusiwi kujenga maeneo ya hifadhi ya misitu, hivyo nyumba na hoteli zote zilizojengwa usawa huu tutazibomoa zote na hatutaangalia jina la mtu wala nafasi yake,” alisema Juma.

ULINZI KILA KONA
Nyumba hiyo ya Mchungaji Lwakatare iliyowekwa alama ya X ipo kitalu namba moja Mtaa wa Ally Sykes eneo la Kawe Beach.
Maofisa hao walifika eneo hilo saa 8 mchana ambapo waligonga geti na kumkuta mlinzi aliyekuwa akilinda nyumba hiyo ambaye alikiri kuwa inamilikuwa na Mchungaji Lwakatare.
“Ndiyo hii ni nyumba yake, ila suala kuwa anaishi hapa mimi sifahamu na wenyewe hawapo,” alisema mlinzi huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa maofisa hao wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Nyumba hiyo ya kifahari yenye ghorofa moja ilikuwa haionekani kutokana na kuzingirwa na miti iliyopandwa ndani.
MAJUMBA, MAHOTELI KUBOMOLEWA
Mbali ya nyumba ya Mchungaji Lwakatare, maofisa hao walifanikiwa pia kuweka alama ya X kwenye nyumba nyingine na hoteli zaidi ya 30 zilizoko maeneo ya ufukwe wa Bahari ya Hindi.
MTANZANIA ilishudia maofisa hao wakiweka alama hizo kwenye nyumba ambazo nyingine waliweka katika upande mmoja wa ukuta.
Miongoni mwa hoteli zilizokumbwa na hekaheka hiyo ni Seascape ambayo ipo jirani ya Hoteli ya White Sand iliyopo Mtaa wa Mbezi Beach.
Kwa upande wa nyumba zilizowekwa alama ya X ni zile zilizoko maeneo ya fukwe ya bahari katika maeneo ya Jangwani Beach, Kunduchi Beach, Ununio na Kawe.

Katika maeneo ambako nyumba na hoteli zimewekewa X, kulikuwa na tangazo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalotoa angalizo  la kuwataka wananchi kutojenga, lakini baadhi yao walionekana kukaidi na kujenga kwenye eneo hilo.
 “Wizara ya Maliasili na Utalii, Wakala wa Huduma za Misitu, Hifadhi ya Misitu ya Mikoko. Onyo, Eneo hili la hifadhi ya mikoko linalindwa kwa mujibu wa sheria za misitu ya mwaka 2992 na ardhi ya mwaka 1999,” lilisomeka tangazo hilo na kuendelea:
“Hairuhusiwi kufanya shughuli yoyote bila kibali kutoka kwa mamlaka husika, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa atakayekiuka.”
KAULI ZA MAWAZIRI
Hivi karibuni, Waziri  wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Likuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, walisema Serikali itabomoa nyumba zilizoko mabondeni.
Walisema pia itatengua vibali vyote vya ujenzi vilivyotolewa kinyume cha sheria ya ardhi na mazingira.
Mawaziri hao walisema ubomoaji huo utaendelea katika Jiji la Dar es Salaam Januari 5, mwaka huu na kwamba watahakikisha mabonde yote yanakuwa wazi na bonde la Msimbazi litaboreshwa na kuwa eneo maalumu kwa ajili ya kupumzika litakalojulikana kama City Park. 
Walisema Serikali itafanya hivyo bila kujali nafasi na vyeo vya wamiliki na wala haitawaonea aibu watu wote waliojenga kwenye maeneo ya wazi, kingo za mito, fukwe za bahari, ardhi oevu na kwenye hifadhi za barabara kwa kisingizio chochote.
Mawaziri hao walitoa kauli hiyo wakati walipokuwa wakijibu  maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua hatima ya kubomolewa kwa nyumba inayomilikiwa na Mchungaji Lwakatare.
Akizungumzia suala hilo, January alisema awali ubomoaji wa nyumba hiyo ulisitishwa kutokana na kesi iliyofunguliwa mahakamani na mchungaji huyo.
Alisema hata hivyo ana imani kwamba kesi hiyo ikishamalizika sheria ya Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) itatekelezwa ipasavyo.
“Baadhi ya maeneo watu walikimbilia mahakamani kuchelewesha utekelezaji wa sheria, safari hii hatuna mzaha, hakuna mtu mkubwa kuliko Serikali. Hata sheria ya mazingira ina mamlaka na ipo juu ya vibali vyote vilivyotolewa na kama mtu amevunja sheria hiyo ni hasara kwake.
“Bahati mbaya suala la nyumba ya Mama Lwakatare  (mchungaji), wanasheria wa NEMC walishaikatia rufaa mahakamani, shauri hilo likimalizika, nyumba hiyo inaweza kuvunjwa,” alisema January.
Nyumba ya Mchungaji Lwakatare ni miongoni mwa majumba ya kifahari yaliyojengwa kando ya mito ya Mbezi Beach, Mndumbwe na eneo la Hifadhi ya Mikoko jijini Dar es Salaam, ambazo kwa mujibu wa sheria ya NEMC zinatakiwa kubomolewa.
Hata hivyo, mpango wa kubomoa nyumba hiyo inayokadiriwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 1.5 ulikwama kutokana na mahakama kuzuia.
Kwa mujibu wa NEMC, kesi hiyo ilifunguliwa na mmiliki wa nyumba hiyo katika Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi ambapo aliweka pingamizi kuzuia kubomolewa.
Kwa nyakati tofauti, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM), alimtaka aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa, kuzivunja nyumba mbili zilizopo Mbezi Beach zilizojengwa katika fukwe ya Bahari ya Hindi ikiwamo ya mchungaji huyo licha ya kwamba kuna zuio la mahakama.
Bulaya ambaye hivi sasa ni mbunge wa Bunda Mjini kupitia Chadema, alitaja viwanja viwili vyenye namba 2019 na 2020 kikiwamo cha Mchungaji Lwakatare ambaye ni kiongozi wa dini.


TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...