Atakaye Saidia kukamatwa kwa SMG Dar kulamba donge Nono



KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna Simoni Sirro, ameahidi zawadi ya Sh milioni moja kwa atakayetoa siri ya jambazi anayetumia bunduki aina ya SMG kwani silaha hiyo ni hatari.
Kamanda Sirro alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, wakati akizungumza na wakazi wa mtaa wa Nyambwera kata ya Tandika Manispaa yaTemeke katika  mkutano wa uhamasishaji ulinzi shirikishi mtaani hapo.
Alisema kuwa silaha hiyo ni kubwa hivyo yupo tayari kutoa fedha hizo kwa yeyote atakayefichua siri za kuwepo kwa aina hiyo ya silaha.
Pia aliwataka vijana wa mtaa huo kuachana na mambo ya  uhalifu kwasababu  uhalifu una mwisho wake na kuwataka wazazi kuwaonya  watoto wao wanaofanya biashara  za kihalifu na kuwakemea waache mara moja.
“Hakuna mtu anayepata heshima kwaajili ya kazi ya wizi au ujambazi wakati kila mtu anajua mwisho wa wizi ni nini kitachotokea, ni vyema kufanya biashara itakayokupatia kipato halali,” alisema.
Kamanda Sirro ametoa onyo kwa majambazi kuacha mara moja  kazi hiyo  na kama hawataki wataishia mikononi  mwake au kwa vijana wake.
Pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa polisi ili kuwafichua majambazi, vibaka, wauza gongo na madawa ya kulevya ili mtaa huo waishi kwa amani.
Kamanda Sirro pia aliwataka wenyeviti wa mtaa kutimiza wajibu wao na kuhakikisha wananchi  wanaishi kwa amani kwani hiyo ni moja ya kazi yao.
Pia aliwataka wananchi kutoa taarifa endapo wataona kuwa mwenyekiti hatimizi wajibu wao ili waweze kuwachukulia hatua za kisheria kwa ni sasa hivi hapa ni kazi tu.

Post a Comment

Previous Post Next Post