VIfaa vyalikwamisha soko la samaki feri


UBORA wa vifaa na kusahaulika kwa wavuvi nchini kumesababisha soko la samaki kuzidi kudidimia kila kukicha.

Akizungumza jana jijini Dar eš Salaam na Mtanzania , Karibu wa Soko la Feri, Mbaraka Kilima amesema, ukosefu wa zana za kisasa kwa wavuvi hapa nchini ndiyo chanzo cha soko la samaki kushuka.

"Vifaa wanavyotumia wavuvi hapa nchini vingi ni vya mbao havina ubora wala kivutio cha kuweza kuwashawishi samaki kuvuliwa kwa wingi,"alisema Kilima.

Alisema ni wakati sasa kwa wizara husika kuhakikisha inaondoa changamoto zinazowakabili wavuvi ili kuendeleza sekta hiyo muhimu nchini.

"Wakulima wana sera yao kabisa ya kilimo kwanza lako no wavuvi wamesahaulika kabisa hat a mwenzetu wengine wanakopeshwa lakini sekta hii imesahaulika,"alisema Kilima.

Alisema wavuvi wamekuwa wakitozwa ushuru mkubwa lakini hakuna mrejesho wa ushuru huo.

Kilimanjaro alisema sekta ya uvuvi inategemewa na watanzania karibu asilimia 98 ambapo wanajipatia kipato na wengine kufanya chakula.

Kilima alisema wanashangaa serikali imekuwa ikipiga vita uvuvi haramu lakini haina sera ya kuwaendeleza wavuvi nchini.


Post a Comment

Previous Post Next Post