Wednesday, February 17, 2016

Azamu kutumia nguvu ya ziada kumaliza Mbeya City
NA GEORGE KAYALA
BAADA ya kuonja uchungu wa kufungwa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kwa kufungwa na Coastal Union bao 1-0,  timu ya Azam FC imeahidi kutumia nguvu ya ziada kuhakikisha inashinda mchezo wake dhidi ya Mbeya City utakaopigwa kwenye Dimba la Sokoine Jumamosi hii jijini Mbeya.
Akizungumza na BINGWA jana, Katibu Mkuu wa timu hiyo, Nassoro Idrisa alisema kwamba uongozi wote, bendi la ufundi na wachezaji wanatambua wanawakati mgumu wa kushinda michezo ya ugenini hivyo watapambana kadiri wawezavyo ili washinde mchezo huo.
“Tunakabiliwa na mchezo mgumu mbele yetu kwani timu inapokuwa nyumbani huwa ina nafasi kubwa ya kupoteza mchezo, ila tutatumia nguvu ya ziada kuhakikisha tunashinda ili yasitokee yaliyotukuta Tanga kwa kufungwa bao 1-0 na Coastal Union,” alisema Idrisa.
Bila kutaja ni nguvu gani watakayoitumia, katibu huyo alisema timu ambayo imeweka kambi Chamazi jijini Dar es Salaam itaondoka Ijumaa kuelekea Mbeya ikiwa na itaingia uwanjani kwa tahadhali kubwa.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliocheza Azam Complex September 27 mwaka jana Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Wafungaji wa magoli ya Azam walikuwa ni  Mudathir Yahaya na Kipre Tchetche huku Mbeya City likiwekwa kimiani na Raphael Alpha.

No comments:

Post a Comment

Waziri Dk Kigwangalla ataka wavamizi maeneo yaliyohifadhiwa kuondoka

Mwandishi wetu,Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amewataka wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi nchini,...