Ben Pol: Sitauchora ‘tattoo’ mwili wangu kamwe


MSANII wa Bongo Fleva, Benard Paul ‘Ben Paul’, amesema  hapendi na hatauchora ‘tattoo’ mwili wake kama baadhi ya wasanii na watu maarufu wafanyavyo kwa kuwa anauheshimu sana.
Ben Paul alisema imekuwa ni kawaida kwa idadi kubwa ya wasanii kujichora ‘tattoo’ na kuwa na mwonekano wa tofauti na watu wengine, lakini kwake jambo hilo halina nafasi.
“Japo ni msanii lakini sipendi kuwa na mwonekano wa tofauti kama kufuga rasta, kuvaa hereni au kujichora mwilini kwa sababu nauheshimu mwili wangu, ndiyo maana nipo kawaida kila wakati,” alifafanua.

Post a Comment

Previous Post Next Post