Wednesday, February 17, 2016

Jux: Nilianza kuwa star kabla ya Vanessa


Na Mwandishiwetu
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Juma Musa ‘Jux’ amesema alianza kupata umaarufu kabla ya mpenzi wake Vanessa Mdee hivyo si sahihi kusema anatembelea nyota ya mrembo huyo kwenye muziki.
Akizungumza na MTANZANIA, Jux alisema kama alikuwa anataka kufahamika kupitia Vanessa basi wangeshafanya fanya wimbo kwa sababu hivi sasa wapo karibu zaidi.
“Nilianza kupata umaarufu kabla ya Vannesa, sipendi watu watafute maneno kupitia uhusiano wetu ndiyo maana hata kwenye maonyesho au mahijiano ni ngumu sana kutuona pamoja,” anasema Jux.
Aliongeza kuwa anavutiwa na Vanessakwa sababu anajituma na ana mpa changamoto ya kutafuta mafanikio kila siku ndiyo maana anamuona ni mwanamke bora kwake.


No comments:

Post a Comment

M-KOPA YAFUNGA UMEME JUA WENYE THAMANI YA Tshs 4,959,000. KATIKA SHULE YA SEKONDARI MWINYI MKURANGA PWANI

 Meneja Msaidizi wa M-Kopa nchini , June Muli akikabidhi boksi la Vifaa vya umeme wa jua kma ishara ya makabidhiano ya mradi wa umeme uli...