Kayala aja na Maajabu ya Damu ya Yesu




MKALI wa nyimbo za injili nchini, George Kayala amekamilisha albamu yake ya pili aliyoipa jina la Maajabu ya Damu ya Yesu ikiwa katika mfumo wa CD ikiwa na nyimbo saba ambazo amedai zina nguvu ya ajabu na zitafanyika msaada kwa kila atakayezisikiliza.
Akizungumza na mtandano huu leo, Kayala alisema kwamba hii ni albamu ya pili baada ya ile ya kwanza iliyojulikana kwa jina la Siwema na amewataka mashabiki wake kujiandaa kupata nakala halisi na si kununua feki.
“Nimekamilisha albamu ya pili itwayo Maajabu ya Damu ya Yesu ikiwa katika mfumo wa CD ikiwa na nyimbo saba ambazo ni Maajabu ya Damu ya Yesu, Kanitendea Mema, Fungua Njia, Dhihirisha Uwaza Wako, Wastahili Sifa, Umenikumbuka na Tanzania,” alisema Kayala.
Mwimbaji huyo alisema kwa sasa anafanya maandalizi ya kurekodi video yake na huenda zoezi likaanza mwishoni mwa mwezi huu ama mwanzoni mwa mwezi wa tatu huku akiwataka wapenzi wote wa muziki kumuunga mkono kwa kununua kazi zake ili apate fedha ya kurekodia video hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post