LIGI KUU MZUNGUKO WA 20 WIKIENDI HII KWA KUZIKUTANISHA SIMBA NA YANGA

Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea wikiendi hii mzunguko wa 20 kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali huku Jumamosi michezo mitano ikichezwa kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu katika ligi hiyo.
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Yanga SC v Simba SC watakua wakichuana kusaka uongozi wa Ligi hiyo katika mchezo namba 153, huku Mgambo Shooting wakiwakaribisha Tanzania Prisons katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Wagonga Nyundo wa jiji la Mbeya, Mbeya City watawakaribisha Azam FC katika uwanja wa Sokoine mjini humi, mjini Shinyanga chama la wana Stand United watawakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Kambarage, huku Toto Africans wakicheza dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Jumapili Ndanda FC watakua wenyeji wa African Sports uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, Mwadui FC watakua wenyeji wa Coastal Union uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga, huku wana lizombe Majimaji FC wakicheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Post a Comment

Previous Post Next Post