Tuesday, February 23, 2016

Wapinzani wa Yanga Afrika kutua keshoWAPINZANI wa Yanga, klabu ya Cercle de Joachim ya Mauritius, wanatarajia kuwasili nchini kesho kwa ajili ya pambano lao la marudiano dhidi ya miamba hiyo ya Jangwani litakalopigwa Februari 27, mwaka huu, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo, Cercle wanatarajia kuwasili nchini mapema siku ya Jumatano kwa ajili ya kupata muda zaidi wa kuzoea mazingira na hali ya hewa ya joto hapa nchini.
Tayari kocha wa timu hiyo, Abdel Kacem, amesema hana uhakika wa timu yake kupata matokeo mazuri kuelekea katika pambano hilo la marudiano, ukizingatia watakuwa wakicheza wakiwa ugenini.
Yanga ilianza vizuri kampeni yake ya kuwania ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuibamiza Cercle kwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa raundi ya awali ya michuano hiyo uliochezwa Uwanja wa Stade George V, mjini Port Louis.
Kuelekea katika pambano hilo la marudiano, tayari vijana wa Yanga wameingia kambini leo kujiandaa na mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mkali na wa kuvutia.
Yanga wapo katika mikakati kabambe ya kuhakikisha msimu huu wanafanya kweli kuelekea katika kutimiza malengo yao ya kufika mbali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

M-KOPA YAFUNGA UMEME JUA WENYE THAMANI YA Tshs 4,959,000. KATIKA SHULE YA SEKONDARI MWINYI MKURANGA PWANI

 Meneja Msaidizi wa M-Kopa nchini , June Muli akikabidhi boksi la Vifaa vya umeme wa jua kma ishara ya makabidhiano ya mradi wa umeme uli...