Friday, March 11, 2016

Kayala azidi kujitanua kwa mashabiki wakeMWIMBAJI wa nyimbo za injili nchini, George Kayala amezidi kujitanua kwa mashabiki wake baada ya kuanzisha ‘group’ maalumu la whatsapp linaowahusisha wale wote walioguswa na albamu yake mpya ya Maajabu ya Damu ya Yesu.
Akizungumza na jijiletu  jana, Kayala alisema kwamba watu wengi wameguswa na nyimbo zilizomo ndani ya albamu hiyo na ili kuhakikisha anajenga mahusiano mazuri nao ndipo akaanzisha group hilo alililolipa jina la Maombi ni Silaha.
“Nimelazimika kutoa nyimbo zangu bure kwa mashabiki wangu ndani na nje ya nchi kwa njia ya whatsapp na wengi wameguswa na vibao hivyo, na ili nisiwapoteze ndipo nikaamua kuunda group hili ambalo pia linatumika kwa kuombea mahitaji mbalimbali ya wadau hao,” alisema Kayala.
Kayala alisema kwamba mashabiki wake wengi amewapata kwa njia ya facebook ambako amekuwa akiwajulisha nini kinachoendelea juu ya huduma yake hii ya uimbaji.

No comments:

Post a Comment

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...