Tuesday, March 15, 2016

NAGU ASEMA TATIZO LA MAJI DAR KUMALIZIKA MAY MWAKA HUUMwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Kilimo Mifugo na Maji, Dk. Mary Nagu akizungumza na waandishi wa habari juu ya utaratibu wa upatikanaji  wa maji jijini Dar es Salaam.Picha na Humphrey Shao.Mweneyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Kilimo Chakula na Maji , Dk. Mary Nagu, amesema kuwa wakazi wa Dar es Salaam watapata maji kwa asilimia 100 ifikapo mwezi wa tano mwaka huu.

Dk Nagu alisema hayo jana alipkuwa akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kuzungumza na wizara ya maji juu ya mipango yao ya kuleta maji jijini Dar es Salaam.

"Rais amesema kuwa anataka nchi hii kuwa ya Viwanda nasi tumewaita watu wa Wizara ya Maji watueleze ni namna gani wanaweza kutatua tatizo la maji katika jiji la Dar es Salaam nao wameahaidi kufikia mwezi watano watakuwa wamemaliza tatizo kwa kuakamilisha mradi wa bwawa la kidunda, Visima 20 Kisarawe 2 na maradi wa maji wa Ruvu chini" anasema Nagu 

alimaliza kwa kusema kuwa wananchi wanaimani kubwa na serikali ya magaufuli hivyo wao kama wao wamejipanga kuahkikisha kuwa  wanaisimamia Dawasco na Dawasa kuakikisha kuwa zinatoa huduma muhimu hapa mjini.No comments:

Post a Comment

Waziri Dk Kigwangalla ataka wavamizi maeneo yaliyohifadhiwa kuondoka

Mwandishi wetu,Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amewataka wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi nchini,...