Tuesday, March 15, 2016

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hii leo tumetembelea kiwanda cha Sukari Kagera

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hii leo tumetembelea kiwanda cha sukari cha KAGERA SUGAR,tumetembelea na kukagua ranchi za Taifa za misenyi na kagera zilizopo mpakani mwa nchi jirani.
Uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda cha Kagera unaongezeka,na tunakwenda kuvipatia nguvu viwanda vya ndani kwa kuondoa kodi zisizokuwa na tija kwenye uzalishaji wa sukari ili viwanda vizalishe sukari ya kutosha.
Kwenye ranchi za Taifa zinazozunguka mkoa wa Kagera na mikaoa mingine zinakwenda kupitiwa upya na wataalamu wameshaanza kazi hiyo,lengo ni kuhakikisha watanzania wananufaika na ranchi hizi,kwa wawekezaji waliohodhi block kwenye ranchi hizi bila kuziendeleza muda wao umefika wa kuondoka kwenye maeneo hayo kabla hatua zingine za kisheria hazijachukuliwa.
Watanzania wanauhitaji wa maeneo ya shughuli za kiuchumi,baadhi ya maeneo yaliyotengwa kwa muda mrefu bila kuendelezwa yanakwenda kutazamwa upya ili ugawaji upya uchukue nafasi na maeneo hayo yatumike kwa uzalishaji,


No comments:

Post a Comment

M-KOPA YAFUNGA UMEME JUA WENYE THAMANI YA Tshs 4,959,000. KATIKA SHULE YA SEKONDARI MWINYI MKURANGA PWANI

 Meneja Msaidizi wa M-Kopa nchini , June Muli akikabidhi boksi la Vifaa vya umeme wa jua kma ishara ya makabidhiano ya mradi wa umeme uli...