KHADIJA KOPA;RUNINGA ZIMESHUSHA MUZIKIWA TAARABU



Malkia wa muziki wa Taarab nchini Khadija Kopa amesema sababu ambayo inasababisha  soko la muziki wa taarab kushuka na kutochezwa kwa wingi kwenye radio na ruringa ni moja ya sababu kubwa inayoifanya  kuanguka kwa muziki huo, pia wasanii wa taarab kutokwenda na wakati kuwa  mbunifu zaidi kwenye utunzi wa nyimbo.
Akizungumza na MTANZANIA  amesema  kuwa  kwa sasa muziki wa Bongo fleva ndio umeshika nafasi ya kuwa juu kuliko muziki wa taarab na sababu kubwa ni vyombo vya habari na wasanii wa taarab kutokujituma zaidi kwenye utunzi wa mashairi na kujua mashabiki wanataka nini kwa wataki huu.
“Muziki wa taarab unashuka kwa sababu ya vyombo vya habari kuwapapromo zaidi muziki wa kizazi kipya ukwel muziki wa taarab bila vyombo  vya habari hatuwezi kufika popote, hapa tulipofikia sisi wengine mpaka tunazeeka ni nguvu za vyombo za habari bila waotusingefika hapa tulipo sasa,” alisema Khadija Kopa.
Aliongezea na kusema kuwa anaomba serikali kuwasaidia kuwashika watu wanaonakili kazi zao na kuzipiga kwenye masherehe mbalimbali huku wao kukosa show.

Post a Comment

Previous Post Next Post