Mungai; Ajiuzuru Uenyekiti wa bodi TATEPA



Na Humphrey  Shao, Dar es Salaam

Aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Uzalishaji wa Chai na Kusafirisha maparachichi, Joseph Mungai, ametangaza kujiuzuru katika nafasi hiyo kutokana na Umri wake kuwa mkubwa.

Mungai ambae aliwaeleza wajumbe wa mkutano mkuu wa wamiliki wa Hisa katika kampuni hiyo kuwa ana kila sababu ya kufurahia hata matokeo mazuri yaliyo ongezeka lakini lazima aachie ngazi.
“nachukua fursa hii kuwashukuru wakurugenzi wenzangu  wa  zamani na wasasa aidha kwa menjimenti zao na wafanyakazi wote katika miaka 22,aidha nawashukuru sasa waliomo katika nafasi hizo kwa juhudi na kujituma kwao katika mwaka uliopita ambao ulikuwa tena wa changamoto kubwa hata hivyo naachia ngazi wakati nimeanza kuona mwanga mwishoni mwa taluma la hasara ya miaka ya hivi karibuni “ alisema Mungai.

Alimaliza kwa kusema kuwa mafanikio ya kundi la TATEPA Limited yanategemea mafunzo ya wakulima wadogo  kwa kuendelea kuwekeza na kukuza ujuzi wao kwa kuwatafutia mitaji na pembejeo.

 Joseph Munga akizungumza na wajumbe wa mkutano mku kabla ya kuachia ngazi katika nafasi ya uenyekiti wa Bodi.

 Joseph Munga akizungumza na wajumbe wa mkutano mku kabla ya kuachia ngazi katika nafasi ya uenyekiti wa Bodi.
 Joseph Mungai akimkabidhi  ndugu George Theobald cheti cha utumishi uliotukuka
 George Theobaldakionyesha cheti juu

Post a Comment

Previous Post Next Post