MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond’, jana
amelisimamisha Bunge baada ya kutambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuwa
ni moja ya wageni waliohudhuria bungeni.
Diamond ambaye alikuwa ameambata na wageni wake kutoka
kundi la Mafiki Zolo la nchini Afrika Kusini, baada ya kutambulishwa wabunge
walishindwa kuzuia hisia zao na kujikuta wakimshangilia kwa nguvu mwanamuzi
huyo.
Wasanii hao ambao waliingia bungeni kwa mwaliko wa Waziri
wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye.
“Waheshimiwa wabunge kuna tangazo la wageni hapa, leo
tumetembelewa na wageni mashuhuri humu ndani, sio wengine ni wanamuziki wa
kundi la Mafikizolo.
“Lakini hawa wameongozana na mwenyeji wao, kijana wetu
anayeitangaza nchi huko duniani, wapo na Nasib Abdul au Diamond,” alisema Spika
Ndugai
Spika alisema kwamba mbali na wasanii hao pia Diamond
amekuja na Meneja wake Babu Tale.
Baada ya tangazo hilo, ukumbi wa Bunge ulilipuka kwa furaha
baada ya wabunge, wageni na waandishi wa habari waliokuwepo ukumbini hapo kugeuka
upande aliokuwepo mwanamuziki huyo ili wamuone.
Nderemo hizo zilidumu kwa dakika mbili hali iliyosababisha baadhi
ya shughuli za Bunge sitishwa kwa muda huku waziri Nape akicheka na kushangilia.
“Ujio huu wa Diamond unatoa hamasa kwamba kuna kitu leo
jioni kinafanyika, tunaomba waziri wa habari atutaarifu ili tujumuike pamoja,”
alisema Spika Ndugai.
Baada ya maelezo hayo Bunge liliendelea na shughuli zake
ambapo wabunge walikuwa wakichangia hoja kwenye Hotuba ya bajeti