NGOs ITAKAZOGAWIA MASHOGA KY JELLY KUFUTIWA USAJILI


http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2016/07/Ummy-Mwalimu1.jpgMASHIRIKA yasiyo ya kiserikali (NGOs) ambayo yatabainika kuwa yanaendelea na miradi ya kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja nchini yatafutiwa usajili wake.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (Pichani) aliandika hivyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa ‘facebook’ na kusisitiza kuwa serikali italisimamia kikamilifu suala hilo.
“Sijapiga marufuku  matumizi ya vilainishi. Ukweli, Nimepiga marufuku mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kununua na kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi na wanaume wenzao. Sababu nimeshazieleza,” aliandika.
Aliongeza “Na nafurahi kuwajulisha kuwa tayari baadhi ya Mashirika hayo yameanza kutekeleza agizo hili kwa kuanza kuondoa vilainishi kwenye miradi yao. Nayapongeza sana. Niendelee kuyataka mashirika mengine kutii agizo hili ambalo tutalisimamia kikamilifu.
“Serikali haitasita kuchukua hatua ikiwemo kuyafutia usajili mashirika yanayoendelea na miradi ya kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja,” alisisitiza.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjbpuEeG2bzTlKcNcRwNGxrVLZVskwiX3XAC_jRbStnGKGobvs3YKYj2YrY1RM4uWn2DUyfVep6bQLZpETKLq_I4-ccwRVYe7h_lyci-ORlpA3JP5FvItlla2W8HUPZL_wWpRyNZEycYpQ/s1600/ky.jpg 
Aliyataka mashirika hayo kushirikiana na serikali kupambana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kujikita kwenye afua nyingine zinazozingatia sheria za nchi sambamba na mila na desturi zetu watanzania.
Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni, Waziri Ummy alisema serikali imechukua uamuzi huo kwani matumizi ya vilainishi hivyo yanachochea kuongezeka kwa vitendo vya ushoga ambavyo ni kinyume cha sheria za nchi.
“Lengo pia ni kudhibiti maambukizi ya VVU kwa sababu katika   wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, asilimia 23 tayari wana maambukizi hayo.
“Tumebaini baadhi ya wadau wanaotekelezeka shughuli za makundi maalum wamekuwa wakikiuka taratibu za  utendaji na kusambaza vilanishi hivyo. Katika nchi yetu hakuna  sheria inayoruhusu uhusiano wa jinsia moja na kuendelea kusambaza vilainishi hivyo ni kama kuhalalisha vitendo hivyo. Mila na desturi zetu haziruhusu uhusiano huo,” alisema.

Post a Comment

Previous Post Next Post