EU yatoa msaada wa Bil 25/- kwa NBS

OFISI ya Taifa ya Twakimu (NBS), imepokea msaada wa Sh bilioni 25 kutoka Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kusaidia kuboresha tasnia ya takwimu kuhusu haki za watoto nchini.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Umaskini wa Watoto wa Tanzania Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, amesema wamepokea msaada huo kwa nia ya kuendeleza tasnia ya takwimu nchini na kusaidia malengo ya nchi ya miaka mitano.
“Tumepokea msaada huu kwa furaha na hamasa kubwa katika kufikia lengo letu la kuboresha na kukuza tasnia ya takwimu nchini ili kuweza kupata taarifa muhimu kwa ajili ya maendeleo ya miaka mitano ya nchi yetu,".http://habarileo.co.tz/images/Frequent/ashatu-Kijaji.jpg
Amesema, wizara yake imewapa kipaumbele watoto kwa kutenga Sh bilioni 18 kila mwezi ili kuwasaidia katika mambo  muhimu ya kila siku hususani elimu bora, makazi na malazi.
Pamoja na hali hiyo Dk. Ashatu amezishukuru nchi za Umoja wa Ulaya kwa msaada huo na kuwataka wasichoke kuwa nao pamoja katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.
Kwa upande wa Mwakilishi wa Balozi wa Umoja wa Ulaya Eric Beaume, amesema msaada huo sio mwisho wao kwani wanapenda kazi ya NBS na matokeo yake hivyo wapo tayari kutoa kiasi kikubwa zaidi ili kuwezesha tume hiyo kutoa takwimu zenye uhakika kwa maendeleo ya Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post