PLIJM AFUKUZA WAANDISHI KATIKA MAZOEZI YA YANGA

 KOCHA wa Yanga, Hans van der Pluijm, ameonekana kuchukizwa na tabia ya waandishi wa habari kufika katika mazoezi ya timu hiyo mara baada ya kuamuru Polisi kuwazui wapiga picha wasufanye kazi yao wakati wa timu hiyo ilipokuwa ikifanya mazoezi katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam .

hali hiyo imemkuta kocha huyo mara baada ya kupata  matokeo mabaya  katika michezo mitatu ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo  alitumia zaidi ya saa moja kuwaweka kitimoto wachezaji wake kabla ya kuanza mazoezi.
Pluijm na msaidizi wake, Juma Mwambusi, waliwasili katika Uwanja wa Gymkhana uliopo Posta jijini saa mbili asubuhi kwa ajili ya kuendelea na programu ya mazoezi kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.



Post a Comment

Previous Post Next Post