Serebuka Festival 2016 kutikisa Dar

WAKAZI wa Dar es Salaam wanatarajia kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali nchini, kwenye tamasha la ‘Serebuka Festival 2016’ ikiwa ni sherehe ya maadhimisho ya miaka miwili ya chaneli ya Startimes Swahili inayoruka kupitia king’amuzi cha Startimes.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhM6MNpNAmCIBqDaTKciULno404V7kQ63a1kQBgpA9RiOqGcaTmUMuc_7GYCT0xnJsbY0ZohpA7Fp_uxGKMQ2eFreQszr7M-uydLYzFb2cjglEo4lZonp5Y-WiNhCACMaBtAV4oxK0Uo6s/s640/pic_0002566.JPG
Lady Jay dee

Msemaji wa kampuni ya Blueline Advertisement Company, ambao ni wadhamini Wakuu wa tamasha hilo, Leonard Mtabuzi, amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama kupata burudani kutoka kwa wasanii wao wakali kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 12 jioni.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg5dP-m5SlOiwuAnIKj1J2WswWi-BQAOGWbx33vQe4EMpa_Kux2FgzEWDuxB3I6srHXnZNQuqPblkJFp8hiHXjIhGXZdJsihzM3dXP1tD1xtvuuvpF49nI6F9NspVRVcgC2mgPUCLGrixtv/s640/2alikiba-1.jpg
Alikiba
“Kama ilivyo  kawaida yetu kuwapa raha watanzania, kesho wasanii mbalimbali kama vile Ali Kiba, Lady Jay Dee, Yamoto Band, Shaa, Jokate, Madee, Snura, Stamina na Juma Nature watatikisa Jiji hili kwa burudani ya nguvu, huivyo tunatarajia k,uona wikendi hii ikiwa ya furaha kwa wanadar es salaam,”amesema Leonard Mtabuzi.
http://www.timesfm.co.tz/wp-content/uploads/2015/07/Juma-Nature.jpg
Juma Nature
Mtabuz, pia amesema kuwa kampuni ya, Blueline Advertisement Company ina lengo ya kuhakikisha kuwa inakata kiu ya wapenzi wa burudani kupitia tamasha hilo hivyo ndiyomaana wamejipanga vilivyo kwa kuwashirikisha wasaanii wote mahili nchini.
Pia ameongeza kuwa wasanii wapo tayari kuhakikisha kuwa wanatoa burudani kwa watanzania wote katika kuhakikisha kuwa wanasherekea miaka miwili ya kisimbusi cha StarTimes.

Post a Comment

Previous Post Next Post