TAZARA WACHANGIA DAMU WAKIADHIMISHA MIAKA 40 YA UWEPO WAO

Zoezi la uchangiaji Damu likiendelea katika makao makuu ya TAZARA ambapo wafanyakazi mbalimbali wa Shirika hilo na watanzania wengine wamejitokeza kucnagia damu 
 Wakati Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia TAZARA wakiadhimisha miaka 40 ya uwepo wake nchini Tanzania maadhimisho hayo yameenda sambamba na zoezi maalum la kuchangia damu zoezi ambalo limefanyika makao makuu ya TAZARA Dar es salaam Tanzania ambapo wafanyakazi wake wameitumia siku ya leo kuchangia damu zoezi ambalo liliongozwa na mpango wa Taifa wa damu salama Tanzania.

Akizungumza na wanahabari wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU amesema kutokana na uhitaji mkubwa wa Damu uliopo Tanzania wao kama TAZARA wameamua kusitisha shughuli za leo kwa ajili ya kufanya zoezi moja la kuchagia damu zoezi ambalo linaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 40  ya kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU akizngumza na wanahabari wakati wakiendelea na zoezi la ucnagiaji wa Damu 

Amesema kuwa zoezi hilo linaonyesha ni jinsi gani wafanyakazi wa TAZARA wamekuwa wakiguswa na maswala mbalimbali ya kijamii hususani swala la ukosefu wa Damu mahospitalini huku akiyataka mashirika mengine na watu mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachangia damu mara kwa mara wawezavyo kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania wamaopoteza maisha yao kwa kukosa Damu.


Aidha mmoja kati ya wahamashishaji kutoka mpango wa taifa wa Damu salama Tanzania Bi Mariam Juma amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhitaji mkubwa damu kutokana na kuongezeka kwa maswala mbalimbali yakiwemo ya ajali,vifo vya mama na watoto wakati wa kujifungua wanaofariki kwa kukosa damu,na magonjwa mengine mengi hivyo akawataka watanzania kujitahidi na kuhakikisha kuwa angalau wanachangia damu kwa mwaka japo mara mbili ili kuokoa maisha ya watanzania wenzao.

Mmoja kati ya wahamashishaji kutoka mpango wa Taifa wa Damu salama Tanzania Bi Mariam Juma akifafanua jambo juu ya umuhimu wa kucnagia Damu kwa watanzania

Mwandishi wa mtandao huu wa HABARI24 BLOG alishughudia wafanyakazi wa TAZARA wakijitokeza kwa wingi kuchangia Damu ambapo walimueleza mwandishi wetu kuwa ni swala la kizalendo na utu kwa mtanzania kujali na kusaidia watanzania wengine ambao wana uhitaji mkubwa wa damu nchini.PICHA ZAIDI ZIPO CHINI HAPA



Post a Comment

Previous Post Next Post