KAMPUNI YA YARA TANZANIA YAZINDUA RASMI USAFIRISHAJI WA MBOLEA KWA NJIA YA TRENI (YARA TANZANIA launches COMPANY OFFICIAL EXPORT OF MANURE through the train)

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Usafirishaji wa mbolea kwa njia ya Reli TRL, Uzinduzi huo umefanyika leo kwenye Ofisi za YARA Tanzania zilizopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRL, Focus Makoye Sahani.

 Azungumzia uzinduzi huo Mkurugenzi huyo alisema kuwa YARA kwa kushirikiana na TRL na SAGCOT, wameamua kuzindua njia hiyo ya usafirishaji ili kupunguza gharama za usafirishaji kwa kutumia barabara na maji ili kuwafikia walengwa kwa wakati na kwa gharama nafuu, ambapo awali kusafirisha Tani moja kutoka Viwandani Ulaya hadi jijini Dar es Salaam, ilikuwa ni Dola za Kimarekani 40, kwa Tani moja na Dar es Salaam hadi Tabora ni Dola za Kimarekani 100 kwa Tani moja kwa njia ya barabara. 

Aidha  Macedo, alisema kuwa kuamua kutumia usafiri wa Treni sasa usafiri utashuka kwa asilimia 35.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo (katikati) Naibu Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRL, Focus Makoye Sahani (kushoto) na Mratibu wa Program ya SAGCOT Centre, Emmanuely Lyimo, kwa pamoja wakionyesha ushirikiano kwa kushikana mikono kuashiria uzinduzi rasmi wa Usafirishaji wa mbolea kwa njia ya Reli TRL uliofanyika leo kwenye Ofisi za YARA Tanzania zilizopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo (katikati) Naibu Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRL, Focus Makoye Sahani (kushoto) na Mratibu wa Program ya SAGCOT Centre, Emmanuely Lyimo (wa pili kulia) na Afisa Habari wa YARA Tanzania, Lynda Byaba (kulia), kwa pamoja wakionyesha ushirikiano kwa kushikana mikono kuashiria uzinduzi rasmi wa Usafirishaji wa mbolea kwa njia ya Reli TRL uliofanyika leo kwenye Ofisi za YARA Tanzania zilizopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Mafoto Blog
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo (aliyenyoosha mkono) akiwaonyesha baadhi ya waandishi wa habari maeneo mbalimbali ya Ofisi kwao wakati walipotembelea kwenye uzinduzi wa usafirishaji kwa njia ya Treni uliofanyika leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo, akionyesha jinsi mbolea inavyopakiliwa kwenye Mabehewa kabla ya kusafirishwa.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya YARA wakipakia mifuko ya Mbolea kwenye Mabehewa tayari kwa kusafirishwa.

Wafanyakazi wa Kampuni ya YARA wakipakia mifuko ya Mbolea kwenye Mabehewa tayari kwa kusafirishwa.
 Bw. Macedo akipanda kwenye Injini ya Treni kuashiria uzinduzi huo leo.
 Bw. Macedo akipanda kwenye Injini ya Treni kuashiria uzinduzi huo leo.
 Mifuko ya Mbolea ikiwa tayari kupakiwa kwenya magari ili kusogezwa eneo la kupakilia kwenye Mabehewa ya Treni
 Wafanyakazi wa YARA wakijiandaa kushusha katika magari na kupakia kwenye Mabehewa.
 Mabehewa yakisubiri kupakiliwa.....
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo, Naibu Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRL, Focus Makoye Sahani wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanahabari waliotembelea Ofisi hizo leo wakati wa uzinduzi huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post