Choki kufanya Tamasha la miaka 30 ya muziki Novemba 26

Msemaji wa mwanamuziki,Ally Choki na Mwandishi wa kitabu cha Maisha ya Ally Choki,Juma Kasesa akizungumziankwa kifupi juu ya kitabu hicho.

Mwanamuziki wa muziki wa Dansi nchini Ally Choki, akionyesha mfano wa kava la kitabu kinachozungumzia maisha yake ya Muziki.
 Mwanamuziki mkongwe Komandoo Hamza Kalala ,akizungumza na waandishi wa habari juu ya maisha ya choki alipokuwa Bantu Group.

Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Dansi hapa nchini , Ally Choki, anataraji kufanya Tamasha kubwa la kutimiza miaka 30 ya muziki na kuzindua kitabu chake katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni Novemba 26.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo choki amesema kuwa siku ya Onesho hilo watu watapata fursa ya kujinunulia kitabu hicho kinachozungumzia maisha yangu yote ya muziki .

"Siku hiyo  tutakuwa na wanamuziki wakongwe wengi kama mzee Zahir Ally Zoro , Hamza Kalala na wengine wengi ni moja ya watu ninao ingia nao kambini kwa ajili ya shoo hii ya iana yake ambayo inandika historia katika muziki wa Dansi hapa nchini"amesema Ally Choki.

Amemaliza kwa kusema kuwa anawaomba watu watu wajitokeze kwa wingi kwani kingilio ni shilingi 15'000/- kwa kila mmoja .

Post a Comment

Previous Post Next Post