SERIKALI
kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ifikapo Machi 30 mwaka huu itawafunguli mashitaka na
kuwapeleka mahakamani wazazi na walezi
wote watakao shindwa kutimiza wajibu wao wa kupeleka watoto shuleni ili kupata elimu ya msingi na sekondari kwa
mwaka 2016.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salama Waziri wa Afya
,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto , Ummy Mwalimu,alisema
sheria ya mtoto namba 2 ya mwaka 2009 kifungu cha 8 kinaelekeza kuwa ni wajibu wa
mzazi kuhakikisha mtoto anapata elimu.
Alisema
elimu ndio njia bora ya kuwajengea watoto
msingi imara wa maisha yao ya badae.
“Natoa
rai kwa wazazi na walezi wote kuhakikisha kuwa watoto wote wanaendelea na masomo endapo wazazi
na walezi hawatatekeleza hilo serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria ambao watazembea , kumficha , kumtorosha na kuzuia mtoto kuanza masomo
sheria itafuata mkondo wake,”alisema Ummy.
Alisema
viongozi na Watendaji wa mikoa , Halmashauri
Maofisa maendeleo ya jamii
na kata watekeleze majukumu yao
ya kuhamasisha jamii ipasavyo juu
ya watoto kujiunga na darasa la
kwanza na kidato cha kwanza kwa mwaka
huu.
Ummy
alisema hakikisheni kuwa agenda yao kubwa katika kazi zao kwa mwezi wa Januari na Februari iwe ni kuhamasisha
wazazi na walezi kupeka watoto wenye
sifa za kujiunga shule ya msingi na sekondari,pia nitahitaji
nipate taarifa ya utekelezaji wa jambo hilo mishoni mwa Februari mwaka huu.
Aidha
aliwataka watu wenye tabia
ya kwaajili watoto walio chini ya
umiri wa miaka 18 kuacha haraka iwezekanavyo kabla oparesheni ya
kutokomeza familia kwa familia haijaanza wakibainika watapelekwa mahakamani.