Wednesday, January 13, 2016

Lukuvi aagiza Ghorofa libomolewe ndani ya Mwezi mmoja


  
 Waziri Lukuvi Akizungumza na watendaji wa BagamoyoNa  Humphrey Shao, Dar es Salaam
WAZIRI wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Shirika la Nyumba la Taifa kuwa wanabomoa jengo refu lilijengwa chini ya viwango katika mtaa wa Indiraghandi ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa.
Lukuvi alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa katika ziara fupi ya eneo hilo na Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani nakubaini matatizo mbalimbali katika sekta  ya Ardhi.
“Miezi sita iliyopita Rais Mstaafu alikuja hapa akaagiza jengo hili libomolewe na nyie mkajiridhisha kweli lafaa kubomolewa sasa inakuwaje mpaka leo linaendelea kuwepo, hivyo naagiza mfanye haraka jengo hili ndani ya mwezi mmoja taratibu za ubomoaji ziwe zimeanza hili kulinusuru taifa kuingia katika janaga jingine.”alisema Waziri Lukuvi.
Wkati huo huo waziri Lukuvi alifanya ziara ya katika Wilaya ya Bagamoyo upotevu wa viwanja 1000 vya wanachi ambavyo walitakiwa kupewa katika eneo la ukuni ambapo vimetoweka katika mazingira ya kutatanisha.
Mara baada ya kupata taharifa hiyo mmoja wa wakazi wa bagamoyo ambaye alitoa malalamiko juu ya viwanja hivyo mbele ya mkutano wa hadhara na kutaja kuwa Halmashauri ilichukua kiasi cha pesa kuanzia laki sita kwa kila mtu mwaka 2005 na kuahaidi kuwapatia viwanja lakini mpaka leo awakapewa.

Mara baada ya kupata taharifa hiyo ndipo waziri Lukuvi aliwagiza watendaji wa wilaya hiyo ndani ya miezi sita wawe wamewapatia wakazi hao viwanja hivyo.
 Lukuvi akiteta jambo na mkuu wa wilay aya Bagamoyo
 Lukuvi akiongozana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kuelekea Masijala
 Ridhiwani Kikwete akiteta na Mwenyekiti wa Wilaya ya Bagamoyo
 Wananchi wakisikila kwa makini waziri wa Ardhi
 Waziri Lukuvi akikagua Masijala ya wazi ya wizara ya Ardhi
Waziri wa Ardhi Wiliam Lukuvi akipokea karatasi za kero za migogoro ya Ardhi

Monday, January 11, 2016

Saccos inavyosaidia kuongeza kipato cha wafanyakazi TanescoNA TUNU NASSOR, DAR ES SALAAM

SACCOS ni kifupi cha neno la Kiingereza lijukanalo kwa Saving And Credit Co-operative Society. Kwa lugha ya Kiswahili ni Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo.
Kwa  mara ya kwanza Saccos  zilianzishwa Ujerumani na  mtu aitwaye Fredrick Taylor.  Sura ya Saccos aliyoanzisha Taylor inabadilika kadiri  shughuli za kijamii na kiuchumi zinavyokua mpaka kufikia aina ya Saccos zilizopo sasa.
Saccos ni asasi ya kifedha. Ni muungano wa watu ambao  lengo lao ni kukusanya fedha  na kukopeshana au  kufanyabiashara moja kwa  moja na kugawana faida.
Taratibu  za  kukopeshana na  kufanya biashara katika  Saccos hufanywa na watu wenye msimamo au  fungamano linalofanana.
Hii ina maana wanaweza  kuwa watu wanaofanya kazi  ya aina moja kwa mfano;  walimu, wafanyabiashara, wafanyakazi katika ofisi fulani, vijana wanaoishi eneo moja mtaani, wanawake walio katika eneo moja, waumini wanaosali pamoja, wakulima, wavuvi, wafugaji, wanakijiji na watu wote wa aina hiyo.
Tanesco Saccos ni chama cha akiba na mikopo cha wafanyakazi wa Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco).
Lengo kuu la kuanzishwa kwa Tanesco Saccos ni kutoa fursa kwa wafanyakazi wa shirika hilo kuongeza kipato na kupunguza mzigo mkubwa kwa shirika kwa kukidhi mahitaji ya watumishi.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa mwaka, Mwenyekiti wa Saccos hiyo, Somoe Nguhwe, anasema Saccos hiyo imekuwa na mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake.
Anasema mafanikio hayo yametokana na uongozi makini kujitoa kwao, kufanya kazi kwa ufanisi na ubunifu mkubwa.
Anasema moja ya mafanikio hayo ni kuanzishwa kwa huduma za kibenki zinazojulikana kama Front Office Service Activities (FOSA) ambazo zinawawezesha wanachama wao kupata huduma hizo karibu na kwa wakati.
Somoe anasema kuwa lengo la kuanzisha huduma hizo ni kuwapunguzia makali ya gharama za kibenki wanazokumbana nazo pindi wanapozihitaji.
Anasema huduma hiyo itawawezesha wanachama kupitisha mishahara yao na kutumia huduma zote za kisasa kama ATM, Sim Banking, kufungua akaunti za amana, kukopa na kurejesha nje ya mshahara na nyinginezo.
“Nawaomba wanachama wa Saccos hii kutumia huduma zote zitakazotolewa na ili kuwezesha kutekelezwa kwa mradi huo kikamilifu,” anasema Somoe.
Anasema kwa sasa wamefikia hatua nzuri za kukamilisha ununuzi na ufungaji wa mfumo huo.
“Tumefikia hatua nzuri kwa kumpata mzabuni ambaye ni kampuni ya FINTECH LTD ya nchini Kenya ambapo mapema mwakani huduma hizi zitaanza rasmi,” anasema Somoe.
Somoe anasema kutokana na umahiri wa uongozi, idadi ya wanachama imeongezeka kutoka 4,477 Desemba mwaka 2013 hadi 4,760 Desemba mwaka jana na kufanya ongezeko la asilimia 6.3.
Anasema akiba za wanachama zimeongezeka kutoka Sh bilioni 14.9 Desemba 2013 hadi Sh bilioni 18.8 mwaka jana na kufanya ongezeko la asilimia 20.8 huku faida juu ya akiba ni Sh milioni 376.6 sawa na asilimia 10 kutoka kiasi  kilichotolewa mwaka 2013 ambapo ilikuwa ni Sh milioni 288.7.
“Hisa za wanachama zimeongezeka kutoka Sh milioni 445.5 mwaka 2013 hadi bilioni 1.2 mwaka jana sawa na ongezeko la asilimia 179.6,” anasema Somoe.
Somoe anasema jumla ya Sh bilioni 20.3 ilitolewa kama mikopo kwa wanachama mwaka jana ikilinganishwa na bilioni 16 mwaka 2013.
Anasema taratibu zote za kumpata mshauri wa kutengeneza mpango wa biashara katika kiwanja cha Kibaha zimekamilika na tayari mzabuni ambaye ni Kampuni ya Property Consult Service amepatikana.
“Bodi ya chama inaangalia uwezekano kushirikisha wadau wa ubia katika nyanja ya ujenzi wa majengo,” anasema Somoe.
Anasema Saccos hiyo imeongeza wigo wa uanachama ambapo wastaafu wa Tanesco na wafanyakazi wa kampuni ya uzalishaji umeme wanaruhusiwa kuwa wanachama.
“Katika kuimarisha uwezo wa kifedha wa ndani wanachama wanahamasishwa kununua hisa na kuongeza akiba,” anasema.
Naye Mhandisi Sophia Mgonja ameisifu Saccos hiyo kwa kulipunguzia mzigo shirika la umeme nchini kutokana na kukidhi mahitaji ya watumishi wa shirika.
“Nimefurahishwa na saccos hii kwa kuweza kuingiza wanachama ambao ni watumishi wa wazalishaji umeme wengine kama Simbion na wengine… hii ni hatua muhimu katika ukuaji wa saccos,” anasema Sophia.
Sophia anawasihi viongozi wa Saccos hii kuwa waaminifu na waadilifu ili kupata matokeo wanayoyatarajia.
“Nawasihi wanachama pia wanapokopa wawe wamejiandaa kufanya kitu na pia kuwe na sababu maalumu ya kufanya hivyo, wajipange kwanza,” anasema Sophia.
Mwisho….

Watanzania tunahitaji Samatta wengineBADO Watanzania wanaendelea na shangwe kufuatia mchezaji wao kipenzi Mbwana Samatta kutua nchini juzi usiku akiwa na tuzo ya uchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani aliyoshinda Alhamisi iliyopita.

Watanzania walikesha usiku kucha katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere wakimsubiri mchezaji huyo aliyekuwa akitokea nchini Nigeria zilikotolewa tuzo hizo.

Samatta alitua takribani saa nane na nusu usiku na kupokewa na umati wa Watanzania walioanza kujikusanya uwanja wa ndege tangu saa moja usiku.

Hamasa hiyo inatoa taswira pana kwa Watanzania kwamba wanahitaji kuona juhudi kama hizo alizofanya Samatta haziwezi kupita bila kuungwa mkono.

Sisi tunarudia tena kumpongeza Samatta lakini pia tunazipongeza salamu za dhati alizotoa Rais John Pombe Magufuli kwa mchezaji huyo kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Kwa kuangalia yote hayo Jijiletu blog tunayo sababu nzito ya kutamka wazi kwamba Watanzania wanahitaji kuwaona akina Samatta wengine wanalitangaza taifa letu kupitia michezo na sanaa.

Tunasema hivyo tukiwa na kumbukumbu nzuri ya jinsi Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, alivyokuwa akionyesha mapenzi ya dhati na wasanii kiasi cha kujumuika nao mara kadhaa hasa pale inapotokea kufanya jambo lililoitangaza nchi yetu nje ya mipaka.

Kadhalika, tumefurahishwa na jinsi Rais alivyoonyesha kuguswa na mafanikio ya mchezaji huyo kiasi cha kutumia muda wake mchache uliojaa majukumu mengi ya kiutendaji na kumtumia salamu za pongezi.

Dimba pia tunawapongeza wadau wengine waliojitokeza hususan Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF, Jamal Malinzi aliyeeleza wazi juu ya taasisi anayoiongoza kufurahishwa na hatua hiyo ya kijana wa Kitanzania.

Kwetu sisi kama wadau wakubwa wa michezo hususan soka, tunaona kwamba hatua aliyofikia Samatta ni kama vile amepata ufunguo utakaosaidia kufungua lango la mafanikio kwa wanasoka wengine wa soka nchini wanaopigania kucheza soka nje ya nchi.

Tunaamini kwa sasa wachezaji wengine wataendelea kuifanyia kazi kauli ya mwanasoka mwingine mwenye mafanikio, Thomas Ulimwengu aliyecheza kwa karibu sana na Samatta katika Klabu ya TP Mazembe ya nchini DRC kwamba njia ya kupata mafanikio kisoka ni wachezaji kuangalia nafasi nje ya mipaka ya Tanzania.

Tunamuombea kila la heri Samatta katika safari yake ya soka popote pale atakapopata nafasi ya kucheza, lakini pia tunazidi kuwaamsha wanasoka wengine wa hapa nyumbani kuzidisha juhudi kila wanapokuwa uwanjani ili siku moja nao wafikie na pengine kupita pale alipoishia Mtanzania mwenzao, Mbwana Samatta.

Tambwe Asema sina Bahati na MapinduziSTRAIKA wa kimataifa wa Burundi, Amis Tambwe, amekuwa akiwalaza macho mabeki wa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na umahiri wake wa kupachika mabao lakini ameshindwa kutamba kwenye Kombe la Mapinduzi.
Akizungumza Tambwe alisema inawezekana kutofunga katika mashindano hayo kunatokana na  upinzani mkali uliopo lakini suala la bahati lina nafasi yake.
 “Mambo mengine sio ya kulazimisha kwani unaweza kujituma kadiri uwezavyo lakini kama Mungu ameandika usifanikiwe huwezi kutimiza malengo,” alisema nyota wa zamani wa Simba.

Rais Magufuli amtembelea Sumaye Muhimbili
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS Dk. John Magufuli, jana amemtembelea na kumpa pole Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye ambaye amelazwa katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Sumaye amelazwa katika taasisi hiyo siku nne zilizopita kwa matibabu ya moyo na madaktari wanaomtibu wamemhakikishia Rais Magufuli kuwa anaendelea vizuri ikilinganishwa na wakati alipofikishwa katika Taasisi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Garson Msingwa, ilieleza kuwa pamoja na kumpa pole, Rais Magufuli pia amemuombea kwa Mwenyezi Mungu apone haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
Akizungumza mara baada ya kuonana na Rais, Waziri Mkuu mstaafu Sumaye amemshukuru Rais Magufuli kwa kwenda kumuona na kueleza kuwa kitendo hicho kimeonesha jinsi alivyo na upendo wa dhati na anavyowajali watu wake.
Kuhusu hali yake, Sumaye, alisema anaendelea vizuri, anapata matibabu mazuri na kwamba kwa kuwa hali yake ni nzuri anatarajia kuruhusiwa kuondoka hospitali hapo baada ya muda mfupi.

UJENZI WA NJIA NNE MOROGORO ROAD ENEO LA MBEZI WASHIKA KASI

Wakandarasi wakiendelea na ujenzi wa Roound about ya Msigani kama inavyoonekana katika picha Barabara ya Morogoro Road katika Mfumo wa nj...