Friday, January 29, 2016

TPDC yawatahadharisha wananchiSHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limesema wananchi waliojenga bila kufuata utaratibu wa mipango miji watakosa fursa ya kuunganishiwa nishati ya gesi kwa matumizi ya nyumbani.
Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam katika semina ya kuwajengea waandishi wa habari uelewa wa masuala ya gesi asilia, Ofisa Utafiti wa TPDC, Eva Swillah, alisema mtandao wa gesi asilia utapita kwenye maeneo yaliyopangwa kutokana na masuala ya kiusalama kwa miundombinu ya gesi.
“Gesi asilia itasambazwa katika maeneo yaliyopagwa na mipango miji tu kwasababu za kiusalama zaidi,” alisema nakuongeza: “miundombinu ya gesi inahitaji uangalizi wa hali ya juu hivyo kuiweka maeneo yasiyopangwa kutaleta usumbufu mkubwa pale maeneo hayo yatakapotakiwa kubadilishwa matumizi.”
Alisema mradi wa kusambaza gesi wa Ubungo-Mikocheni wa kilomita 6.2 wa bomba la 12 umekamilika, ambapo nyumba 70 zimeunganishwa, magari 70 yameshafanyiwa matengenezo ya kutumia gesi, Viwanda vitano vimeunganishwa na gesi na kituo kimoja cha kujazia gesi kwenye magari kilichopo Ubungo kimekamilika.
Akielezea gharama za gesi alisema kwa matumizi ya nyumbani kwa sasa ‘unit’ moja ni sh 1,000 na kwamba gharama za kuunganishwa inategemea na umbali wa mteja kutoka lilipo bomba la gesi.
Kuhusu gharama za kuweka mfumo wa gesi kwenye gari alisema kwa magari madogo inagharimu dola za Kimarekani 1000 sawa na sh milioni 2 na kwasasa kazi hiyo inafanywa na Kampuni ya Ukandarasi ya BICO ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (DIT).
Aidha alisema matumizi ya gesi ni nafuu kuliko matumizi ya mafuta na kwamba ni rafiki wa mazingira kwasababu haitoi moshi mwingi.
“Kwa sasa hivi kilo moja ya gesi ambayo ni sawa na mafuta lita moja inauzwa sh 1,450 na unaweza kwenda umbali mara moja na nusu zaidi ya mtu anaye tumia nishati ya mafuta,” alisema Swilaah.
Naye Mkurugenzi wa Mkondo wa Chini, Dk. Wellington Hudson, alisema TPDC ipo mbioni kuanza jenzi wa miradi mipya ya kusambaza gesi kwa matumizi ya nyumbani, viwandani, kwenye magari na kufua umeme katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Dar es Salaam.
Alisema miradi hiyo ambayo itaunganishwa na bomba jipya inatarajia kuunganisha nyumba 50,000 ambapo kwa Dar es Salaam zitaunganishwa nyumba 30,000, Lindi 9000 na Mtwara 11,000.
Alisema miradi ya Mtwara na Lindi ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha upembuzi yakinifu na baada ya kukamilika kwa hatua hiyo watakamilisha michoro tayari kwa kuanza ujenzi.
“Kwa upande wa Dar es Salaam mchoro umekwisha kamilika na tumeanza mawasiliano na benki mbalimbali ikiwemo Benki ya Exim ya China na Benki Exim ya India ili kupata fedha za kuanza ujenzi wa mradi,” alisema Dk. Hudson.
Alisema mradi huo wa Dar es Salaam pia  itahusisha ujenzi wa vituo 15 vya kujaza gesi, magari 8,000 kuanza kutumia gesi na kwamba mradi huo utamilikiwa na TPDC kwa asilimia 100.
“Kutakuwa na mabomba matatu la kwanza litaanzia Wazo- kupitia barabara ya Bagamoyo- Ali Hassan Mwinyi- Bibi Titi hadi barabara ya Morogoro.
 “Bomba jingine litaanzia Ubungo kupitia Barabara ya Mandela kuelekea Bandarini na lingine litaanzia Kinyerezi kupita Barabara ya Pugu,” alisema Dk. Hudson.

VIfaa vyalikwamisha soko la samaki feri


UBORA wa vifaa na kusahaulika kwa wavuvi nchini kumesababisha soko la samaki kuzidi kudidimia kila kukicha.

Akizungumza jana jijini Dar eŇ° Salaam na Mtanzania , Karibu wa Soko la Feri, Mbaraka Kilima amesema, ukosefu wa zana za kisasa kwa wavuvi hapa nchini ndiyo chanzo cha soko la samaki kushuka.

"Vifaa wanavyotumia wavuvi hapa nchini vingi ni vya mbao havina ubora wala kivutio cha kuweza kuwashawishi samaki kuvuliwa kwa wingi,"alisema Kilima.

Alisema ni wakati sasa kwa wizara husika kuhakikisha inaondoa changamoto zinazowakabili wavuvi ili kuendeleza sekta hiyo muhimu nchini.

"Wakulima wana sera yao kabisa ya kilimo kwanza lako no wavuvi wamesahaulika kabisa hat a mwenzetu wengine wanakopeshwa lakini sekta hii imesahaulika,"alisema Kilima.

Alisema wavuvi wamekuwa wakitozwa ushuru mkubwa lakini hakuna mrejesho wa ushuru huo.

Kilimanjaro alisema sekta ya uvuvi inategemewa na watanzania karibu asilimia 98 ambapo wanajipatia kipato na wengine kufanya chakula.

Kilima alisema wanashangaa serikali imekuwa ikipiga vita uvuvi haramu lakini haina sera ya kuwaendeleza wavuvi nchini.


photo story of Dibate of Media and Election at Aliance Francia's Dar es Salaam Tanzania


 Balozi wa Ufaransa nchini

 Barozi wa Ufaransa nchini Tanzania akiwa nakatibu mkuu wa Baraza la Habari nchini KajubI Mukajanga
 wana habari walioshiriki mdahalo huo


Thursday, January 28, 2016

Dibates ,Media and Election on progress at Aliance Flancia's

Jumla ya miamba minne ya habari na harakati za maendeleo imeweza kukutana na mmoja wa waandishi kutoka nchini ufaransa katika mdahalo wa masuala yalijiri katika uchaguzi mkuu kupitia vyombo vya habari.

Miamba hiyo ni Kajubi Mukajanga Katibu mkuu wa Baraza la Habari nchini, Aidan Eyakuze mkurugenzi wa Twaweza nchini,Gadi Ramadhani mcharaji vibonzo magazetini na msanii mbinfubwa maonysho,Maria Sarungi Tsehai pamoja na Haby Niakate mwandishi wa habari kitoka ufaransa.

Mjadala huu ambao unaendelea umeweza kupita katika mjadala wa umuhimu wa kupiga kurai

Mafuriko yawalaza nje tena Wakazi wa JangwaniNa Humphrey Shao

WAKAZI wa mitaa mabondeni kuzunguka Bonde la mto Msimbazi na mitaa ya jangwani wameendelea kuteseka na mafuriko kufuatia mvua kubwa zianzonyesha jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa blog hii alifika katika mitaa hiyo na kujionea namna gani watu wanavyopata tabu nakushindwa kuishi katika makazi yao kama ilivyokuwa hapo awali.

Jijiletu blog ilishuhudia watoto wadogo na wanawake wakiwa wahanga wakubwa hasa watoto wa shule ambao walishindwa kwenda shule kutokana na kukosa usngizi kwa jili kukesha kujikinga na mufuriko huku madahtari yao yakiwa yamekwenda na maji.Yanga yawasili Tanga kuivaa Coast kwa MbwembweNa  Humphrey Shao

Mabigwa wa ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanazania Bara(VPL) Dar es Salaam Yanga Afrika imewasili mjini tanga tayari kujianda na mchezo wao dhidi ya Coast Union utakaopigwa katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Yanga ambayo iliondoka jijini Dar es Salaam majira ya Saa nne asubuhi kuelekea mkoani humo tayari imeshawasili mji tanga na kufikia katika Hoteli kubwa ya Kisasa ya Kwetu Hotel.
Klabu ya Yanga mabyo ipo kileleni mwa ligi kuu hiyo itakuwa ndio mchezo wake wa mwisho wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania kabla ya kusafiri kwenda nchini Moritius kucheza michezo ya kimataifa.

Kocha wa timu Hans van Plujim aliambia blog hii kuwa timu yake ipo vizurio na inajianda kwa ajili ya mchezo huo ambao ametamba kuchukua point tatu mbele ya wagosi hao.
Atakaye Saidia kukamatwa kwa SMG Dar kulamba donge NonoKAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna Simoni Sirro, ameahidi zawadi ya Sh milioni moja kwa atakayetoa siri ya jambazi anayetumia bunduki aina ya SMG kwani silaha hiyo ni hatari.
Kamanda Sirro alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, wakati akizungumza na wakazi wa mtaa wa Nyambwera kata ya Tandika Manispaa yaTemeke katika  mkutano wa uhamasishaji ulinzi shirikishi mtaani hapo.
Alisema kuwa silaha hiyo ni kubwa hivyo yupo tayari kutoa fedha hizo kwa yeyote atakayefichua siri za kuwepo kwa aina hiyo ya silaha.
Pia aliwataka vijana wa mtaa huo kuachana na mambo ya  uhalifu kwasababu  uhalifu una mwisho wake na kuwataka wazazi kuwaonya  watoto wao wanaofanya biashara  za kihalifu na kuwakemea waache mara moja.
“Hakuna mtu anayepata heshima kwaajili ya kazi ya wizi au ujambazi wakati kila mtu anajua mwisho wa wizi ni nini kitachotokea, ni vyema kufanya biashara itakayokupatia kipato halali,” alisema.
Kamanda Sirro ametoa onyo kwa majambazi kuacha mara moja  kazi hiyo  na kama hawataki wataishia mikononi  mwake au kwa vijana wake.
Pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa polisi ili kuwafichua majambazi, vibaka, wauza gongo na madawa ya kulevya ili mtaa huo waishi kwa amani.
Kamanda Sirro pia aliwataka wenyeviti wa mtaa kutimiza wajibu wao na kuhakikisha wananchi  wanaishi kwa amani kwani hiyo ni moja ya kazi yao.
Pia aliwataka wananchi kutoa taarifa endapo wataona kuwa mwenyekiti hatimizi wajibu wao ili waweze kuwachukulia hatua za kisheria kwa ni sasa hivi hapa ni kazi tu.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...