Friday, February 12, 2016

FURAHISHA OMARY AMTWANGA MPINZANI WAKE FAINALI NGUMI UZITO WA BANTAM

 Hamdani Issa Red Corner (JKT) Akitupiana makonde na Furahisha Omary Blue cOrner katik faina li ya mchezo wa ngumi za ridhaa nchii  ambapo Omary alishinda kwa point
 Furahisha Omary akimtupia konde Hamdani Issa

 Hamdani Issa Red Corner (JKT) Akitupiana makonde na Furahisha Omary Blue cOrner katik faina li ya mchezo wa ngumi za ridhaa nchii  ambapo Omary alishinda kwa point

SHAMSA FORD NA DIDA WAZICHAPA ULINGONI KAVUKAVU

 Shamsa Ford na Dida wa Mchops wakitwangana makonde Jukwaani  katik afainali za mchezo wa ngumi za Ridhaa hapa nchini

SERIKALI YAWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI WAKALA WA VIPIMO

SERIKALI imeamua kuwasimamisha kazi watendaji wawili kutoka Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kuanzia leo ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa mafuta bandarini kutokana na zuio la kufunga kwa mita kwa zaidi ya miaka mitano.
Waliosimamishwa kazi ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Bi. Magdalena Chuwa na Meneja Vipimo Kitengo cha Bandari, Bi. Bernadina Mwijarubi. Bi. Mwijarubi ndiye anashughulikia kitengo cha mafuta bandarini.
Akitangaza uamuzi huo kwenye kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika leo (Ijumaa, Februari 12, 2016) ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Adelhelm Meru awaandikie barua za kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi huo.
“Katibu Mkuu Viwanda, waandikie barua za kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi. Katika kipindi hiki hawatatakiwa kusafiri kwenda popote hadi uchunguzi utakapokamilika. Pia utafute mtu wa kukaimu nafasi hiyo ili kazi ziendelee,” alisema.
Waziri Mkuu pia amesema ofisi yake itawaandikia barua ofisi ya TAKUKURU na polisi ili wafuatilie suala hilo mara moja na ikithibitika kuwa walihusika hatua rasmi zitachukuliwa na itathibitika hawakuhusika basi watarudishwa.
Waziri Mkuu pia aliagiza mfumo wa upimaji mafuta kwa kutumia flow meters uendelee kutumika na ule upimaji wa kukadiria uache kutumiwa mara moja.
Jana (Alhamisi, Februari 11, 2016) Waziri Mkuu alifanya ziara kukagua flow meters za zamani zilizopo Kurasini (Kurasini Oil Jetty) na kisha akatembelea na kukagua flow meters mpya ambazo zinajengwa Kigamboni. Mita hizo zimegharimu dola za marekani milioni 6 (sawa na sh. bilioni 12.96/- za sasa).
Pia Waziri Mkuu alitembelea sehemu ya kuchukulia mafuta yanayotoka bandarini (TPA Manfold) iliyoko Kigamboni na kukagua mitambo ya kusambazia mafuta kwenye matenki ya mafuta ya kampuni ya TIPER yaliyoko Kigamboni yanayomilikiwa kwa ubia baina ya Serikali na kampuni ya Oryx Energies.
Katika ziara hiyo ilibainika kuwa Kampuni ya TIPER imejiunganishia bomba la moja kwa moja kutoka kwenye bomba kubwa la mafuta linalotoka bandarini hali iliyomlazimu Waziri Mkuu kuagiza kwamba bomba hilo litolewe kwenye maungio hayo ndani ya mwezi mmoja.
“Jana niliagiza kuwa bomba hilo ling’olewe. Nimetoa mwezi mmoja ili kurekebisha mfumo huo. Simamieni vizuri na kuhakikisha kuwa na wao pia wanarudi kwenye manfold kama ilivyo kwa wengine,” alisema Waziri Mkuu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
IJUMAA, FEBRUARI 12,

Wednesday, February 10, 2016

MAGUFULI AFANYA ZIARA YA GHAFLA MUHIMBILIJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Description: Description: Description: Description: Description: Coat of ArmsKURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametembelea kwa ghafla wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam, na kujionea hali ya msongamano mkubwa wa wazazi uliosababishwa na uhaba wa vitanda na nafasi finyu katika wodi hiyo.
Rais Magufuli aliyekuwa akitoka katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alikokwenda kumuona na kumjulia hali Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubery Bin Ally, amelazimika kwenda katika wodi hiyo baada ya msafara wake kusimamishwa na kundi la akina mama, waliomtaka kwenda katika wodi ya wazazi ili akajionee jinsi wazazi wanavyokabiliwa na kero mbalimbali ikiwemo ya kulala chini kutokana na kukosa vitanda.
Baada ya kujionea mwenyewe kero ya msongamano na kuzungumza baadhi wazazi waliojifungua, Rais Magufuli amewaahidi wazazi hao kuwa atashughulikia kero alizozishuhudia.
"Nimeiona hali halisi mimi mwenyewe, watu wanapata shida, watu wana mateso, na ndio maana nimeamua kuja kwa makusudi, sikuomba ruhusa ili nijionee hali ilivyo, nimejifunza mengi, ninayabeba na nitajua namna ya kuyatatua" Alisema Rais Magufuli.
Kabla ya kutembelea wodi ya wazazi, Dkt. Magufuli amemjulia hali Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubery Ally aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo  amempa pole na kumuombea apone haraka.
Pamoja na kupokea pole ya Rais, Mufti wa Tanzania ameongoza dua ya kumuombea heri Rais Magufuli ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake katika kuwahudumia watanzania.
Dua kama hiyo pia imefanywa na wananchi wengine waliokuwa wakimsubiri nje ya majengo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo katika dua hiyo wamemuomba Mwenyezi Mungu kumlinda na kumuongoza katika majukumu yake ya kuiongoza nchi.
"Mwenyezi Mungu mbariki Rais wetu, mpe hekima, busara na upendo katika kazi zake za kuiongoza nchi hii ili watanzania wote wanufaike" ilisema sehemu ya dua hiyo iliyoongozwa na mmoja wa akina Mama.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
10 Februari, 2016.  


MAYANJA AITIA YANGA KIBINDONIKOCHA Mkuu wa wekundu wa Msimbazi Simba Mganda, Jackson Mayanja, ameweka wazi kuwa amenasa mbinu na mfumo wa wapinzani wake   Yanga na kunasa udhaifu wa kikosi hicho ambao umempa 'kiburi' cha kusema kiama chao ni Februari 20 mwaka huu, timu hizo zitakapovaana Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Simba iko mjini Shinyanga kucheza mechi zake mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na tayari imekwishamaliza moja Jumapili dhidi ya Kagera Sugar, huku ikisubiri kuvaana na Stand United Jumamosi ijayo.

Katika muda huo, mahasimu wao Yanga watakuwa wamekwenda nchini Mauritius kuanzia kesho Alhamisi kwa ajili ya kucheza mechi ya Klabu Bingwa Afrika.

Watakaporudi, timu hizo mbili zitavaana hapo Februari 20 ambapo Simba imesema ikitoka Shinyanga tu inapitiliza moja kwa moja kuweka kambi kisiwani Zanzibar kwa ajili ya mechi hiyo.

Kocha Msaidizi wa Simba, Mayanja ambaye ndiye anayekaimu nafasi ya ukocha mkuu ameapa kwamba Yanga haiponi hata kwa dawa katika mchezo huo wa kwanza wa watani wa jadi msimu huu.
Simba imepanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na sasa ina pointi 1 tu nyuma ya Yanga wanaoongoza kwa pointi 43, huku Simba na Azam zikiwa na pointi 42 kila moja.
Kocha huyo alisema amewaangalia Yanga mara nyingi na amegundua kuwa hawana kikosi cha kumtisha na kama wakicheza mpira kwa kiwango walichoonyesha kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union walipopigwa bao 2-0 na ile dhidi ya Prisons walipolazimishwa sare ya bao 2-2 ugenini basi waandike maumivu kwani  maafa watakayokutana nayo ni makubwa.
Mayanja ameniambia kwamba, anahitaji kufanya vizuri katika mechi zote zilizosalia za Ligi Kuu hivyo anachokiangalia zaidi kwa sasa ni mchezo wao dhidi ya Stand United.
Alisema timu ndogo ndio zinasumbua zaidi hivyo mara nyingi anaumiza kichwa pale atapokutana na Stand au timu nyingine ya Ligi Kuu lakini kwa Yanga gemu anaiona ni rahisi zaidi.
"Ukiijulia Yanga vizuri kocha huna presha kwani niliwahi kuwafunga nikiwa Kagera, kikubwa ni kujua nini natakiwa kufanya na majukumu yapi yanahitajika kwa wachezaji wangu," alisema.
Aliongeza: "Rasmi tutakamata usukani wa ligi tutakapokutana na Yanga Februari 20, iwe isiwe lazima tuhakikishe tunakaa kileleni kwa kuchukua pointi tatu muhimu mikononi mwa watani zetu wa jadi, hiyo itapendeza sana na kwa kiwango cha timu yangu sasa Yanga wataumia sana.
"Ingawa mpira unabadilika na huwa tukikutana na Yanga hata kama timu inakuwa mbovu inabadilika na kucheza kwa kiwango, lakini kama Yanga watacheza kwa kiwango walichokionyesha kwenye mechi zao mbili basi wamekwisha maana hawana jipya," alisema Mayanja.
Kuhusu Amissi Tambwe, Donald Ngoma pamoja na Simon Msuva alisema: "Nina beki mahiri na makini ambazo naamini zitawaficha akina Tambwe, Ngoma na Msuva siku hiyo na hawatafurukuta kama kwenye mechi za hivi karibuni ambako hawakuonekana, sasa kwetu kwanini tuwashindwe, we subiri utaona."
Mayanja alisema hatishwi na jinsi Yanga inavyofanya vizuri katika Uwanja wa Taifa kwani akiangalia kikosi chake kinafanya vizuri zaidi nyumbani na ugenini.
"Hiyo ni mechi ya kuvutia kwani ukiangalia Yanga ilipoteza pointi mkoani, lakini vijana wangu wanafanya kazi vizuri hatujapoteza, pia ukiangalia rekodi za Uwanja wa Taifa wao wanafunga mabao mengi na sisi pia, kikubwa naifahamu Yanga na kuhakikisha nakiandaa kikosi kwa ajili ya kutafuta ushindi," alisema.

YANGA YAKODI NDEGE KUKWEPA JANJA YA MORITIUSJESHI la Yanga lenye wachezaji 21, viongozi 7 wa benchi la ufundi na utawala pamoja na mmoja kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linaondoka kesho Alhamisi kuelekea nchini Mauritius, likiwa 'kamili gado' kwa Ndege ya kukodi tayari kuwavaa mabingwa wa huko, Cercle de Joachim katika mechi ya mkondo wa kwanza, mzunguko wa awali wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika

Yanga mabyo imeamua kukodi ndege hili kukwepa hujuma za wapinzani wao ambao waliamu kuwapangia ruti ya mzunguko hili waweze kufika nchini humo wakiwa wamechoka.

Mara baada ya kubaini hayo tajiri wa Timu hiyo Yusufu Manji aliamua kukodisha Ndege kwa ajili ya timu yake hili ifike ikiwa na hali na morali.

y
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu inatarajiwa kupigwa Jumamosi wiki hii saa 10:00 alasiri kwa saa za Tanzania kwenye Uwanja wa Stade George V, mjini Port Loius, huku Yanga ikipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kutokana na udhaifu walionao wapinzani wao.
Awali, Yanga ilikuwa iondoke leo Jumatano alfajiri lakini safari yake ikasogezwa mbele baada ya ndege ya Afrika Kusini kuelezwa kwamba imejaa hivyo kusababisha ratiba ipanguke.
Msafara wa Yanga unaoondoka kesho utaongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya TFF, Ayoub Nyenzi na wanatarajia kuondoka alfajiri ya kesho kwa ndege ya Shirika la ndege la Afrika Kusini, ambapo kabla ya kwenda Mauritius, watapitia kwanza jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Licha ya kutambua kuwa wapinzani wake kwa sasa ni dhaifu, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm, amekubali kusafiri umbali wa maili 1,531 ambazo ni sawa na kilomita 2463.91 kwenda huko kusaka ushindi akiwa na silaha zake zote nzito ili kujiweka tayari kwa lolote linaloweza kutokea katika mchezo huo.
Idadi hiyo ya wachezaji 21 inawajumuisha pia nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub 'Cannavaro', beki la kushoto Haji Mwinyi Mgwali na kiungo mkabaji Mzimbabwe, Thaban Kamusoko ambao walikuwa majeruhi lakini sasa wako fiti.
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, alisema jana kuwa kikosi hicho kitaondoka na jeshi kamili kwenda Mauritius huku ikiwaacha kipa namba tatu, Benedicto Tinocco na Godfrey Mwashiuya ambao wana matatizo ya hati za kusafiria na Matheo Anthony ambaye hayuko fiti kiafya.
Muro alisema Cannavaro, Haji na Kamusoko wataungana na wenzao 19 walio fiti ambao ni Ally Mustapha ‘Barthez’, Deogratius Munishi 'Dida,' Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Vincent Boussou na Pato Ngonyani.
Viungo ni Salumu Telela, Said Juma 'Makapu', Haruna Niyonzima na Issofou Abubacar wakati washambuliaji ni Amissi Tambwe, Deus Kaseke, Simon Msuva, Malimi Busungu, Donald Ngoma na Paul Nonga.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zimelieleza DIMBA Jumatano kwamba, kikosi cha timu hiyo kitafikia kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota tano nchini Mauritius, ambayo ina uwanja mdogo wa mazoezi na bwawa kubwa la kuogelea ingawa mtoa habari hakutaka kuitaja jina kwa sasa.
Kocha wa Yanga, Pluijm amesema pamoja na kwamba ameelezwa wapinzani wake ni dhaifu, lakini atawapangia kikosi ambacho kitampa ushindi mnono ugenini ili kazi ya kuvuka nyumbani iwe rahisi.
"Tunajua tunakwenda kucheza mechi ngumu ugenini. Ni lazima iwe ngumu sana kwa sababu hatuwafahamu vizuri wapinzani wetu lakini kama timu yangu ikicheza kwa kiwango ninachokijua, sioni kama wanaweza kutuzuia tusipate ushindi wa ugenini," alisema Pluijm.
Yanga inakwenda Mauritius ikiwa na ari ya ushindi baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kuicharaza mabao 4-0 JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku wakijivunia kutotishwa na hali ya hewa ya nchi hiyo.
Kwa miezi ya Januari na Februari nyuzi joto la Mauritius ni 29.2 °C ambayo inafanana na jijini Dar es Salaam hivyo kutokua kikwazo cha kukosa ushindi.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) mchezo huo utachezwa na waamuzi kutoka nchini Madagascar wakati Kamisaa wa mchezo anatoka nchini Msumbiji.
Mwamuzi atakayesimama kati siku hiyo atakuwa ni Hubert Marie Bruno ambaye atasaidiwa na Randrianarivelo Ravonirina na Augustin Gabriel Herinirina, wakati mwamuzi wa akiba ni Anndofetrra Avombitana Rakotojaona huku Kamisaa akiwa ni Feizal Ismael Sidat.
Yanga ikipita hatua hiyo baada ya mechi za marudiano jijini Dar es Salaam wiki mbili zijazo, itakutana na mshindi kati ya APR ya Rwanda na Mbabane Swallows ya Swaziland na kama ikivuka tena hatua hiyo, itakutana na Al Ahly ya Misri au mshindi kati ya Recreativo de Libolo ya Angola na Racing Micomiseng ya Equatorial Guinea.
Mbali na Yanga, wawakilishi wengine katika mashindano ya kimataifa ni Azam FC ya Dar es Salaam, Mafunzo pamoja na Jamhuri za Zanzibar.
Azam FC itaanzia kucheza ugenini katika raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kati ya Machi 11, 12 na 13 kabla ya kumalizia nyumbani kati ya Machi 18, 19 na 20 na ikivuka mtihani huo, itakutana na ama Esperance ya Tunisia, wawakilishi wa Chad au News Stars de Douala ya Cameroon.
Mabingwa wa Zanzibar, Mafunzo wao wataanzia raundi ya awali na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati JKU itacheza na Gaborone ya Botswana katika Kombe la Shirikisho.


Tuesday, February 9, 2016

ALBINO 80 UFARIKI KILA MWAKA KWA KUKOSA MAFUTA YA NGOZI

ASILIMIA 80 ya watu wenye ulemavu wa ngozi hufariki dunia kila mwaka nchini kwa kukosa matibabu dhidi ya tatizo la saratani ya ngozi.
Akizungumza na MTANZANIA mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Saratani duniani Ofisa Mahusiano wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Josephat Tona alisema hiyo ni kwa sababu huchelewa kufika katika vituo vya afya.
“Umri wa kuishi wa albino ni miaka 35 na 40 tofauti na watu wengine ambao hufika hadi kati ya miaka 50 hadi 70. Asilimia 80 wanafariki kwa sababu ya kuugua saratani ya ngozi ambayo kwa mujibu wa watalaamu inasababishwa na miale ya jua,” alisema.
Alisema ili kujikinga dhidi ya saratani hiyo huhitaji mafuta maalumu ya kupaka kwenye ngozi hata hivyo hushindwa kumudu gharama ya kuyanunua mafuta hayo.
“Naiomba serikali itenge bajeti itakayowezesha Albino kupata huduma za afya zilizo bora, itusaidie pia kupata mafuta ya kuzuia mionzi ya jua ambayo ni ghali na mara nyingi huwa yanatoka nchi za Ulaya, nakumbuka mara ya mwisho ilikuwa 2013 ambapo tulipatiwa jumla ya ‘tube’ 4000 za mafuta za kugawa nchi nzima ambayo kimsingi hazitoshi,” alisema


TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...