Friday, February 19, 2016

SDL MZUNGUKO WA 9 WIKIENDI HII

Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kuendelea wikiendi hii katika mzunguko wa lala salama (raundi ya 9), kwa timu zote 24 kushuka dimbani pointi 3 muhimu katika msimamo ili kuweza kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Jumamosi Kundi A, Green Warriors v Transit Camp (Mabatini), Singida United v Abajaro Tabora (Namfua), Mvuvumwa FC v Mirambo (Lake Tanganyika).
Kundi B, Jumapili Pamba FC v Madini FC (CCM Kirumba), AFC ARUSHA v Bulyanhulu (Sheikh Amri Abeid), huku Jumatatu Alliance School v JKT Rwamkoma (CCM Kirumba).
Jumamosi Kundi C, Cosmopolitan FC v Abajaro Dar (Karume), Jumapili Mshikamano FC v Kariakoo FC (Mabatini), Villa Squad v Changanyikeni (Karume).
Kundi D, Jumamosi African Wanderes v Mkamba Rangers (Wambi Mafinga), Jumapili Wenda FC v Sabasaba FC (Sokoine) huku Jumatatu The Mighty Elephant v Mbeya Warriors (Majimaji)

LIGI KUU MZUNGUKO WA 20 WIKIENDI HII KWA KUZIKUTANISHA SIMBA NA YANGA

Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea wikiendi hii mzunguko wa 20 kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali huku Jumamosi michezo mitano ikichezwa kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu katika ligi hiyo.
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Yanga SC v Simba SC watakua wakichuana kusaka uongozi wa Ligi hiyo katika mchezo namba 153, huku Mgambo Shooting wakiwakaribisha Tanzania Prisons katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Wagonga Nyundo wa jiji la Mbeya, Mbeya City watawakaribisha Azam FC katika uwanja wa Sokoine mjini humi, mjini Shinyanga chama la wana Stand United watawakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Kambarage, huku Toto Africans wakicheza dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Jumapili Ndanda FC watakua wenyeji wa African Sports uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, Mwadui FC watakua wenyeji wa Coastal Union uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga, huku wana lizombe Majimaji FC wakicheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.

SPIKA NDUNGAI AKUTANA NA UJUMBE WA BUNGE LA SWEDEN

 pika wa Bunge Mhe Job NdugaiakizungumzanaWabungewa Sweden  waliomtembelealeoOfisinikwakeJijini Dar es Salaam tarehe 19 Febuari, 2016.
 
1.     Spika wa Bunge Mhe Job NdugaiakizungumzanaWabungewa Sweden  waliomtembelealeoOfisinikwakeJijini Dar es Salaam tarehe 19 Febuari, 2016.


 Spikawa Bunge Mhe Job NdugaiakizungumzanaKiongoziwaMsafarawaWabungekutoka Sweden waliomtembelealeoOfisinikwakeJijini Dar es Salaam Bw. Kenneth Forslund. KulianiNaibuSpikawa Bunge Dkt Tulia Ackson
1.     Spikawa Bunge akiwakatikapichayapamojanaWabungewa Bunge la Sweden waliokujakumtembeleaOfisinikwakejijini Dar es salaam pamojanaViongoziwengineWabunge
 wabunge wa bunge la Jamhuri ya mungano wa Tanzania
1.     Spikawa Bunge akiagananaUjumbewaWabungewa Bunge la Sweden marabaadayakuzungumzanaoOfisinikwakejijini Dar es salaam.

Ben Pol: Sitauchora ‘tattoo’ mwili wangu kamwe


MSANII wa Bongo Fleva, Benard Paul ‘Ben Paul’, amesema  hapendi na hatauchora ‘tattoo’ mwili wake kama baadhi ya wasanii na watu maarufu wafanyavyo kwa kuwa anauheshimu sana.
Ben Paul alisema imekuwa ni kawaida kwa idadi kubwa ya wasanii kujichora ‘tattoo’ na kuwa na mwonekano wa tofauti na watu wengine, lakini kwake jambo hilo halina nafasi.
“Japo ni msanii lakini sipendi kuwa na mwonekano wa tofauti kama kufuga rasta, kuvaa hereni au kujichora mwilini kwa sababu nauheshimu mwili wangu, ndiyo maana nipo kawaida kila wakati,” alifafanua.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...