Thursday, March 3, 2016

TWIGA STARS WASEMA NI KUFA NA KUPONA

Kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars), leo kimefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa kuwakabili timu ya Taifa ya Wanawake kutoka Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kesho Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.
Twiga Stars inayonolewa na kocha mzawa mwanamke, Nasra Juma imekamilisha ratiba yake leo asubuhi kwa kufanya mazoezi mepesi katika uwanja wa Karume ofisi za TFF, huku kocha wake Nasra akisema vijana wake wote wapo katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo huo.
Akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa TFF uliopo Karume, Nasra amesema ana waheshimu Zimbabwe wana timu nzuri, ndani ya miaka minne wameshacheza nao zaidi ya mara nne, mapungu yaliyojitokeza katika michezo iliyopita wamefanyi kazi na hivyo kesho ana imani watafanya vizuri.
Aidha kocha Nasra, amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kesho Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi kuwapa sapoti Twiga Stars katika mchezo huo utakaonza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Naye nahodha wa kikosi hicho Sophia Mwasikili, amesema wachezaji wote wapo katika hali nzuri, wana ana ari na morali ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo wa kesho, na kuwaomba watanzania kuwapa sapoti kwa kujitokeza kwa wingi kuja kuwashangilia uwanjani watakapokuwa wakipeperusha bendera ya Tanzania.
Wapinzani wa Twiga Stars, timu ya taifa ya Zimbabwe wanawasili leo jioni tayari kwa mchezo huo, huku waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Ethiopia wakiwa tayari wameshawasili leo mchana kwa shirika la ndege la Kenya (KQ).

MWAKIFWAMBA AIPA TANO SERIKALINA BETHSHEBA WAMBURA,(RCT)
RAIS  wa  shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifamba,ameiunga mkono Serikali katika juhudi zake za kudhibiti uharamia wa kazi za Filamu .
Akizungumza  jana jijini Dar es Salaam,Mwakifamba alisema kwa muda mrefu wamekuwa na kilio juu ya uharamia wa kazi za Filamu lakini hawakupata msaada lakijni tangu Serikali iwaahidi kudhibiti suala hili tija ya soko la Filamu inaonekana.
“Sisi kama wadau wa tasnia ya filamu tunamini uharamia ukithibitiwa ,tutapata wawekezaji wengi katika kwenye biashara halali ya usambazaji filamu,” .
“Ambao kimsingi utatoa tija ya ajira na kuongeza pato la wadau wanaofanikisha kazi ya filamu kukamilika,”alisema.
Aidha ,Mwakifamba alisema wanaiomba serikali kutolegeza kamba na kufanya zoezi hili kuwa la kudumu kwa maslahi mapana ya kudhibiti mianya yote ya uharamia.
Alisema pia wanaviomba vyombo vya Habari na idara ya polisi kuwaripoti watu wote wanaouza Filamu ya ndani au nje ya nchi isiyokuwa na stika ya TRA.

Wednesday, March 2, 2016

HARUSI TRADE FAIR KURINDIMA MARCH 11Na Humphrey Shao

Maonyesho  makubwa ya urembo na mavazi yanataraji kufanyika mapema mwezi huu katika ukumbi wa Kardnali rugambwa osterbay.

akizungumza na mwandishi  wa makala haya mtayarishaji wa maonyesho hayo Mustafa Hassanali alisema kuwa maonyesho hayo amabyo yatafanyika hapa nchini ikiwa ni mara yake ya saba tangu yaanzishwe yatakuwa na vitu vizuri na vya aina yake.

Mustafa alisema kuwa mwaka huu watu wanaofanya maharusi wamejiandaa kwa uzuri zaidi kuliko watu wanavyodahani hivyo wanatakiwa kufika kwa wingi

BAGAMOYO KUSHUHUDIA MAWE MARCHI 5Na Mwandishi Wetu


BONDIA Seba Temba wa kg 66 kutoka mkoa wa Morogoro anatarajia kupanda ulingoni march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo kupambana na mkali wa mkoa huo wa Pwani Iddi Pialali mpambano uho ambao umeandaliwa na Muhsin Sharif 

promota huyo alisema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine mengi ya mchezo wa ngumi likiwemo la wanawake Joyce Awino kg 64  na Mariam Tembo na Abdallah Pazi kg 76 atakumbana na Georger Dimoso na Flank Lampad kg 69 atavaana na Mwaite Juma wakati bondia kutoka mkoa wa Tanga Jacobo Mganga kg 72

atapambana na Maono Ally

mpambano uho ni rasmi kabisa kwa ajili ya kutoa burudani kwa wakazi wa Bagamoyo mkoa wa Pwani pamoja na vitongoji vyake ambao walikuwa wakisubili burudani hiyo ya mchezo wa masumbwi nchini

nae bondia Seba Temba amejinasibu kwa kujigamba lazima amlaze Iddi Pialali na ndio itakayokuwa njia yake ya mazoezi kabla ya kupambana na bondia Pius Kazaula mpambano utakaofanyika march 27 katika uwanja wa ndani wa taifa siku ya sikukuu ya Pasaka

NGUM KUPIGWA MWANANYAMALA MARCH 3

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA mbalimbali wanatarajia kupmbana siku ya Alhamisi ya March 3 katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala jijini Dar Es Salaam
akizungumza wakati wa utambulisho wa mpambano uho wenye lengo la kuinua vipaji vya mabondia chipkizi na kuendeleza wale ambao wanafanya vizuri katika mchezo wa masumbwi

Mratibu wa mpambano uho Ibrahimu Kamwe 'Big Rght'  amesema kuwa uwo ni mpango maalumu ya kukuza vipaji vya mabondia chipkizi utakaokuwa endelevu mpaka pale watakapo wachuja na kupata mabondia wa kuwaendelez zaidi 

alitaja watakaozipiga siku hiyo kuwa ni Mwinyi Mzengera atakaezipiga na George Geremiya wakati Herman Shekivul akimenyana na Seleman Daud wakati Hassani Mbalale atazidunda na Amos Mohando Kassim Chuma atakumbana na Said Nyonzo uku Shaban Manjoly akipambana na Paul Nachelewa wakati Mbena Rajabu atapimana ubavu na Said Katinko na HashimuChisola atakumbana na Sebastian Mkombozi na Maono Ally atacheza na Amani Juma

katika mchezo uho siku hiyo kingilio kitakuwa ni Tsh;5000/= kwa watu wote

nae Promota wa mpambano uho Abuu Chaka  aliongeza kwa kuseka kuwa wameamua kuwainua vijana kwa ajili ya kuendeleza vipaji vyao hivyo amewataka mabondia wote chipkizi kufanya mazoezi na kujituma kwa ajili ya mashindano mbalimbali yatakayokuwa yakifanyika kila mwanzoni mwa mwezi kwa kuwainuwa vijana hawo nimeamua kujitolea 

hivyo naomba wadau wengine wainge mfano uhu wa kujali michezo pia watoe sapoti mbalimbali kwa ajili ya mchezo wa masumbwi mchezo

WAPINZANI WA TIWGA STARS KUWASILI KESHO

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake ya Zimbabwe, inatarajiwa kuwasili kesho Alhamis mchana wakiwa na msafara wa watu 29, wakiwemo wachezaji 20 pamoja na viongozi 9 tayari kwa ajili ya mchezo wa siku ya Ijumaa dhidi ya wenyeji Twiga Stars uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Zimbabwe watafikia hoteli ya DeMag iliyopo Kinondoni, ambapo jioni watapata fursa ya kufanya mazoezi katika uwanaja wa Azam Complex utakaotumika kwa mchezo siku ya Ijumaa.
Upande wa waamuzi wa mchezo huo wanatrajiwa kuwasili kesho mchana kwa shirikia la ndege la Kenya (KQ) wakitokea nchini Ethiopia, huku kamisaa wa mchezo kutoka Congo DR akiwasili jioni kwa KQ.
Maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika ambapo ulinzi na usalama utakuwepo wa kutosha, tiketi za mchezo huo zitauzwa eneo la uwanja Chamazi siku ya Ijumaa. Viingilio vya mchezo ni shilingi elfu mbili (2,000) kwa mzunguko na shilingi elfu tatu (3,000) kwa jukwaa kuu.
TFF inawaomba wadau, wapenzi wa mpira wa miguu kujitokeza kwa wingi siku ya Ijumaa kuwapa sapoti Twiga Stars katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Cameroon.

MALINZI ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA INFANTINO

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Gianni Infantino kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) mwishoni mwa wiki nchini Uswisi.
Katika barua hiyo, Malinzi amesema TFF ina imani na ahadi zake za kuendeleza mpira wa miguu, na kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ataendelea kushirikiana naye katika kila jambo katika nafasi yake hiyo na kumtakia kila la kheri na mafanikiko mema.

Mdee Waitara wapandishwa kizimbani

Wameshitakiwa kwa kosa moja tu la kumjeruhi Katibu tawala wa jiji la Dar es salaam Bi Theresa Mbando siku ya kuahirishwa uchaguzi wa meya wa jiji la Dar es salaam wa chadema  jijini Dar es Salaam wamepandishwa kizimbani nacwafuasi wao katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu kujibu mashtaka yanayowakabili

Tuesday, March 1, 2016

Magufuli kujenga bomba la mafuta mpaka Uganda

WAZIRI ATOA MOTISHA KWA TWIGA STARS

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa motisha kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake (Twiga Stars) wakishinda katika mchezo wake dhidi ya Zimbabwe unaotarajiwa kuchezwa siku ya Ijumaa Machi 04, 2016 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura alipotembelea kambi ya timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wachezaji wa Twiga Stars, Wambura amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa michezo wamekusanya shilingi milioni 15 ambazo zitatumika kama motisha kwa wachezaji hao.
Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa iwapo timu hiyo itaibuka na ushindi katika mechi yake dhidi ya Zimbabwe kila mchezaji atapata gawio la shilingi laki tatu (300,000) kama motisha na kuongeza kuwa itafanyika hivyo hivyo katika mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Zimbabwe.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa michezo kuzidi kujitokeza na kuisaidia timu hiyo ikiwa ni pamoja na kuhudhuria kwa wingi katika mchezo wa Machi 04, 2016 dhidi ya Zimbabwe utakayochezwa katika uwanja wa Chamazi.
Aliongeza kuwa msaada zaidi unahitajika ili kuiwezesha timu hiyo kukidhi mahitaji yake muhimu,hivyo alitoa wito kwa wadau mbalimbali kutoa michango yao kupitia Twiga Special Fund, Akaunti na: 20110001677 iliyoko NMB tawi la Bank House jijjini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa ameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha Twiga Stars inapata huduma muhimu ikiwemo motisha kwa wachezaji na benchi la ufundi.
Mwesigwa pia amewapongeza wadau wote waliojitolea kusaidi timu hiyo ambapo amesema kujitokeza kwa wadau hao kunaongeza morali ya wachezaji.
Msaada huo wa shilingi milioni 15 umetolewa na wadau watatu ambapo mmoja aliyechangia shilingi milioni 3 aliomba jina lake lihifadhiwe, wengine ni Kampuni ya ASAS shilingi milioni 2 na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) shilingi milioni 10.

PROFESA MAJI MAREFU AWAONGOZA WASANII KUMZIKA MAMA YAKE BANZASTONE

 maji marefu akiongea na zembwela
 Profesa maji marefu akiwa na Ally Choki
 Profesa Maji Marefu akiwa na muumini mwijuma
 Muumini Mwijuma akiwa na Jose Mara
 Profesa Marefu akiwa naondoka makaburini

 profesa maji marefu akianda gari yake

FASHION ONE’s TRENDS and STYLE COMING TO DStv
FASHION ONE’s TRENDS and STYLE
COMING TO DStv
Fashion One launches 1 March across 48 countries in Africa, replacing Fashion TV
February 2016
On 1 March 2016, a wealth of ideas, trends and creativity will be coming to subscribers with the launch of Fashion One on DStv channel 178. Fashion One is well known across the African continent and will now reach an estimated 10 million households and will be available on DStv to Premium, Compact +, Compact,Family and Bomba customers.
Fashion Onecaters to a fashionable and stylish audience with content covering the very latest in entertainment, international fashion, lifestyle news and events. Showcasing a strong portfolio of original programs from reality shows to documentaries, food to travelogues and beauty tips, the channel also covers African markets and captures the essence of local trends and styles.
The channel will debut in March with Style Wars and new seasons of Eco Fashion and Fashion on a Plate. Style Wars is a six-episode long reality series where stylists compete to create original and inventive outfits for commercials and photo shoots. Designed to challenge each person’s versatility, the competition provides and exciting look into this colourful and performance-oriented world. Ngugi Vere, a Zimbabwean-born stylist and creative consultant, currently living in South Africa, will go up against other determined stylists from London, Los Angeles, Australia and New York. The show starts on 3 March and airs every weekend at 12pm (EAT).
When fashion and gastronomy meet, you’ll find Fashion on a Plate Season 2 which sees top chefs and restaurants from around the world using their ingenuity to interpret what ‘fashion on a plate’ means to them. From inception to presentation, we get to see how a simple ingredient is turned into a work of art in this this six-episode docu-series, starting on 21 March at 10pm (EAT), and airs every Monday.
Eco Fashion Season 3 carries on the fight against a world of waste as eco-friendly fashionistas use recycling, repurposing and other innovative techniques to create environmentally sustainable couture. This groundbreaking docu-series will take you on a mind-opening journey into the realm of environmentally sustainable fashion. It starts on 22 March and airs every Tuesday at 11:30pm (EAT).
“We are thrilled about the collaboration with MultiChoice which bring us to the position of number one fashion channel in Africa,” said Fashion One LLC.’s Head of Marketing, Mr. Gorden Li, “the channel will introduce African audiences to fashion like they’ve never seen it before, as well as great stories about local fashion and lifestyles. We look forward to collaborating with the local fashion and entertainment industry to bring these stories to your screens.”
MultiChoice Tanzania acting General Manager, Mr.Francis Senguji, added: “Fashion One will give our DStv customers front row seats to the biggest international fashion shows and runways that they’ve become used to seeing. They’ll also be introduced to a rich blend of local fashion, entertainment and lifestyle shows. Its fashion like you’ve never seen it before.”
For more information log on to www.dstv.com
Ends.


TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...