Friday, March 25, 2016

TAIFA STARS KUWASILI DAR LEO USIKU


Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kinatarajiwa kuwasili leo saa 8 usiku katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. JK Nyerere kikitokea nchini Chad kilipokuwa na mchezo dhidi ya wenyeji jana jioni.
Msafara wa Taifa Stars unaongozwa na mkuu wa msafara ambaye pia ni Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ravia Idarus Faina utaondoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa N’Djamena saa 8 mchana kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia, kabla ya kuunganisha ndege saa 4 usiku tayari kwa safari ya kurejea nyumbani Tanzania.
Stars inarejea nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya wenyeji Chad, bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta katika mchezo uliochezwa uwanja wa Omnisport Idriss Mahaymat Ouya jijini N’Djamena katika mchezo wa kundi G kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017.
Mara baada ya kuwasili jijini Dar es salaam, kikosi cha Taifa Stars kitaingia moja kwa kwa moja kambini katika hoteli ya Urban Rose iliyopo eneo la Kisutu kujiandaa na mchezo wa marudano utakaochezwa siku ya Jumatatu ya Pasaka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Thursday, March 24, 2016

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA OFISI ZA WIZARA HIYO UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE NA KITUO CHA POLISI BUGURUNINaibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani waliopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Waandishi wa Habari wakati wa ziara yake aliyoifanya kutembelea Idara za Wizara hiyo zilizomo katika Uwanja huo.Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro alipotembelea Kituo cha Polisi Buguruni wakati wa ziara yake katika Kituo hicho.Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha (katikati), akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) wakati Waziri huyo alipotembelea Uwanja huo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno.Mkuu wa Ofisi ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Abuu Mvano (kulia), akiongozana  na Naibu Waziri wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), alipotembelea Idara za Wizara hiyo zilizopo katika Uwanja huo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisalimiana na maafisa wa Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara aliyoifanya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.  Katikati ni Mkuu wa wa Ofisi ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Abuu Mvano.Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi, alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kukagua shughuli zinazofanywa na Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege,  ACP Martin Otieno.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...