Friday, April 8, 2016

PICHA ZA WABUNGE WAKIWA KIKAO CHA KUJADILI BAJETIPicha tofauti za Chalse Mwijage akiwa na JICA Katika mkutano wa KAIZEN

 Waziri wa Viwanda na Biashara Chalse Mwijage akizungumza na wandishi wa habari juu ya huduma ya KAIZEN Viwandani Profesa Tetsushi Sonobe Mwakilishi wa wa Kaezen kutoka nchini Japan akitoa Somo kwa waandishi  na wafanyakazi wa Wizara ya Viwanda na Biashara
 Wawakilishi kutoka nchini Japan
Takao Kikuchi kutoka Jica akitoa maelezo mafupi

Tuesday, April 5, 2016

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA YATEMBELEA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI NA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFANaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Kangi Lugola, wakati Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kushoto ni mjumbe mwingine wa kamati hiyo, Juliana Shonza.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu, akiongoza kikao wakati  Kamati hiyo ilipokutana na Viongozi na Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Projest Rwegasira.Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwa katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam wakati Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo. Katikati meza kuu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Adadi Rajabu na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Adadi Rajabu (wa tatu kulia), wakikagua mojawapo ya samani za ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, ambazo zimetengenezwa na Jeshi la Magereza, wakati  Kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba, akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ilipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo. Wa kwanza kutoka kushoto (waliokaa) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira na wa tatu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi Rajabu.Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho wa  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Alphonce Malibiche, akielekeza jinsi ya kutambua taarifa sahihi za mwombaji wa kitambulisho cha Taifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati Kamati hiyo ilipotembelea Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (kushoto) mara baada ya Kamati hiyo kumaliza ziara yake katika  Makao Makuu ya Wizara hiyo na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akiagana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (kushoto), mara baada ya Kamati hiyo kumaliza ziara yake Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya.(Picha na Wizara ya Mambo ya Nchi)

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...