Saturday, April 30, 2016

KHADIJA KOPA;RUNINGA ZIMESHUSHA MUZIKIWA TAARABUMalkia wa muziki wa Taarab nchini Khadija Kopa amesema sababu ambayo inasababisha  soko la muziki wa taarab kushuka na kutochezwa kwa wingi kwenye radio na ruringa ni moja ya sababu kubwa inayoifanya  kuanguka kwa muziki huo, pia wasanii wa taarab kutokwenda na wakati kuwa  mbunifu zaidi kwenye utunzi wa nyimbo.
Akizungumza na MTANZANIA  amesema  kuwa  kwa sasa muziki wa Bongo fleva ndio umeshika nafasi ya kuwa juu kuliko muziki wa taarab na sababu kubwa ni vyombo vya habari na wasanii wa taarab kutokujituma zaidi kwenye utunzi wa mashairi na kujua mashabiki wanataka nini kwa wataki huu.
“Muziki wa taarab unashuka kwa sababu ya vyombo vya habari kuwapapromo zaidi muziki wa kizazi kipya ukwel muziki wa taarab bila vyombo  vya habari hatuwezi kufika popote, hapa tulipofikia sisi wengine mpaka tunazeeka ni nguvu za vyombo za habari bila waotusingefika hapa tulipo sasa,” alisema Khadija Kopa.
Aliongezea na kusema kuwa anaomba serikali kuwasaidia kuwashika watu wanaonakili kazi zao na kuzipiga kwenye masherehe mbalimbali huku wao kukosa show.

PICHA;Mshindi wa Tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika Tasnia ya Habari Mwaka 2016, Rose Haji MwalimuMATUKIO KATIKA PICHA YA TUZO ZA UMAHIRI WA UANDISHI WA HABARI EJAT

 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi akiwa na Katibu wa Baraza la Habari Tanzania Kajubi Mukajanga na Mkurugenzi wa TMF Ernest Sungura
 Majaji wa EJAT, Jesse Kwayu na Mzee Ndimara Tegambwage wakibadilishana mawazo
 Rais wa MCT, Jaji Thomas Mihayo
 Jopo la Majaji likiwa limesimama kwa Pamoja
 Majaji wa EJAT , Nathan Mpangala  na Mzee Juma Dihule
 Mgeni rasmi wa Shughuli hiyo kamishna wa tume ya Haki za BINADAMU
 Nora Damiani akikabidhiw atuzo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa TCRA, Innicent Mungi
 Mzee Ndimara Tegambwage akizungumza jambo na Hadhira
 Mkurugenzi wa TBC Taifa, Susani Mungi akikabidhi Tuzo kwa mshindi wa habari za Uchunzi Televisheni, Frank Bahati wa TBC
 Mkurugenzi wa TBC Taifa, Susani Mungi akikabidhi cheti kwa msindi wa pili Habri za Uchunguzi Televisheni, Khamisi Suleimani


 sma mahela kipokea tuzo yake
 Mpiga picha bora wa magazeti Robert Okanda akipokea Tuzo
 Robert Okanda kionyesha tuzo yake juu
 Said Michael (Wakudata) akiwa na Abdul Kingo
  Said Michael (Wakudata) akipokea tuzo ya mchora katuni bora Mshindi wa jumala Frank Bahati akipokea cheki yake
Friday, April 29, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI KATIKA NCHI ZA UKANDA WA MASHARIKI NA KUSUNI MWA AFRIKA LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua mkutano kuhusu kuwezesha wanawake kiuchumi katika nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Mkutano huo umeandaliwa na Jopo la Ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon alilolituewa Mwanzoni mwa huu, kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi ifikapo 2030. Umefanyika Leo April 29,2016 Hyatt Hotel Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Jopo la ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kuwezesha wanawake kiuchumi Baada ya kufungua mkutano kuhusu kuwezesha wanawake kiuchumi katika nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Mkutano huo unazungumzia kuhusu kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi ifikapo 2030. Umefanyika Leo April 29,2016. (Picha na OMR)

KAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU KUKETI KESHOKAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU

Kikao cha Kamati ya Rufaa ya Nidhamu kitafanyika Jumamosi Aprili 30, 2016 kuanzia saa 4.00 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kitajadili rufaa za timu, makocha, viongozi na wachezaji waliokata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Nidhamu baada ya kamati hiyo kuwatia hatiani na kuwaadhibu kwa makosa ya kupanga matokeo ya michuano ya Ligi Daraja la Kwanza.

Rufaa zitakazojadiliwa kwenye kikao hicho ni za:
1.   Timu ya Geita Gold
2.   Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Geita Gold FC
3.   Denis Richard Dioniz - Kipa wa Geita Gold
4.   Fatel Rhemtullah – Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora
5.   Saleh Mang’ola – Mwamuzi wa Soka wa Mkoa wa Dodoma
6.   Timu ya Soka ya Polisi Tabora
7.   JKT Oljoro Fc ya Arusha
8.   Yusufu Kitumbo – Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora


MECHI ZA LIGI BARA

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendeleo mwishoni mwa wiki hii kwa michezo sita itakayofanyika kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Mabingwa wanaotetea taji hilo, Yanga ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa Toto Africa katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza huku Coastal Union ikipambana na African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Mechi nyingine zitakuwa ni kati ya Mwadui FC watakaokuwa wenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mwadui, Shinyanga wakati Mbeya City watakuwa wageni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani Morogoro na katika Dimba la Sokoine jijiji Mbeya Tanzania Prisons itaumana na JKT Ruvu katika mfululizo wa mechi za ligi hiyo.

Jumapili Simba itaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Michezo yote itaanza saa 10.000 jioni na kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni ya Azam.


KAMATI YA NIDHAMU SASA KUKAA MEI 3, 2016
Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kilichopangwa kufanyika Jumapili, Mei Mosi 2016, kimeahirishwa hadi Jumanne Mei 3, mwaka huu.

Sababu za kuahirisha kikao hicho ni kwamba baadhi ya wajumbe wamepata udhuru hivyo wangeshindwa kuhudhuria kikao hicho kitakachofanyika
jijini Dar es Salaam kupitia mashauri mbalimbali yaliyowasilishwa.  Wafuatao kesi zao sitasikilizwa katika kikao hicho:

(i)          John Bocco – Azam FC
(ii)        Shomari Kapombe – Azam FC
(iii)       Aishi Manula – Azam FC
(iv)       Amissi Tambwe – Yanga SC
(v)         Donald Ngoma  - Yanga SC
(vi)       Paulo Jinga – JKT Rwamkoma FC
(vii)     Kipre Tchetche – Azam FC
(viii)    Abel Katunda – Transit Camp
(ix)       Zephlyn Laurian – JKT Rwamkoma FC
(x)        Idrisa Mohamed – JKT Rwamkoma
(xi)       DR. Mganaga Kitambi (Daktari) – Coastal Union
(xii)     Herry Chibakasa – Friends Rangers
(xiii)   Ismail Nkulo – Polisi Dodoma
(xiv)    Said Juma – Polisi Dodoma
(xv)     Idd Selaman – Polisi Dodoma
(xvi)    Edward Amos – Polisi Dodoma
(xvii)  Stewart Hall (Kocha)– Azam FC

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


Picha tofauti za sura ya Khadija Kopa

 Khadija Kopa
  Khadija Kopa
  Khadija Kopa
  Khadija Kopa
  Khadija Kopa
  Khadija Kopa
  Khadija Kopa
  Khadija Kopa
  Khadija Kopa
  Khadija Kopa
  Khadija Kopa
  Khadija Kopa
  Khadija Kopa
  Khadija Kopa
  Khadija Kopa
 Khadija Kopa

WADAU WA MITINDO NA UREMBO WAALIKWA KUSHIRIKI MAONESHO UCHINA

Makamu wa Rais wa Maonyesho ya Wachina Maharufu kama China International Beauty Expo African Hall,Rex Chan akizungumza na Waanddishi w...