Friday, May 13, 2016

LUHWAVI AKAGUA UHAI WA CHAMA KWENYE MASHINA YA CCM WILAYANI KIHABA

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Lihwavi akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM shina namba nne, la mjumbe Leticia Deodatus,  Kibaha mkoa wa Pwani, akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama, jana. (Picha na Bashir Nkoromo).

--
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajabu Lhwavi akisalimiana na Mjumbe wa Shina namba tisa, tawi la KKKM, Kata ya Picha ya Ndege, Wilayani Kibaha mkoa wa Pwani, Bibie Lukemo, alipotembelea shina hilo, jana, kukagua uhai wa chama akiwa katika ziara ya kikazi wilayani humo. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Picha ya Ndege. Mwalimu Mohammed Lukemo. (Picha na Bashir Nkoromo).
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajabu Luhwavi akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo maalum ambalo viongozi wanaotembelea shina namba tisa, tawi la KKKM, Kata ya Picha ya Ndege kupanda mti kama huo, alipofika kwenye shina hilo, jana kukagua uhai wa Chama. (Picha na Bashir Nkoromo).
 Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo maalum ambalo viongozi wanaotembelea shina namba tisa, tawi la KKKM, Kata ya Picha ya Ndege kupanda mti kama huo, alipofika na Naibu Katibu Mkuu wa CCM- Bara, Rajabu Luhwavi, kwenye shina hilo, jana kukagua uhai wa Chama. (Picha na Bashir Nkoromo).

 Mjumbe wa Shina namba tisa, tawi la CCM KKKM, kata ya Picha ya Ndege Kibaha mkoa wa Pwani, Bibie  Lukemo, akisoma taarifa ya shina hilo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi alipotembelea shina hilo kuimarisha na kukagua uhai wa chama jana. (Picha na Bashir Nkoromo).

 Wanachama wa CCM, Shina namba tisa, tawi la CCM KKKM kata ya Picha ya Ndege Kibaha mkoa wa Pwani, wakionyesha kadi zao za CCM, walipokuwa wanamshangilia Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi alipotembelea shina hilo jana akiwa katika ziara ya kuimarisha na kukagua uhai wa Chama. (Picha na Bashir Nkoromo).
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi na Katibu wa CCM mkoa wa Pwani, Joyce Masunga, wakikagua daftari la wageni, walipokuwa nyumbani kwa amjumbe wa shina namba tatu, Tawi la Twende Pamoja, Kata ya Sofu, wilayani Kibaha mkoa wa Pwani,  Gasper Gama (kulia), Luhwavi alipotembelea shina hilo kukagua na kuimarisha uhai wa Chama, jana. (Picha na Bashir Nkoromo).

Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Lihwavi akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM shina namba tatu, tawi la Twende Pamoja, Kata ya Sofu, wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani, akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama, jana. (Picha na Bashir Nkoromo).

AZAM YASHUSHA MAKOCHA WAWILI KUTOKA SPAIN

 Mkocha Mkuu Mpya wa Timu ya Azam FC, Zeben Hernandez (katikati) akiwa ameambatana na msaidizi wake, Rayco Gacia (kushoto) wakiwa wamewasili  katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana wakitokea nchini Hispania (kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Klabu hiyo, Sadi Kawemba.
LIPUMBA AMVAA MAGUFULI SAKATA LA SUKARI

 Rais Magufuli alitoa amri ya kuzuia kuagiza sukari toka nchi za nje tarehe 18 Februari wakati alipokuwa anawashukuru waandishi wa habari, wasanii na makundi mbalimbali yaliyoshiriki kwenye kampeni za Mgombea Urais wa CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015. Katika hafla hiyo alieleza viwanda vya sukari vina bidhaa hiyo na wanashindwa kuuza kwa sababu ya sukari iliyoagizwa kutoka nje. Aliwashutumu wafanyabiashara kuwa wanaagiza sukari ambayo inakaribia kwisha muda wake wa kutumiwa na binadamu na wanaileta nchini na kuiweka kwenye viroba vipya. Alimuagiza Waziri Mkuu asimamie zoezi hilo na yeye ndiye atowe vibali vya kuagiza sukari.
Baada ya tamko hilo la Rais, serikali ilitangaza bei elekezi ya shilingi 1800 kwa kilo nchi nzima. Hata hivyo serikali haikufafanua bei ya kiwandania ni shilingi ngapi? Na bei ya jumla katika kila eneo ni shilingi ngapi?
Waziri Mkuu akihitimisha hotuba yake ya Bajeti, alieleza kulingana na takwimu za serikali kuna tani 37,000 zilizomo nchini. Aliagiza Maofisa biashara katika halmashauri za wilaya wafanye ufuatiliaji katika maduka kuona sukari haifichwi na haiuzwi kwa bei ya juu. Bidhaa hii inapaswa kuuzwa kwa bei elekezi ili wananchi wapate sukari wakati wowote watakapoihitaji.
Sukari imeadimika na inauzwa kwa bei ya juu. Vyombo vya habari vimetoa taarifa kuwa kuna maeneo sukari inauzwa zaidi ya shilingi 4000 kwa kilo.
Vyombo vya Habari vimemnukuu Rais Magufuli kuwa “ametangaza kupambana na wafanyabiashara wasiozidi 10 waliohodhi biashara ya sukari, akisema ndiyo wameshiriki kuua viwanda na kujitajirisha.”
Taarifa ya Ikulu ya tarehe 6 Mei 2016 inaeleza “Dkt. Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuwafuatilia wafanyabiashara wanaofanya njama za kuficha sukari na kusababisha upungufu wa bidhaa hiyo, na ameapa kuwa serikali yake itawachukulia hatua kali watakaobainika kufanya hivyo.
Pamoja na kutoa maagizo hayo Rais Magufuli amewaondoa shaka watanzania juu ya upungufu wa sukari, kuwa serikali imeagiza sukari kutoka nje ya nchi ambayo itasambazwa kwa wananchi kwa bei nafuu ili kufidia upungufu uliopo.
"Wale wote waliokuwa wameficha sukari waiachie, wasipoiachia sukari, huwezi kuificha kama sindano, nimeshaagiza vyombo vya dola, vikague magodown yote, atakayekutwa na sukari ameificha, yule ni mhujumu uchumi kama wahujumu wengine, asije akanilaumu, asijee-akanilaumu, na ninasema kwa dhati, wewe mfanyabiashara uliyepata nafasi ya Tanzania kuleta bidha za sukari, halafu unanunua unakwenda kuficha ili kusudi wazee hawa wahangaike, ili mwezi mtukufu wa Ramadhani utakapoingia watu wakose sukari, dawa yao ninayo" Amesema Rais Magufuli.
Katika Hotuba ya Bajeti Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ameeleza kuwa “mahitaji ya sukari nchini ni wastani wa tani 420,000 kwa matumizi ya kawaida na tani 170,000 kwa matumizi ya viwandani. Hadi kufikia Machi 29, 2016 uzalishaji umefikia tani 290,112 ikilinganishwa na matarajio ya tani 288,802 katika mwaka 2015/2016.” Viwanda vya Tanzania havizalishi sukari ya matumizi katika viwanda vya vinywaji na vyakula. Kwa hiyo sukari iliyotarajiwa kuagizwa toka nje ni tani 131,198 za sukari ya matumizi ya kawaida na tani 170,000 za sukari ya matumizi ya viwandani. Jumla tani 301,198.
Wakati Rais anazungumza na wapiga debe wake wa kampeni alieleza kuwa viwanda vya sukari vinashindwa kuuza sukari kwa sababu ya sukari iliyoagizwa kutoka nje. Hivi sasa viwanda vinaeleza havina sukari. Vitaanza uzalishaji mwezi wa Julai. Rais amesisitiza sukari imefichwa kwenye magodown.
Hata hivyo kitabu cha hotuba ya bajeti ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kinafafanua hali ya sukari ilivyokuwa hadi kufikia tarehe 29 Machi 2016. Wazalishaji walikuwa na tani 17,996. Wasambazaji wakubwa na wa kati tani 14,652. Jumla tani 32,648.
Ikiwa matumizi ya kawaida ya sukari kwa nchi nzima ni tani 420,000 kwa mwaka maana yake kila mwezi tunatumia tani 35,000. Ili pasiwepo na ukosefu wa sukari, wafanya biashara wa sukari wanatarajiwa wawe na alau hifadhi ya sukari ya kutosha mwezi mmoja wa mahitaji huku wakisubiri sukari nyingine kutoka viwandani au nje ya nchi.
Msimu wa uzalishaji sukari viwandani umemalizika. Mtibwa Estate walifunga Kiwanda tarehe 16/01/2016,  Kilombero tarehe 26/02/2016, TPC tarehe 15/03/2016, Kagera Sugar tarehe 11/04/2016.
Ikiwa mwezi Aprili, nchi imetumia tani 35,000, akiba ya sukari iliyokuwepo mwishoni mwa mwezi Machi itakuwa imemalizika. Sukari itakayokuwepo ni ile iliyoagizwa kutoka nje na kuingia nchini.
Kwa kutambua hali hii ya upungufu wa sukari nchini, mwishoni mwa mwezi Machi 2016, Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilimuomba Rais Magufuli kuruhusu kutoa vibali vya kuagiza sukari ili kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo.
Lakini Rais ameishaeleza viwanda vyetu vuna sukari nyingi. Sukari isiagizwe toka nje.  Ni wazi Maafisa wa Bandari, Bodi ya Sukari na Mamlaka ya Kodi watasita kuruhusu upakuaji wa sukari iliyoagizwa hata kabla ya tamko la Rais.
Wakuu wa mikoa, Wakuu wa Wilaya, Polisi Takukuru wote wanashiriki kwenda kubaini sukari iliyofichwa. Wanaenda na vyombo vya habari. Shehena kubwa iliyokamatwa ilikuwa tani 5000. Hata hivyo “licha ya kukamatwa sukari inayodaiwa kufichwa, imebainika kuwa baadhi ya waliohifadhi hawakuwa wameificha, bali walikuwa wanakamilisha taratibu za kodi na vibali.”
Pamoja na msako mkali sukari iliyokamatwa nchi nzima haifiki tani 10,000. Lakini kwa kuwa Rais ameishasema sukari imefichwa, viongozi nao wanarudia kauli hiyo kuwa sukari imefichwa yasije yakawakuta yaliyomsibu Mama Anna Kilango Malecela.
Soko la Dunia
Bei ya sukari katika soko la dunia mwezi Agosti 2015 ilikuwa dola za Marekani 250 kwa tani moja. Kama dola moja ni shilingi 2000, tani moja ya sukari iliuzwa shilingi laki tano, sawa na shilingi 500 kwa kilo moja. Ukiongeza gharama za usafiri kilo moja ya sukari itafika Dar es Salaam kwa gharama isiyozidi shilingi 600 kwa kilo. Ukiweka ushuru wa forodha na VAT pamoja na faida ya wauzaji, kilo moja ingeweza kuuzwa chini ya shilingi 1000.
Bei imepanda kidogo. Mwezi Aprili tani moja ilikuwa inauzwa kwa wastani wa dola za Marekani 340. Tukichukua thamani ya dola ni shilingi 2200 na gharama za usafiri ni asilimia 20. Gharama ya tani moja ya sukari ni mpaka Dar es Salaam ni shilingi 763,000 kwa tani. Gharama ya kuagiza sukari pamoja na kulipa ushuru wa fordha na VAT haitazidi shilingi 1100. Sukari ya kutoka nje inaweza kuuzwa kwa shilingi 1250/- – 1500/-
Shirika la Chakula Duniani – FAO na Shirika la Uchumi na Uhirikiano wa Maendeleo - OECD linakadiria bei ya sukari katika soko la dunia itakuwa kati ya dola 350 na 390 kwa tani moja katika miaka ya 2016 – 2024.  Hivi sasa viwanda vyetu vina gharama kubwa za uzalishaji. Haviwezi kuhimili ushindani wa bei ya sukari inayozalishwa Brazil. Isitoshe soko la sukari la Ulaya na Japan linalindwa na nchi hizo kuwannfaisha wakulima.  Bei ya sukari nchini Hata Marekani inalinda soko lake la sukari haidhuru kwa kiasi kidogo ukilinganisha na Japan na Ulaya.
Taratibu za kodi au kuweka quota ya sukari itakayoagizwa toka nje zinaweza kutumiwa kulinda viwanda vya ndani. Serikali iwaeleze wananchi ukweli kuwa gharama ya kulinda viwanda vya ndani ni bei ya juu ya sukari ukilinganisha na bei ya soko la dunia. Kwa sababu ya tofauti kubwa ya bei kuagiza sukari toka nje na kuiuza nchini kuna faida kubwa.
Kugawa vibali vya kuagiza sukari bure kunaweka mianya ya rushwa. Serikali inaweza ikauza kwa mnada leseni za kuagiza kiasi cha sukari ya kuziba pengo la uzalishaji wa ndani. Kampuni zinazozalisha sukari zinaweza kushiriki katika mnada huo. Makampuni yaliyoshinda mnada na kapata leseni ndiyo peke yake yatakayoruhusiwa kuagiza sukari.
Maamuzi ya Rais
Taarifa ya Wizara ya Kilimo ya Hali halisi ya sukari inaonesha wazi hapakuwa na sababu za msako wa sukari iliyofichwa. Nina wasiwasi Rais hakushauriana na watendaji wake Bodi ya Sukari na Wizara ya Kilimo kabla ya kuamua kuzuia uagizaji wa sukari toka nje wakati akizungumza na wapiga debe wake wa kampeni. Hafla ile haikustahiki kutolea maamuzi kuhusu masuala ya sukari. Ni vyema Rais awape fursa taasisi na Wizara husika kutekeleza majukumu yao badala ya yeye kufanya maamuzi katika majukwaa ya siasa.
Sheria haimpi mamlaka Rais au serikali kupanga bei ya sukari. Bei elekezi haina nguvu za kisheria lakini pia inawachanganya wananchi na wafanya biashara. Kama bei elekezi ni bei ya reja reja nchi nzima, bei elekezi ya viwandani na ya jumla ni ipi?
Vitisho na viapo vya Rais dhidi ya Wafanya biashara havijengi taswira ya serikali kuithamini na kuishawishi sekta binafsi kuwekeza nchini Tanzania. Kauli za Rais zilisisitiza kuwa sukari iko nyingi nchini na imefichwa na wafanya biashara wachache. Takwimu za Wizara ya Kilimo zinaonesha kuwepo kwa uhaba wa sukari.
Vitisho na ubabe wa Rais vinaweza kuwaogopesha Mawaziri na Watendaji serikalini wasimueleze bayana hali halisi. Kauli za kufichwa kwa sukari zinarudiwa na Wakuu wa Mikoa na hata vyombo vya habari pamoja na kwamba hakuna ushahidi wa kufichwa kwa sukari. Sukari kuwekwa kwenye hakumaanishi kuwa umefichwa.
Rais Magufuli aombe ushauri kuhusu changamoto na taratibu za kujenga uchumi wa soko shirikishi. Uzoefu wa Rais Mkapa wa kujenga utawala wa serikali unaweza ukamsaidia.
Mimi binafsi nilivutiwa na hotuba ya Rais alipozindua Bunge. Nia yake ya matumizi mazuri ya fedha umma, ukusanyaji wa mapato na mapambano dhidi ya rushwa ni mambo yamewavutia Watanzania wengi. Hata hivyo taratibu za kiutendaji na maamuzi ya sera kwenye majukwaa ya siasa vinanipa wasiwasi mkubwa. Ninakumbuka andiko la mwana habari maarufu baada ya uteuzi wa Mhe. John Pombe Magufuli kuwa Mgombea Urais wa CCM aliyeuliza Nani atakayemfunga gavana Rais Magufuli?


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu suala la kuadimika kwa sukari nchini. Kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu CUF Taifa, Bonifasia Mapunda na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Abdull Kambaya

SEKTA YA SHERIA KUCHANGIA UTEKELEZAJI DHANA YA KUIMARISHA VIWANDA NCHINI.


Frank Mvungi-Maelezo.
Serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 inatarajia kufanya mapitio katika sheria mbalimbali ili kutoa mapendekezo yatakayowezesha kufanyika kwa marekebisho  au kutungwa kwa sheria mpya kulingana na mahitaji ya sasa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na afisa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria  Tanzania Bw. Hemed Lusungu wakati wa Mkutano na vyombo vya Habari uliolenga kutoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo.
Akifafanua  Lusungu amesema kuwa Sheria zitakazofanyiwa utafiti ili ziboreshwe na kuendana na Kasi ya Serikali ya awamu ya Tano ni sheria za uwekezaji (Review  of the legal frame work Governing Investiment for viable economic growth).
“Tunataka sheria katika eneo la Uwekezaji ziendane na dhana ya mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli inayolenga kukuza viwanda vya ndani hivyo ni lazima tutazame eneo hili ili kuwa na sheria zitakayowezesha suala hili” alisisitiza Lusungu.
Akizungumzia mapitio katika sheria za Usafirishaji Lusungu amesema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na sheria zinazokidhi mahitaji ya sasa hivyo utafiti wao utatoa mapendekezo ili kulinda haki za wasafiri na wasafirishaji.
Alisema faida za Tafiti zinazofanywa na Tume hiyo ni kusaidia kwa kiasi kikubwa kuchochea marekebisho ya sheria mbalimbali na pia kusaidia kutungwa kwa sheria mpya kulingana na mahitaji ya wakati akitolea mafano sheria ya Ununuzi wa Umma sura ya 410 .
Aliongeza kuwa sheria hiyo imekuwa ikilalamikiwa kurefusha mchakato wa manunuzi na kufanya bei ya bidhaa au huduma kuwa kubwa.
Kwa kuzingatia umuhimu wa Sheria hiyo Tume imeshafanya mapitio katika maeneo husika na kutoa mapendeklezo ambayo yataondoa kasoro zilizokuwepo awali.

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria na ilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria, Sura ya 171.
Majukumu ya tume kama yalivyoainishwa katika kifungu cha 4 (1),(2) na (4) Cha sheria ya Tume ni kufanya mapitio, utafiti na kutathmini maeneo au mfumo wa sheria husika na kutoa mapendekezo kwa Lengo la kuiboresha.

DIAMOND ALISIMAMISHA BUNGE

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond’, jana amelisimamisha Bunge baada ya kutambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuwa ni moja ya wageni waliohudhuria bungeni.
Diamond ambaye alikuwa ameambata na wageni wake kutoka kundi la Mafiki Zolo la nchini Afrika Kusini, baada ya kutambulishwa wabunge walishindwa kuzuia hisia zao na kujikuta wakimshangilia kwa nguvu mwanamuzi huyo.
Wasanii hao ambao waliingia bungeni kwa mwaliko wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye.
“Waheshimiwa wabunge kuna tangazo la wageni hapa, leo tumetembelewa na wageni mashuhuri humu ndani, sio wengine ni wanamuziki wa kundi la Mafikizolo.
“Lakini hawa wameongozana na mwenyeji wao, kijana wetu anayeitangaza nchi huko duniani, wapo na Nasib Abdul au Diamond,” alisema Spika Ndugai
Spika alisema kwamba mbali na wasanii hao pia Diamond amekuja na Meneja wake Babu Tale.
Baada ya tangazo hilo, ukumbi wa Bunge ulilipuka kwa furaha baada ya wabunge, wageni na waandishi wa habari waliokuwepo ukumbini hapo kugeuka upande aliokuwepo mwanamuziki huyo ili wamuone.
Nderemo hizo zilidumu kwa dakika mbili hali iliyosababisha baadhi ya shughuli za Bunge sitishwa kwa muda huku waziri Nape akicheka na kushangilia.
“Ujio huu wa Diamond unatoa hamasa kwamba kuna kitu leo jioni kinafanyika, tunaomba waziri wa habari atutaarifu ili tujumuike pamoja,” alisema Spika Ndugai.
Baada ya maelezo hayo Bunge liliendelea na shughuli zake ambapo wabunge walikuwa wakichangia hoja kwenye Hotuba ya bajeti

CCM ZANZIBAR YAKANUSHA UTAPELI

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimelaani vikali tabia ya baadhi ya watu wanaotumia vibaya jina la Chama hicho kuwatapeli wananchi kutoa fedha ili wapatiwe nafasi za ajira katika Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) jambo ambalo sio sahihi.

Kimewataka wafuasi wa Chama hicho na wananchi kwa ujumla kuacha tabia ya kuwaaminisha watu  kwamba CCM inatoa nafasi mbali mbali za ajira kwani kufanya hivyo ni kuwagombanisha viongozi na wananchi wao.

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai alisema Chama hicho hakihusiki na utoaji wa ajira ya aina yoyote, hivyo watu wanasambaza utapeli huo kwa njia ya simu na mitandao ya kijamii lengo lao ni kuchafua taswira njema ya chama hicho.

Akifafanua zaidi Ndugu Vuai amesema suala la ajira katika taasisi za kiserikali na binafsi zinazolewa kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa hasa baada ya kutolewa matangazo maalum kulinga na nafasi za ajira zilizopo na sio kutumia simu za mkononi kuwapigia watu ili waweze kutoa fedha kwa ajili ya kuwapatiwa ajira hizo.

“Nimepigiwa simu nyingi na baadhi ya watu wangu wa karibu wakiniuliza juu ya taarifa za Chama kuwa kuuza nafasi za ajira, taarifa ambazo nimezipokea kwa mshangao mkubwa kwani ndani ya chama chetu hakuna utaratibu huo” na kuongeza kusema kwamba “nawataka wananchi kuwa macho na makini na matapeli wanaotumia hila tofauti kuwaadaa watu kwa nia ya kujipatia fedha kwa njia za 
udanganyifu”. Alisisitiza Vuai.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar, alitoa wito kwa wananchi kuwa makini na matapeli hao na mtu yeyote atakayepigiwa simu na kuambiwa atoe kima chochote cha fedha kwa lengo la kupatiwa ajira na CCM asikubali kufanya hivyo na badala yake atoe taarifa haraka katika vyombo vya dola, ili sheria ichuke mkondo wake.

Aliwasihi wananchi kuendelea kuamini  kwamba CCM ni Chama kilichokomaa kisiasa na uzoefu mkubwa wa kusimamia demokrasia ya kweli, usawa, haki, utawala bora, a hivyo hakiwezi kujihusisha na vitendo viovu kwa jamii.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM alisisitiza kua; suala la ajira za JWTZ, Idara Maalum za SMZ na zile za Taasisi nyengine za seriikali, zote hizo zinatolewa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW).
Alisema kuwa haiwezekani hata kidogo Chama hicho (CCM) kitowe ajira na kuongeza kuwa taarifa hizo zinazosambazwa na watu ni za kitapeli na zinalenga kuchafua jina la Naibu Katibu Mkuu huyo pamoja na CCM kwa jumla.
Aliwaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo na wawe macho na utapeli wa aina hiyo uliozagaa Zanzibar na maeneo mengine nchini, kwani unafanywa na wapinga maendeleo ya CCM na Taifa kwa jumla.

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA UGANDA YOWERI KAGUTA MUSEVENI NCHINI UGANDARais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni jijini Kampala mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uapisho wa Rais Museveni.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Mei, 2016 amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni muda mfupi baada ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais huyo iliyofanyika katika uwanja wa Kololo Jijini Kampala.
Katika Mazungumzo hayo Rais Magufuli amempongeza Rais Museveni kwa kuapishwa kuwa Rais wa Uganda kwa kipindi kingine cha miaka 5 na kumhakikishia kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi Uhusiano, ushirikiano na udugu wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo.
Viongozi hao pia wamezungumzia mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima (Ziwa Albert) nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania ambapo pamoja na kuishukuru Uganda kwa uamuzi wake wa kuamua bomba hilo lipitie Tanzania, Rais Magufuli amemshauri Rais Museveni kufupisha muda wa ujenzi wa mradi huo, kwa kutumia mbinu inayojumuisha usanifu na ujenzi (Design and Construct method) na kutumia wakandarasi wengi watakaogawanywa katika vipande tofauti badala ya kutumia mkandalasi mmoja.
"Nashauri tutumie mbinu ya usanifu na ujenzi pamoja, hii ni njia ya haraka zaidi, na pia tugawe vipande vya ujenzi kwa njia yote ya bomba la mafuta yenye urefu wa kilometa 1,410 tunaweza kuwa na Wakandarasi watano mpaka sita ambao watatumia njia hiyo mpya ya usanifu na ujenzi.
"Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumepunguza muda utakaotumika kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta, inaweza hata kuchukua mwaka mmoja tu" Amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo faida za mradi huo wa mafuta zitaanza kupatikana mapema badala ya kusubiri miaka miwili au mitatu ijayo, na kwamba hiyo itakuwa inaendana na kauli mbiu yake ya "Hapa Kazi Tu"
Pia Rais Magufuli amemshukuru Rais Museveni kwa uamuzi wa nchi hiyo wa kuipa Tanzania umiliki wa asilimia 8 katika mradi huo wa bomba la mafuta.
Kwa upande wake Rais Museveni amesema amefurahishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo, na pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake kubwa ambazo amezifanya katika mapambano dhidi ya rushwa nchini Tanzania.
"Napenda kasi yako ya uongozi, napenda jinsi unavyopambana na rushwa, kwa sababu rushwa ilikuwa inazaa matatizo mengine kama vile ucheleweshaji wa mizigo bandarini na vikwazo vya mpakani, hivyo nakupongeza sana kwa hilo" Amesema Rais Museveni.
Katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais Museveni iliyofanyika kabla ya mazungumzo hayo, pamoja na Rais Magufuli viongozi wengine kutoka Tanzania waliohudhuria ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa na Mkewe Mama Salma Kikwete na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU
Kampala
12 Mei, 2016Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni jijini Kampala mara baada ya kumaliza mazungumzo yao nchini Uganda. PICHA NA IKULU
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, WASANII NA MICHEZO, MHESHIMIWA JOSEPH OSMUND MBILINYI (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI KUHUSU BAJETI YA WIZARA HIYO KWA MWAKA WA FEDHA 2016/17

1.   UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,kwa mujibu wa kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, napenda kuchukua fursa hii kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Mheshimiwa Spika, kabla sijawasilisha maoni hayo, napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia uhai na afya njema na kuniwezesha kusimama mbele ya bunge hili kufanya kazi hii. Napenda pia kumshukuru Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe (Mb) kwa kuniteua tena kuwa Waziri Kivuli katika Wizara hii. Aidha, namshukuru Naibu Waziri Kivuli wa Wizara hii, Mheshimiwa Devotha Minja (Mb); na wabunge wote wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa michango yao na ushirikiano mkubwa walionipa katika maandalizi ya hotuba hii.

Mheshimiwa Spika, mwisho lakini sio kwa umuhimu, napenda kuwashukuru sana wana-Mbeya kwa kuendelea kuniamini. Mwaka 2010 wana Mbeya waliingia kwenye historia ya dunia kwa kunichagua mbunge wao na hivyo kunifanya kuwa msanii wa kwanza wa muziki wa Hip Hop duniani kuwa Mbunge.  Aidha, mwaka 2015 wameendelea kunichagua kuwa mbunge wao kwa kunipigia kura nyingi za kishindo na hivyo kunifanya kuweka rekodi ya mbunge aliyechaguliwa kwa kura nyingi kuliko wote katika bunge hili (The Most Voted MP). Nawashukuru sana wana mbeya wenzangu – nasema asanteni sana.

Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo, sasa naomba nianze kutoa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu bajeti ya wizara hii.

2.   UHURU WA HABARI NA UTAWALA WA KIDEMOKRASIA
Mheshimiwa Spika, bila kuathiri misingi ya utawala wa sheria na chaguzi huru na za haki katika utawala wa kidemokrasia; msingi mwingine wa utawala wa kidemokrasia ni haki na uhuru wa aina mbalimbali (‘combinatorial freedoms and rights’) kwa mfano uhuru na haki ya kukusanyika (freedom of assembly), uhuru na haki ya kuabudu (freedom of worship), uhuru na haki ya kutoa maoni (freedom of speech), uhuru na haki ya kupata habari (freedom of press) nk.

Mheshimiwa Spika, msingi mmojawapo katika hiyo niliyotaja unapoondolewa, utawala ule unakuwa umekosa sifa zinazotosheleza kuitwa ‘wa kidemokrasia’.

Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu wa misingi hii ya utawala wa kidemokrasia, nchi za kidemokrasia duniani zimeweka hati ya Haki za binadamu   (Bill of Rights) katika Katiba zao. Kwa Tanzania, sehemu yote ya Tatu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazungumzia kwa kirefu juu ya haki za binadamu na uhuru wa aina mbalimbali.

Mheshimiwa Spika,matendo yoyote yanayofanywa na serikali yoyote duniani ya kuminya uhuru na haki za binadamu zilizotajwa na Katiba za nchi husika, ni dalili za dhahiri za utawala usiozingatia misingi ya kidemokrasia na kwa maneno halisi ni utawala wa ki-imla (dictatorship regime).

Mheshimiwa Spika, wanazuoni wa masuala ya uhuru wa habari wanasema kwamba; “every dictator dislikes free media”[1] yaani kila dikteta hapendi vyombo huru vya habari. Kutokana na hali hiyo, jambo la kwanza ambalo hufanywa na utawala wa ki-dikteta ni kuminya uhuru na haki ya kupata na kutoa habari.
Mheshimiwa Spika, Serikali ya awamu ya tano tayari imeshaanza   vibaya kwa kuikanyaga haki na uhuru wa habari. Kwanza, tofauti na ukandamizaji wa uhuru wa habari  tuliozoea wa kufungia magazeti yanapoandika mambo ya kuikosoa Serikali; Safari hii,  Serikali kwa  mara ya kwanza katika historia ya Tanzania,  imefuta moja kwa moja usajili wa gazeti binafsi la Mawio kwa kipindi cha chini ya miezi sita toka imeingia madarakani. Aidha, kwa kipindi hicho hicho, Serikali imefuta asasi za kiraia zaidi ya 100 na haijatoa sababu za msingi za kufanya hivyo.
Mheshimiwa Spika,kana kwamba haitoshi, Serikali sasa imezuia Televisheni ya Umma, inayoendeshwa na kodi ya wananchi TBC1kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mijadala inayofanyika Bungeni.
Mheshimiwa Spika, dalili hizi sio njema kwa ukuaji wa Demokrasia na uhuru wa habari hapa nchini na zinatoa taswira ya utawala wa ki-dikteta kama nilivyoeleza hapo awali.
Mheshimiwa Spika, licha ya  Mpango wa Maendeleo wa Taifa kuonesha kwamba  Serikali itawekeza katika demokrasia; “investing in the electoral process, and expand the freedom of expression, transparency and access to information” ikiamaanisha kuwekeza katika mchakato wa uchaguzi, kupanua uhuru wa kujieleza, uwazi na kupatikana kwa taarifa; lakini Serikali hii ya Dkt. John Pombe Magufuli  imeweka kando Mpango huo na kuanza kutekeleza Mpango mwingine wa siri wa kukandamiza uhuru wa habari. Aidha, Serikali hii ya CCM  imeendelea kuitumia Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cyber Crime Act) ambapo vijana kadhaa wamefunguliwa mashitaka mahakamani kutokana na kutumia  uhuru wao wa kikatiba  wa kujieleza kupitia mitandao ya kijamii. Hii ni mifano michache ambayo inaonesha matendo ya Serikali ya awamu ya tano kukinzana na mpango wake yenyewe wa Maendeleo ya Taifa.
Mheshimiwa Spika, kutokana na Serikali hii ya ‘hapa kazi tu’ kuendeleza kazi ya kuvishughulikia vyombo vya habari wakiwemo waandishi wa habari na kutunga na kuendeleza  sheria ngumu na kandamizi kwa uhuru wa habari; tayari mashirika mbalimbali ya kimataifa yamefanya tafiti na kugundua kwamba kuna ukandamizaji mkubwa wa uhuru wa habari Tanzania. Aidha, jumuiya ya kimataifa kwa nyakati tofauti imeshatoa matamko ya kulaani vitendo hivyo.
Mheshimiwa Spika,Shirika la Kimataifa  linalojishughulisha na masuala ya uhuru wa vyombo vya habari linalojulikana kama ‘Freedom House’ lilitoa matokeo ya utafiti wake Julai, 2015 na kusema kwamba nia na madhumuni ya Serikali ya Tanzania kuanzisha Sheria ya Makosa ya Kimtandao (Cybercrimes Act) na Sheria ya Takwimu (Statistics Act) ilikuwa ni kuvipunguzia wigo vyombo vya habari  wa kufanya kazi kwa uhuru.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa utafiti huo; Freedom House wanasema kwamba uamuzi wa Serikali kuanzisha Sheria hizo, ulitokana na hofu ya Serikali na Chama cha Mapinduzi kushindwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita wa 2015 kutokana na kushindwa kuondoa umasikini kwa wananchi, kuboresha huduma za jamii, kuboresha miundombinu pamoja na  ufisadi uliokithiri. Kwa sababu hiyo, Freedom House; wanaendelea kusema kwamba; ili kujilinda CCM ikishirikiana na Serikali yake; ilikuwa na lengo la kuvinyamazisha vyombo vya habari visije vikaweka hadharani jinsi CCM ilivyoshindwa kuondoa umasikini kwa wananchi; ilivyoshindwa kuboresha huduma za jamii; na madhaifu yake mengine.
Mheshimiwa Spika, pia katika ripoti hiyo, Tanzania imetajwa kuwa  miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ambapo waandishi wa habari wameendelea kuwekewa vikwazo vya kisheria na kisiasa na kushambuliwa kimwili na kutishiwa maisha jambo linaloathiri utendaji wao na hivyo kuminya uhuru wa habari.
Mheshimiwa Spika, mbali ya utafiti huo wa taasisi makini ya kimataifa inayoaminika duniani kuonesha kwamba kuna ukandamizaji wa uhuru wa habari hapa nchini, ni mwaka jana tu, muda mfupi baada ya sheria ya makosa ya kimtandao kuanza kutumika nchini, Umoja wa Ulaya ulilaani kitendo cha kukamatwa kwa maafisa wa Kituo cha Sheria na  Haki za Binadamu nchini na kunyang’anywa vifaa vyao vya kazi kwa kile kilichodaiwa ni kukiuka kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya kimtandao. Ikumbukwe kwamba maafisa hao wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu walikuwa wakikusanya taarifa za waangalizi wa kitaifa kuhusu matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Mheshimiwa Spika, madhila kama hayo yaliwakumba pia vijana wataalamu wa vyama vya Upinzani vinavyounda UKAWA waliokuwa wakifanya kazi ya kujumlisha matokeo ya kura za urais. Hawa walikamatwa na kunyang’anywa vifaa vyao vya kazi zikiwemo simu na kompyuta, na hatimaye kushtakiwa kwa kutumia sheria ya makosa ya kimtandao.
Mheshimiwa Spika, tamko hilo la umoja wa ulaya linalolaani matumizi mabaya ya sheria ya makosa ya kimtandao kukandamiza uhuru wa habari na haki za binadamu limeambatanishwa pamoja na hotuba hii. (tazama kiambatanisho na. 1)
Mheshimiwa Spika, wakati Serikali hii ya CCM inakanyaga demokrasia kwa kuminya uhuru wa habari hapa nchini; serikali hii hii ya CCM iliridhia na kusaini Azimio la Kimataifa la Uwazi katika Uendeshaji wa Serikali (Open Government Partnership -OGP) mnamo mwezi Septemba, 2011. Ili kujiunga na OGP ni lazima nchi wanachama wakubali na misingi ya uhuru na haki zilizoainishwa katika Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu na  mikataba mingine ya Kimataifa kuhusu haki za binadamu na utawala bora na waweke mkakati wa kukuza utamaduni wa uwazi katika uendeshaji wa Serikali.
Mheshimiwa Spika, Azimio la OGP limeridhiwa na kusainiwa na nchi 69; na sehemu ya azimio hilo inasema kama ifuatavyo:
“Together, we declare our commitment to: Increase the availability of information about governmental activities.
Governments collect and hold information on behalf of people, and citizens have a right to seek information about governmental activities. We commit to promoting increased access to information and disclosure about governmental activities at every level of government. We commit to increasing our efforts to systematically collect and publish data on government spending and performance for essential public services and activities. We commit to pro-actively provide high-value information, including raw data, in a timely manner, in formats that the public can easily locate, understand and use, and in formats that facilitate reuse. We commit to providing access to effective remedies when information or the corresponding records are improperly withheld, including through effective oversight of the recourse process. We recognize the importance of open standards to promote civil society access to public data, as well as to facilitate the interoperability of government information systems. We commit to seeking feedback from the public to identify the information of greatest value to them, and pledge to take such feedback into account to the maximum extent possible”.
Mheshimiwa Spika, hilo ndilo azimio ambalo nchi yetu iliridhia na kwa kifupi kabisa lina maanisa kwamba nchi zote zilizoridhia azimio hili zinafungwa na masharti ya azimio hili kuweka mazingira rafiki ya upatikana wa habari hasa kuhusu utendaji wa Serikali kwa uwazi na uhuru wa hali ya juu kabisa. Lakini kinachofanywa na Seriali hii ya CCM ni kinyume kabisa na azimio ililosaini.

3.   UKIUKAJI WA KATIBA YA NCHI KUHUSU MASUALA YA UHURU WA KUPATA HABARI
Mheshimiwa Spika, Ibara ya 18 (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inatamka kwamba:“Kila mtu anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii”
Mheshimiwa Spika, licha ya Katiba ya nchi yetu kutoa haki na uhuru wa kupata habari kwa kila mwananchi, Serikali imeamua kwa makusudi kuvunja katiba ya nchi kwa kuikanyaga haki ya kupata habari.
Mheshimiwa Spika, katika Mkutano wa Pili wa Bunge lako tukufu, Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mhe. Nape Nnauye, alitoa kauli ya Serikali kwamba; Shirika la Habari la Utangazaji (TBC) halitarusha tena matangazo ya  moja kwa moja kuhusu mijadala ya vikao vya Bunge kuwa kisingizio kwamba  gharama za kufanya hivyo ni kubwa. Waziri Nape alianisha kuwa Shirika hilo linatumia zaidi ya shilingi bilioni 4 kwa mwaka kurusha matangazo ya Bunge.
Mheshimiwa Spika, nimesema kwaba Serikali ilitumia kisingizio cha gharama lakini ni wazi kuwa  ina sababu nyingine ya kuzuia vyombo vya habari kurusha mijadala ya bunge moja kwa moja  kwa sababu; baadhi ya vyombo vya habari, likiwemo Shirika la Uhai Production kupitia Televisheni yao ya Azam, vilijitolea kutumia gharama zao kurusha matangazo hayo lakini  wakazuiwa. Aidha, asasi ya Tanzania Media Fund inayoshughulika na kuviwezesha vyombo vya habari na wanahabari ilitoa ahadi yake kuwa ingeweza kugharamia urushwaji wa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge na ilikuwa tayari kulipia gharama za TBC ili wananchi waweze kufuatilia yanayoendelea Bungeni lakini nayo pia ilizuiliwa.
Mheshimiwa Spika, baada ya ahadi hizo za wadau wa habari nchini kabla ya kuanza kwa mkutano huu wa bajeti serikali kupitia Bunge ikaja na sababu nyingine za ziada kuwa haitaruhusu vyombo vya habari kurekodi vikao vya Bunge na hata waandishi wa habari hawataruhusiwa kuchukua taarifa yoyote Bungeni mpaka pale itakapotolewa rasmi kupitia Ofisi ya Bunge.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mikutano ya Bunge ni muhimu kwa ajili ya wananchi kujua na kufuatilia utendaji wa wawakilishi wao ndani ya chombo hiki cha uwakilishi, na kwa kuwa serikali ilisitisha kwa amri TBC kutoendelea kurusha matangazo hayo ni dhahiri serikali ina sababu za ziada kuliko sababu za gharama.
Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa serikali haipo tayari kuona wananchi wakipokea matangazo ya moja kwa moja ya Bunge  na inaelekea kuna sababu ambayo Kambi Rasmi ya Upinzani na wananchi kwa ujumla hawaijui kuhusu suala hili. Aidha ni mkakati wa serikali hii ya awamu ya tano kuvibana vyombo vya habari na kuwanyima wananchi kujua moja kwa moja kinachoendelea ndani ya Bunge.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapenda kuweka msimamo wake rasmi kuwa serikali imevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 18 kama nilivyonukuu katika hotuba hii. Jambo hili ni la kulaaniwa na watu wote wapenda demokrasia ndani na nje ya Bunge hili. 
Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuliomba radhi bunge hili kwa kosa la  kuminya uhuru wa habari  kinyume na Katiba ya Nchi na kuviacha vyombo vya habari hususan vya umma kufanya kazi zao za kuuhabarisha umma  kwa uhuru kwa kuwa vinatumia kodi ya wananchi. Kitendo cha Serikali hii ya awamu ya tano inayojinasibu kwa kauli ya hapa kazi tu, cha kukimbilia kudhibiti vyombo vya habari, kinatoa taswira kwamba Serikali hii inaogopa kivuli chake kabla hata kazi yenywe haijaanza. Na matokeo yake, badala ya ‘hapa kazi tu’ sasa imekuwa ‘hapa hofu tu’ ambapo mawaziri na watendaji wote serikalini sasa wanafanya kazi kwa hofu badala ya weledi na taaluma.

4.   UMOJA WA WASANII NA UKUAJI WA TASNIA YA USANII NCHINI
Mheshimiwa Spia, wahenga wetu hawakukosea kusema kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Ili sekta ya usanii nchini ikuwe na iwe na tija inayokusudiwa ni lazima wasanii waungane ili wawe na sauti moja yenye nguvu kudai haki na maslahi yao.
Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwa sababu ukuaji wa sekta hii unasuasua. Na sababu ya kusuasua huko, ni njama zinazoendeshwa na Serikali hii ya CCM ya kuwagawa wasanii ili wawatumie vizuri kwa maslahi ya kisiasa.
Mheshimiwa Spika, kitendo cha Waziri wa wizara hii na Rais kuwaita wasanii fulanifulani na kufanya nao mazungumzo na kuwabagua wasanii wengine, kunawagawa wasanii, na kunajenga matabaka miongoni mwa wasanii. Kundi la wasanii walioonana na Rais au Waziri wanajiona kuwa ‘superior’ kuliko wengine.
Mheshimiwa Spika, hali kama hiyo haina afya hata kidogo katika ukuaji wa tasnia ya usanii. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatoa rai kwa wasanii kujiunga na vyama  kulingana na aina ya usanii wanaofanya, ili kama kuna jambo ambalo Serikali inataka kuwashirikisha wasanii basi iwaalike wawakilishi wa vyama hivyo kuliko kukutana na msanii mmoja mmoja au baadhi yao.
Mheshimiwa Spika, tunashauri pia kwamba; kuwe na utaratibu wa kisheria kwamba; kabla msanii hajasajiliwa na BASATA kama sheria inavyotaka, basi msanii huyo awe mwanachama hai wa vyama vya wasanii kama vile vyama vya muziki mfano TUMA, CHAMUDATA, Chama cha Taarabu na hata chama cha muziki wa Injili ambavyo vipo ila vinalegalega kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ubinafsi wa wasanii wenyewe; vinginevyo wataendelea kunyonywa na kubaki kulalamika.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatambua umuhimu wa kulinda kazi za sanaa na wasanii wa hapa nyumbani. Kwa sababu hiyo, tunaitaka Serikali kuweka utaratibu wa kisheria utakaowezesha vituo vyote vya redio na televisheni nchini kupiga asilimia 80 ya muziki wa wasanii wa nyumbani ili kulinda sanaa zetu na kukuza soko la bidhaa za wasanii wa ndani. Nchi nyingi duniani zina sheria za kwalinda wasanii wao wa ndani hivyo inabidi nasi kwenda na kasi ya dunia.

5.   TASNIA YA MICHEZO
Mheshimiwa Spika, licha ya ukweli kwamba michezo inajenga afya, lakini michezo ni ajira pia. Kwa sababu hiyo, vijana wetu wanaoshiriki katika michezo wana ndoto pia ya kupata fursa ya  ajira katika tasnia hiyo.


Mheshimiwa Spika, pamoja na uhalisia kwamba Tanzania ina vijana wengi wanaopenda michezo, lakini wanashindwa kufikia ndoto zao za kujikwamua kimaisha kupitia tasnia hiyo kutokana na vyama vya michezo kukosa fedha kwa ajili ya kuwaendeleza wanamichezo wetu. Wakati mwingine chama cha michezo kinakosa fedha ya kuilipia nauli timu yake kwenda kwenye mashindano nje ya nchi badala yake inalazimika kupeleka watu wawili au watatu. Katika hali kama hiyo, ndoto za wanamichezo wetu haziwezi kufikiwa.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni  inaitaka Serikali kuvipa ruzuku vyama vya michezo ili viweze kujiendesha na hivyo kuweza kuwasaidia wanamichezo wa nchi hii kutimiza ndoto zao katika tasnia ya michezo.

Mheshimiwa Spika, michezo ni mojawapo ya vitu ambavyo vinawaunganisha watu kwa haraka zaidi na ni tunu ambayo inajenga ujirani mwema, urafiki, umoja na udugu. Kwa muda mrefu michezo hapa nchini imekuwa ikichuliwa kama suala la burudani na kujifurahisha tu, bila ya kulipa umuhimu unaostahili.

Mheshimiwa Spika, ili kuboresha tasnia  ya michezo nchini , Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe ;
i.                    CCM itakiwe kurejesha serikalini viwanja vyote vya michezo ambavyo ni mali ya wananchi na viweze kuendelezwa kwa ajili ya kukuza sekta hii nchini.
ii.                  Shule zote   za msingi na sekondari pamoja na  vyuo   vitakiwe kuwa na maeneo ya michezo ya nje na ya ndani kabla ya kupatiwa usajili.
iii.                 Kuwe kwa utaratibu wa kisheria ili kusimamia ajira za sekta ya michezo ikiwemo mikataba ya wachezaji, maslahi yao na mafao yao. Lengo ni kuhakikisha kuwa wachezaji wote wanaopata nafasi ya kuchezea ngazi za ligi za kitaifa au kuwakilisha taifa wanapata malipo ya ajira na mafao kama watumishi wengine wa umma.
iv.              Turejeshe mashindano ya mashirika na taasisi za umma na kuyaboresha zaidi ili yawe na mvuto kwa kutoa zawadi nono pamoja na kuvutia wadhamini mbalimbali.
v.                Kila mkoa utakiwe kuchagua shule moja ya msingi na moja ya sekondari ambazo zitaboreshwa na kuwa shule maalumu za michezo. Watoto watakaojiunga na shule hizi maalumu za kitaifa za michezo (national sports academy) watafundishwa elimu ya kawaida sawa na wenzao wa shule zingine ila watatofautiana na wenzao kwa kuwa wao watawekewa mkazo zaidi kwenye michezo mbalimbali.

6.   TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE (TWIGA STARS)
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatambua jitihada zinazofanywa na timu yetu ya Taifa ya wanawake katika kuliletea taifa letu heshima katika tasnia ya michezo. Aidha, tunaipongeza kwa kwa mchezo mzuri kati yake na timu ya taifa ya wanawake ya  Zimbabwe  uliofanyika mwezi Machi, 2016 huko Cameroon.

 
Mheshimiwa Spika,timu hii ina rekodi ya mafanikio makubwa katika mechi za kimataifa. Mwaka 2010 ilifanikiwa kufuzu kuingia fainali ya CAF Women’s Champion na kuibuka mshindi kwa  kufunga timu ya Eritrea mabao 11 kwa 4.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio hayo, timu hii inakabiliwa na changamoto nyingi jambo linaloifanya ishindwe kuendelea kung’ara katika mechi za kimataifa. Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya michezo, ukosefu wa wadhamini, upungufu wa viwanja vya michezo na kukosa motisha kwa wachezaji. Changamoto nyingine ni ukosefu wa hamasa kwa viongozi na wananchi kwa jumla katika kuifahamu na kuisaidia timu hii.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuhakikisha kuwa timu hii inatafutiwa wadhamini lakini pia Serikali itoe hamasa kwa viongozi na  wananchi  kujitokeza zaidi kuwekeza kwenye vipaji vya wanawake ili kuhamasisha wanawake wengi zaidi kujiunga na timu hii. Ni matumaini  ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwamba Waheshimiwa wabunge wanawake watakuwa mstari wa mbele katika kutoa hamasa ili kuipa nguvu timu ya taifa ya Wanawake.

7.   UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, WASANII NA MICHEZO KWA MWAKA WA FEDHA 2015/16
Mheshimiwa Spika,kwa mujibu wa randama ya Wizara hii, fedha za maendeleo zilizoidhinishwa na bunge kwa ajili ya wizara hii kwa mwaka wa fedha 2015/16 ni shilingi bilioni 3.Lakini mpaka kufikia Februari, 2016, hakuna fedha yoyote iliyokuwa imetolewa na hazina kwa ajili ya maendeleo. Hata hivyo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haina hakika kama fedha hiyo itakuwa imetolewa hadi kufikia muda huu.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa maelezo ni kwa nini inachelewesha kupeleka fedha za maendeleo kiasi hiki? Hivi kweli hata kama Serikali itatoa hizo bilioni 3 katika robo ya mwisho wa mzunguko wa bajeti, itafanya shughuli gani?

Mheshimiwa Spika, licha ya Serikali kushindwa kutekeleza bajeti ya maendeleo iliyodhinishwa na bunge kabisa kwa mwaka wa fedha 2015/16; inashangaza kwamba bajeti ya maendeleo inayoombwa kwa wizara hii kwa mwaka 2016/17 imepunguzwa kwa shilingi bilioni moja. Safari hii Wizara hii imetengewa shilingi bilioni 2 tu kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, kitendo cha kupunguza bajeti ya maendeleo kunadhihirisha kwamba sasa Serikali imedhamiria kwelikweli kuminya uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini. Hii ni kwa sababu vyombo vya habari vya Umma ikiwemo TBC vinaendeshwa kwa fedha za maendeleo.  Hivyo, ikiwa fedha za maendeleo hakuna, tusitegemee ufanisi katika vyombo hivyo.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilitegemea kwamba Serikali ingeongeza fedha za maendeleo katika wizara hii  ili  TBC iweze kurusha moja kwa moja mijadala ya Bunge, kwa kuwa awali Serikali ilisema imeamua kusitisha urushaji wa matangazo hayo kutokana na ukosefu wa fedha. Sasa fursa imetokea ya kuongeza fedha katika bajeti ili matangazo hayo yarushwe lakini kinyume chake Serikali imepunguza bajeti ya maendeleo ya wizara hii.

8.    HITIMISHO
Mheshimiwa Spika, hoja kubwa katika hotuba hii ni madai ya haki ya uhuru wa habari ambao Serikali hii ya awamu ya tano imewapoka wananchi kinyume na Katiba ya nchi. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapenda kuifahamisha Serikali hii ya CCM kwamba; kitendo inachokifanya cha kupoka haki ya kikatiba ya uhuru wa kupata habari ni cha hatari sana kwa mustakabali wa amani ya nchi yetu.
Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwa sababu wananchi wana hasira kubwa kutoka na hali ya maisha kuwa ngumu zaidi hasa baada ya Serikali hii ya awamu ya tano kushika madaraka. Hasira hizi za wananchi angalau zilikuwa zinapunguzwa wakati wanapofuatilia katika televisheni jinsi wawakilishi wao (wabunge) wanavyowasemea kuhusu matatizo yanayowakabili. Sasa hawana fursa tena ya kuona chochote kinachoendelea bungeni.
Mheshimiwa Spika, wakati Serikali inazuia televisheni ya umma isirushe matangazo ya moja kwa moja ya mijadala bungeni; Serikali inatumia chombo hichohicho kufanya propaganda ya kumjenga Rais Magufuli kisiasa aonekane kama mtu mwema anayejali watu wakati ukweli ni kwamba ukandamizaji huu demokrasia wa kuminya uhuru wa habari unafanywa na yeye mwenyewe kupitia waziri wake Nape.
Mheshimiwa Spika, kitendo cha kuwazuia wananchi wasione kinachoendelea bungeni wakati hali zao zinazidi kuwa ngumu kutokana na ukosefu wa huduma mbalimbali za jamii; kinaweza kuwapandisha wananchi hasira zaidi na hivyo kuchukua hatua ya kufanya ‘mass action’ kupinga ukandamizaji huu wa haki ya uhuru wa habari unaofanywa na Serikali hii yenye dalili zote za udikteta.
Mheshimiwa Spika, ili kuzuia hayo yote yasitokee, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kuiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuviagiza vituo vyote vya television vyenye leseni ya TCRA kuingiza kwenye ving’amuzi vyao Chaneli ya Bunge na kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge kwa wananchi bure.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba kuwasilisha.

Joseph Osmund Mbilinyi (Mb)
WAZIRI KIVULI NA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI
YA UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA
HABARI, UTAMADUNI, WASANII NA MICHEZO
13 Mei, 2016
KIAMBATANISHO NA. 1: TAMKO LA UMOJA WA ULAYA KUHUSU UKANDAMIZAJI WA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA

EUROPEAN UNION
JOINT LOCAL STATEMENT ON HUMAN RIGHTS INFRINGEMENTS

         Monday, 09 November 2015

The European Union Head of Delegation, the Heads of Mission of Belgium, Denmark, Finland, France, Germany, Ireland, Italy, the Netherlands, Spain, Sweden, the United Kingdom and the Heads of Mission of Canada, Norway, Switzerland and the United States of America; issue the following statement in the United Republic of Tanzania:
The Heads of Mission of the European Union Delegation, Belgium, Denmark, Finland, France, Germany, Ireland, Italy, the Netherlands, Spain, Sweden, the United Kingdom and the Heads of Mission of Canada, Norway, Switzerland and the United States of America recall that the Government of the United Republic of Tanzania had committed to applying the Cyber Crimes Act of 2015 in a manner that respects fundamental freedoms and to addressing a potentially negative interpretation of the law. However, the first cases of application raise concern in view of their potential infringement of fundamental freedoms.
The Heads of Mission are concerned about the recent arrest of members of staff of the Legal and Human Rights Centre and confiscation of key technical outfits, reportedly motivated by Section 16 of the Cyber Crimes Act. The events took place while the organization was compiling observations made by national election observers around the country, a task for which the Legal and Human Rights Centre has been accredited by the National Electoral Commission. The Heads of Mission recall that the Legal and Human Rights Centre is a member of the Tanzania Coalition of Human Rights Defenders.
As spelt out in the African Charter on Democracy, Elections and Governance, the Heads of Mission are “convinced of the need to enhance the election observation missions in the role they play, particularly as they are an important contributory factor to ensuring the regularity, transparency and credibility of elections”.
Heads of Mission call on the Government of Tanzania to assure that the implementation of the Cyber Crime Act does not lead to infringement of universal human rights and fundamental freedoms, particularly the freedoms of expression and association and the right to participate in genuine elections and that it respects principles of good governance and the role of election observers and civil society organizations in the democratic processes.
For more information, please contact: 
Ms. Luana REALE, Head of Political, Press and Information Section- Delegation of the European Union to Tanzania   Direct Line: +255 22 2164503  Email: Luana.REALE@eeas.europa.eu
Website: http://eeas.europa.eu/delegations/tanzania/index_en.htm
 Facebook: https://www.facebook.com/EuropeanUnionTanzania Twitter: https://twitter.com/EUinTZ[1] Egorov G.  et.al. (2009) Media Freedoms in Dictatorships, Harvad University.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...