Friday, June 3, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI NCHINI PAPOA NEW GUINEA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wazee na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea Baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific  uliojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa uliomalizika Jana.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya Picha yenye Nembo inayotumika Nchini Papua New Guinea kutoka kwa Wazee na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea baada ya kuzungumza nao katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea alipokamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific  uliojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa uliomalizika Jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea baada ya kuzungumza nao katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea alipokamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific  uliojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa uliomalizika Jana. (Picha na OMR)

CHEKI VIPODOZI VILIVYOMKATAA DIAMOND NA KUMTOA MABAKA USONI

 Na Humphrey Shao, Dar es Salaam

siku chache mara baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nayefanya vizuri katika soko la kimataifa , Diamond Platinumz  kujitokeza hadaharani akizungumza na waandishi wa habari watu wahoji juu ya matumzi yake ya vipodozi zilivyomfanya awe na mabakmabaka usoni.

Diamond ambaye ananekana pichani akiwa akiwa kama na madoadoa doa u rangi mbii tofauti zinazoonekana katika paji la uso wake kutokana  na matumizi ya vipodozi ambayo yanonesha kutozaa matunda katika sura ya mwanamuziki huyo.

waandishi kadhaa katika mkutano huo walipata kujiuliza juu mwanamuziki huyo kuanza kujiaribu na vipodozi vyenye kemikali ambavyo vimeweza kutoa rangi yake ya asili na kuamuacha na mabaka usoni

ACT YAWAOMBA UKAWA KUFANYA MIKUTANO YA PAMOJA NCHI NZIMA


CHAMA CHA ACT WAZALENDO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Awali ya yote, tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana kwa kuitikia wito wa kuja kutusikiliza. Karibuni sana!
Ndugu Waandishi wa Habari
Leo tumewaiteni ili kuwaeleza msimamo wa Chama chetu cha ACT Wazalendo juu ya uamuzi uliofanywa na Kamati ya Bunge ya Maadili na Madaraka ya Bunge kuwasimamisha wabunge saba wa upinzani akiwemo Mbunge wa ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe.
Ikumbukwe kuwa uamuzi huu wa Kamati ya Maadili ambayo sehemu kubwa ya wajumbe wake ni wabunge wa Chama cha Mapinduzi(CCM) unafuatia msimamo wa wabunge wa upinzani wakiongozwa na Mbunge wa Chama chetu kupigania maslahi ya wananchi kupata habari za bunge.
ACT tunaamini  Wabunge hawa wametolewa kafara kwa kupinga vikali uamuzi wa Serikali kuzuia matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja.
Ndugu waandishi wa Habari

Chama chetu kimeandaa mapokezi haya yaliyopewa jina maalum la “Opereshen” Linda Demokrasia, lengo likiwa ni kuwapa nafasi mashujaa  hawa waliofukuzwa bungeni kwa ajili ya kusimamia maslahi ya umma, kuelezea  kilichotokea na kinachoendelea bungeni ambacho watawala hawataki kijulikane.
Pia katika mkutano wa hadhara Kiongozi wa Chama ndugu  Zitto Kabwe atafafanua kwa kina muktadha wa siasa za sasa na hatari ya kuua vita dhidi ya ufisadi kutokana na namna demokrasia inavyofifishwa  
Ndugu waandishi wa Habari
Kwa kutambua umuhimu wa utetezi wa maslahi ya wananchi na kuisimamia serikali kupitia Bunge Chama chetu baada ya mkutano wa Dar esSalaam utakaofanyika Jumapili ya Juni 5 mwaka huu katika viwanja vya Mbagala Zakiem, pia Chama kitafanya mikutano mingine mikubwa ya hadhara katika mikoa ya  Mwanza ( 11 Juni, 2016), Kigoma (12 Juni, 2016), Mbeya (18 Juni, 2016) na Morogoro (19 Juni, 2016).
Chama chetu kimeviandikia barua vyama vya CUF, CHADEMA na NCCR-Mageuzi kuviomba kushiriki kwenye  mapokezi hayo.Tunasubiri majibu ya vyama tulivyowaalika kwa kuwaandikia barua kwa kuwa mpaka sasa hawajatujibu rasmi kama watashiriki ama la zaidi ya kutufahamisha kuwa wamepokea barua zetu

Ndugu Waandishi wa Habari
Sisi ACT-Wazalendo,tunaamini “Operesheni Linda Demokrasia” ni muhimu ikapiganwa na vyama vyote pasipo kujali itakadi ya vyama kwa kuwa  hoja hiyo ya kutaka Bunge lioneshwe moja kwa moja ilipoibuliwa  na Mbunge Ndugu  Zitto Kabwe  kuhoji hatua ya serikali kubana uwazi Bungeni,wabunge wote wa upinzani walisimama na kuiunga mkono hoja na kuitetea
Ndugu Waandishi wa Habari
Tunawashukuru tena kwa kuitikia kwenu wito wa kufika na tunawatakia majukumu mema ya ujenzi wa Taifa.
Ahsanteni sana!
Ndugu Ado Shaibu Ado
Katibu, Itikadi Uenezi na Mawasiliano ya Umma,
ACT Wazalendo
Waandishi wakifatilia kwa makini

SHIRIKISHO LA MUZIKI LATOA TAHADHARI KWA WASANII

 Rais wa Shirikisho la Muziki nchini , Addo November, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mipango ya shirikisho hilo katika kupambana na uaramia wa kazi za Sanaa, pembeni yake ni Katibu wa shirikisha hilo ,John Kitime na Mjumbe Dani MsimamoNa Humphrey Shao, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la muziki nchini limewaonya wanamuziki ambao wamejiingiza katika mikataba na vyombo vya habari kupiga nyimbo zao pasipo kufata sheria ya haki miliki watakuwa wamejinyima haki yao wenyewe.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo , Katibu mkuu wa shirikisho hilo, John Kitime amesema kuwa kutokana na sheria ya haki miliki na haki shiriki kutaka kuanza kufanya kazi vupo vyombo vya habari ambavyo vimeanza kuunda makundi ya wanamuziki ambao wapo chini yao jambo amablo sio dawa ya kukwepa sheria hii.
“hili jambo sio geni hata nchi za jirani ilipoanza watu walijaribu kufanya hivyo lakini kutokana na uelewa wa wasanii alikuwez kufanikiwa hivyo mpaka leo kila mtu anapata mafao yake hata kama atakuwa mzee ilimradi tu ule mziki wake ukiwa unaishi”alisema Kitime.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho hilo ,Addo November , alitoa wito kwa wasanii kujiungakatika vyama vayao amabavyo vinaweza kuwaunganisha katika shirikisho ambalo linaweza kuwa na sauti moja kwa maslahi ya wasanii. Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wasanii ,Juma Ubao, akizungumza na waandishi
 Waaandishi wakifatilia kwa makini mkutano huo
 Waaandishi wakifatilia kwa makini mkutano huo
 Wajumbe wa shirikisho hilo
Katibu wa Shirikisho la Muziki nchini, John Kitime akizunguza na waandishi wa Habari

Thursday, June 2, 2016

PEMBA Let your mind drift to the most beautiful Island in East AfricaDar es Salaam, Tanzania, June 2, 2016- On the Swahili coast of the Zanzibar Archipelago in East Africa, lies semi-autonomous Pemba Island. As one of the world’s leading Clove producer in only 988 square kilometers, the Island is divided into two regions of Chake-Chake and Mkoani. It is found on the North of its twin Island Unguja.

Most of Pemba’s inhabitants are Swahili speakers who descended from Persian Gulf and came for business in the East African coast around 10thC and later conquered by the Arab traders and Sultans.

Pemba and Unguja has formed the Paradise Islands of Zanzibar, which later came to join Tanganyika in 1964 to form Tanzania. Now Zanzibar is one of the most important destination in Tanzania’s Tourism, with the growth of over 9.6% annually.

Pemba, also popularly known as the ‘Green Island’ or ‘Al Jazeera Al Khadra’, is a beautiful tourist destination with numerous tourists attractions such as unspoiled diving areas with very rich marine life, famous spiritual mystics and physical healers. It is also home to amazing white sandy beaches and tourism sites such as Jozan Forest reserve, the Ancient forest which is the home of flying fox.

You can visit Chake Chake Museum and enjoy snorkeling around Misali Island with amazing colorful fishes. Experience the popular bullfight which was introduced by the Portuguese and the beautiful archeological sites such as Ras Mkumbuu and the 10th Century Mosque, one of the oldest Muslim Settlements in Africa.


Apart from cloves, the Pemba dwellers also use the fertile place for small scale agriculture to grow rice, coconuts, banana, cassava and red beans.

HABARI KATIKA PICHA ZA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, PROF. JUMANNE MAGHEMBE NA MBOBEZI WA PICHA BW. ROBERT ROSS1.    Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akikabidhiwa kitabu cha picha za wanyamapori  waliopo katika Pori la Akiba la Selous na Mtaalamu wa picha wa  Kimataifa, Bw. Robert Ross wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Mpingo House jijini  Dar es Salaam. Kitabu hicho cha picha za wanyamapori waliopo  katika pori la Akiba la Selous kinatarajiwa kuzinduliwa leo na Mhe. Waziri ambaye atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu , Injinia Angelina Madete, katika Hoteli ya Slip way. Kitabu hicho kinatarajiwa kutumika  kama nyenzo muhimu katika kutangaza Utalii wa Tanzania katika Nyanja za Kimataifa.1.    Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akikabidhiwa kitabu cha picha za wanyamapori  waliopo katika Pori la Akiba la Selous na Mtaalamu wa picha wa  Kimataifa, Bw. Robert Ross wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Mpingo House jijini  Dar es Salaam. Kitabu hicho cha picha za wanyamapori waliopo  katika pori la Akiba la Selous kinatarajiwa kuzinduliwa leo na Mhe. Waziri ambaye atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu , Injinia Angelina Madete, katika Hoteli ya Slip way. Kitabu hicho kinatarajiwa kutumika  kama nyenzo muhimu katika kutangaza Utalii wa Tanzania katika Nyanja za Kimataifa.1.    Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akiangalia baadhi ya picha katika  kitabu cha picha za wanyamapori  waliopo katika Pori la Akiba la Selous na mara baada ya kukabidhiwa kitabu hicho na  Mtaalamu Kimataifa, Bw. Robert Ross (kushoto)  wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Mpingo House jijini  Dar es Salaam. Kitabu hicho cha picha za wanyamapori waliopo  katika pori la Akiba la Selous kinatarajiwa kuzinduliwa leo jioni katika Hoteli ambapo Kitabu hicho kitakuwa ni nyenzo muhimu katika kutangaza Utalii wa Tanzania  katika Nyanja za Kimataifa.1.    Huu ni mwonekano wa nje wa  kitabu cha Picha  zilizochukuliwa katika Pori la Akiba Selous na Mtaalamu wa picha wa  Kimataifa, Bw. Robert Ross, Kitabu hicho kinatarajiwa kuzinduliwa leo na Waziri, Prof. Maghembe ambaye atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Injinia Angelina Madete  katika hoteli ya Slipway.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...