Friday, June 10, 2016

POLISI KANDA MAALUM YAKAMATA WATUHUMIWA 700 KWA WIKI

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Siro akionyesha bahadhi ya Silaha za kienyeji zilizokamatwa
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Siro akionyesha mkasi wa kukatia makufuli ya majumbani
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Siro akionyesha Nondo za kuvunjia

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Siro akionyesha Gongo iliyowekwa katika chupa za Valuer
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Siro akionyesha Shehena ya Bange iliyokamatwa

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Siro akionyesha mitambo ya kutengenezea Gongo

NIDA KUBAINI WAFANYAKAZI HEWA KWA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Rose Mdami
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),wameanza mpango wa kutoa namba ya utambulisho kwa kila mtanzania ili kuweza kujua idadi ya watanzania wanaoishi nchini Mfumo ambao pia utaweza kuwatambua wafanyakazi hewa bila shida.
Mpango huo utaenda sambasamba na utoaji wa vitambulisho vipya ambavyo vitakuwa na saini ya mtoaji na mpokeaji .
Akizungumza Dar es Salaam, jana Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Rose Mdami alisema, vitambulisho hivyo vitasaidia kuleta usalama katika nchi.
Amesema ifikapo Desemba 31 mwaka huu, kila mtanzania anatakiwa awe amepata namba ya utambulisho huku mchakato wa kuandaa vitambulisho vipya ukiendelea.
Rose alisema wapo baadhi ya watanzania ambao walipata vitambuli hapo awali lakini vitambulisho hivyo vitaendelea kutumika kama kawaida kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.
Pia amesema  tayari wameazima mashine 5000 kutoka NEC ambazo zitawapa taarifa mbalimbali na zilizo makini kwa ajili ya utoaji wa vitambulisho hivyo.
Rose amesema kwa siku wana mpango wa kuandikisha wananchi 20,000 ambapo kuna jumla ya watanzania milioni 22.
Hata hivyo alisema mpango huu wa utoaji wa namba ya utambulisho kwa kila mtanzania utasaidia hata kugundua wafanyakazi hewa waliopo .
Alisema mpango huo haraka unaanza agosti mwaka huu sehemu za kazi hivyo kila mfanyakazi anatakiwa apate namba hiyo ya kumjulisha kuwa yeye ni mfanyakazi wa sehemu hiyo alipo.
Hivyo watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika vituo vyao kwa ajili ya kuchukua namba za utambulisho kwa ajili ya faida yao na nchi kwa ujumla.
 waandishi wakisikilza
 Alpha Male benchi akizungumza na waandishi
 Mkurugenzi tehema mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mohamed Khamisi 
 WAPIGA PICHA VYOMBO MBALIMBALI

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...