Sunday, June 19, 2016

Ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari Prof Elisante Ole Grabriel katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, kijiji cha Mtama  (hawapo pichani) wakati wa ziara yake katika Halmashauri Mkoa wa Lindi na Mtwara kuangalia usikivu wa vituo vya Redio na Televisheni vya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel( wa pili kulia) akizungumza na wawakilishi Kutoka Star Times wakati wa ziara yake katika Halmashauri Mkoa wa Lindi na Mtwara kuangalia usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kulia ni Mkurugenzi wa Shirika  hilo Dkt Ayoub Riyoba.
 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja wawakilishi kutoka kampuni ya Star Times na wanakijijji wa kijiji cha Mtama wakati wa ziara yake katika Halmashauri Mkoa wa Lindi na Mtwara kuangalia usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashuri ya Lindi Bw. Matei Makwinya.

PICHA NA WHUSM

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI ATEMBELEA KITUO CHA UHAMIAJI CHA HOROHORO AKAGUA MPAKA WA KENYA NA TANZANIA

 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto), akisalimiana na maofisa  wa vyombo vya ulinzi na usalama, mara baada ya kuwasili katika kituo cha Uhamiaji Horohoro, wilayani Mkinga mpakani mwa Kenya na Tanzania, barabara kuu ya Mombasa-Tanga. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

 Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akiweka saini katika kitabu cha wageni, mara baada ya kuwasili katika kituo cha Uhamiaji Horohoro, wilayani Mkinga mpakani mwa Kenya na Tanzania, barabara kuu ya Mombasa-Tanga. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti  njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

 CAP PIX 3
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Horohoro, DCI Deogratius  Magoma, akimuelekeza jambo Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira mara baada ya ukaguzi wa ofisi za jengo la kituo hicho zinazotumika katika utoaji huduma za uingiaji na utokaji wa raia wa kigeni na raia wa Tanzania wanaopitia mpaka wa horohoro , wilayani Mkinga, jijini Tanga. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

 Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, DCI Andrew Kalengo, akimuelekeza jambo  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, mara baada ya kutembelea daraja la Mwakijembe, linalotumiwa na wakazi wa nchi za Tanzania na Kenya. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (aliyevaa kiraia),  akifafanua jambo kwa viongozi wa Idara ya Uhamiaji Wilayani Nkinga,  mara baada ya kutembelea jiwe linaloonyesha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kijiji cha Jasini kilichopo Kaunti ya Kwale. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua  na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

OLE MEDEYE NA BOMANI WAWA VIONGOZI UDP

 Joh Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mamose Cheyo akimpongeza Kaimu Katibu mkuu wa  Chama  hicho Dk Goodluck Olemedeye
  Mwenyekiti wa Chama cha UDP  John Mamose Cheyo
 Andrew Bomani akitafakari

 Andrew Bomani akizungumza na waandishi wa habari
Kaimu Katibu mkuu wa UDP ,dK Goodluck Olemedeye akizungumza na waandishi w ahabari mara baada ya uteuzi huo

MAGHEMBE AFUNGA MAFUZO YA MAOFISA WA NGAZI ZA JUU WA TANAPA MKOANI KATAVI

 Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo ya kijeshi kwa viongozi wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),mafunzo yaliyofanyika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili mfumo wa utendaji kazi wa shirika hilo kutoka mfumo wa kiraia kuwa Jeshi Usu.

 Maofisa wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakila kiapo cha utii wakati wa kuhitimu mafunzo ya kijeshi kwa viongozi hao ikiwa ni sehemu ya kubadili mfumo wa utendaji kazi wa TANAPA kutoka wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu,mafunzo kwa viongozi hao yamefanyika katika kambi ya Mlele iliyopo mkoani Katavi.

 Mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) akionesha umahiri katika kulenga shabaha kwa kutumia Bunduki wakati wa kuhitimu mafunzo ya kijeshi kwa viongozi hao ikiwa ni sehemu ya kubadili mfumo wa utendaji kazi wa TANAPA kutoka wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu,mafunzo kwa viongozi hao yamefanyika katika kambi ya Mlele iliyopo mkoani Katavi.


 Mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) akionesha umahiri katika kulenga shabaha kwa kutumia Bunduki wakati wa kuhitimu mafunzo ya kijeshi kwa viongozi hao ikiwa ni sehemu ya kubadili mfumo wa utendaji kazi wa TANAPA kutoka wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu,mafunzo kwa viongozi hao yamefanyika katika kambi ya Mlele iliyopo mkoani Katavi.

 Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akitunuku cheti kwa Mhifadhi ,Erastus Rufungulo wakati wa kufunga mafunzo ya kijeshi kwa maofisa wa shirika hilo.ikiwa ni sehemu ya kubadili mfumo wa utendaji kazi wa TANAPA kutoka wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu,mafunzo kwa viongozi hao yamefanyika katika kambi ya Mlele iliyopo mkoani Katavi.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akitunuku cheti kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) wakati wa kufunga mafunzo ya kijeshi kwa maofisa wa shirika hilo.ikiwa ni sehemu ya kubadili mfumo wa utendaji kazi wa TANAPA kutoka wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu,mafunzo kwa viongozi hao yamefanyika katika kambi ya Mlele iliyopo mkoani Katavi.

MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAANDAA FUTARI KWA WAFANYAZI WAKE, DAR

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (kushoto) akiongozana na mgeni Ramsi Kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA, Sheikh Ali Hamis, wakati alipofika kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam jana Juni 17, 2016 kwa ajili ya kumwakilisha Mufti  Mkuu wa Tanzania katika Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mfuko huo. Picha na Mafoto Blog
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (katikati) mgeni Ramsi Kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA, Sheikh Ali Hamis, wakiwaongoza wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, kuchukua Futari wakati wa hafla Futari iliyoandaliwa na Mfuko huo katika Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam jana Juni 17, 2016.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akizungumza na wafanyakazi wa mfuko wake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na mfuko huo  kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam, jana Juni 18, 2016. Kushoto ni mgeni rasmi, Sheikh Ali Hamis. 
 Mgeni rasmi Sheikh Ali Hamis, akizungumza na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF,(hawapo pichani)  wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na mfuko huo  kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam, jana Juni 17, 2016. Katikati ni Mkurugenzi mkuu wa Mfuko huo, William Erio.
*********************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
JAMII imetakiwa kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwani mfuko huo ni faraja kwa Watanzania na unaofanya mambo makubwa kwa lengo la kuwasaidia wananchi.
Wito huo umetolewa na mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Ali Hamis wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na uongozi wa mfuko huo kwa wafanyakazi wake.
Alisema kuna faida kubwa kwa wananchi kujiunga na mfuko huo kwani watafaidika na mafao mbalimbali yanayotolewa na PPF.
Aidha Sheikh Hamis alisema kuwa ipo haja kwa watendaji wa mfuko huo kuendelea kuwaelimisha wananchi ili waendelee kujiunga na PPF.
Alifurahishwa na namna uongozi wa mfuko huo ulivyoandaa hafla ya futari hiyo maalum kwa kuwafuturisha wafanyakazi wake na kwamba hilo ni jambo jema kwani wafanyakazi wanafahamiana na kubadilishana mawazo.
Sheikh Hamis aliitaka jamii kuwaenzi waasisi wa taifa hili kwa kuendelea kudumisha Amani na umoja kwani wamefanya jambo jema la kuwafanya wananchi wote kuwa kitu kimoja bila kujali dini wala kabila.
Kwa mujibu wa Sheikh Hamis,  PPF ni aina ya mfuko unaowawezesha wananchi kujikomboa.
Hivyo ameuomba uongozi wa mfuko huo uendelee na jitihada za kuwafikia wananchi kwenye maeneo mbalimbali hapa nchi na hasa maeneo ya vijijini.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa PPF, William Erio aliwashukuru wafanyakazi kwa kushiriki futari hiyo,ambayo imekuwa ikiandaliwa kika mwaka na kuwashirikisha wafanyakazi wake wote.
Naye mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi TUICO aliushukuru uongozi wa mfuko huo kwa kuwaandalia futari hiyo.

Futari hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi wa PPF kutoka makao makuu, kanda za Ilala, Temeke na Kinondoni.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi katika hafla hiyo, Sheikh, Ali Hamis, wakati wa hafla hiyo. 
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi katika hafla hiyo, Sheikh, Ali Hamis, wakati wa hafla hiyo. 
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, Tawi la Tuico, akiwashukuru wafanyakazi wa mfuko huo kwa kushiriki kikamilifu katika hafla hiyo.
 Sheikh Mohamed Ali, kutoka Baraza Kuu la Waislam Tanzania BAKWATA, akiomba dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...