Skip to main content

Posts

Showing posts from July 24, 2016

NGOs ITAKAZOGAWIA MASHOGA KY JELLY KUFUTIWA USAJILI

MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali (NGOs) ambayo yatabainika kuwa yanaendelea na miradi ya kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja nchini yatafutiwa usajili wake.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (Pichani) aliandika hivyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa ‘facebook’ na kusisitiza kuwa serikali italisimamia kikamilifu suala hilo. “Sijapiga marufuku  matumizi ya vilainishi. Ukweli, Nimepiga marufuku mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kununua na kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi na wanaume wenzao. Sababu nimeshazieleza,” aliandika. Aliongeza “Na nafurahi kuwajulisha kuwa tayari baadhi ya Mashirika hayo yameanza kutekeleza agizo hili kwa kuanza kuondoa vilainishi kwenye miradi yao. Nayapongeza sana. Niendelee kuyataka mashirika mengine kutii agizo hili ambalo tutalisimamia kikamilifu. “Serikali haitasita kuchukua hatua ikiwemo kuyafutia usajili mashirika yanayoendelea na miradi ya kusambaza …

KILA MWAKA NCHINI WAGONJWA WAPYA WA SARATANI 45,000 HUGUNDULIKA.

Na Mwandishi wetu,Addis Ababa

Ugonjwa wa saratani nchini Tanzania  ni chanzo cha magonjwa na vifo,hivyo inakadiriwa Takribani wagonjwa wapya wa saratani 45,000 hugundulika kila mwaka.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika Mkutano wa 10 wa kupambana na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume barani Afrika unaofanyika nchini hapa.

Waziri Ummy (Pichani) amesema kati ya wagonjwa hao asilimia 38  ni wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake, asilimia 14  saratani ya ngozi, asilimia 10  saratani ya matiti na saratani ya tezi ni asilimia 4

Hatahivyo,takribani watu 35,000 hufariki kila mwaka kutokana na magonjwa ya Saratani.

Licha ya changamoto mbalimbali zinazokwamisha jitihada za kukabiliana na magonjwa hayo ikiwemo  uhaba wa Miundombinu ya kutolea huduma za afya, vifaa tiba, Uhaba wa Watumishi wa Afya, rasilimali fedha na gharama kubwa za dawa za matibabu ya saratani,Waziri Ummy amesema Serikali ya …

NECTA RICHARD: NATAKA KUWA MHANDISI NISAIDIE NCHI YANGU

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam WASICHANA wengi nchini wamekuwa wakiyaona masomo ya sayansi kuwa ni magumu na mzigo mkubwa kwao hali inayotoa nafasi kwa wavulana kuchangamkia masomo hayo ambayo yanatajwa kuwa na fursa nyingi za kiuchumi. Tumesikia matamko mbalimbali ya viongozi wa ngazi za juu wa serikali wakiwahimiza wasichana kuachana na mtizamo huo hasi kwa kuanza kuyapenda na kujifunza masomo ya sayansi ili nao waje kuwa wataalamu wa fani tofauti tofauti hapo baadae. Necta Richard ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Jangwani ni miongoni mwa wasichana walioamua kuitikia wito huo wa kusoma masomo ya sayansi. Anasema amejipanga kuhakikisha kuwa anafikia ndoto yake ya kuwa Injinia mkubwa wa baadae nchini pindi Mungu atakapomuwezesha kuhitimu masomo yake. MTANZANIA lilipata fursa ya kuzungumza na Necta punde baada ya kumaliza kuwasilisha hotuba mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa maadhimisho ya Siku…

VILAINISHI VILIVYOKAMATWA SHINYANGA VYAJA NA MAPYA

Wizara imepokea taarifa kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Shinyanga imevamia ofisi za shirika la Jhpiego mkoani humo na kukamata baadhi ya watumishi wake kwa madai ya shirika hilo kugawa mafuta maalumu yanayodhaniwa kutumiwa kuhamasisha ngono za jinsia moja. Baada ya taarifa hiyo wizara inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
Si kweli kwamba shirika la Jhpiego limekuwa likihamasisha ngono baina ya wapenzi wa jinsia moja. Shirika hilo kupitia mradi wa “Sauti” linasaidia serikali katika jitihada za kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa makundi yaliyopo kwenye hatari kubwa ya maambukizi.  Moja ya makundi yanayolengwa ni wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao. Shirika limekua likitoa elimu ya mabadiliko ya tabia kwa wanaume hao huku likiwapatia mafuta hayo kama sehemu ya kuwasaidia kupunguza hatari ya maambukizi. Mafuta hayo yaliingizwa nchini kwa kufuata taratibu za kisheria kwa ufadhili wa Mfuko Maalumu wa Rais wa Marekani wa kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI (…

MUHIMBILI YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI BORA 53 CHETI, FEDHA

Na Mwandishi Maalumu, Dar es Salaam HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imefanya hafla fupi ya kuwakabidhi cheti wafanyakazi bora 53 waliochaguliwa kati ya 3200. Akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Profesa Lawrence Museru alisema wafanyakazi hao walifanya vyema mwaka 2015/16. Mbali ya cheti hicho wafanyakazi hao pia wamepewa fedha kiasi cha Sh. 500,000 kama motisho ili wazidi kufanya kazi kwa bidii kuongeza mafanikio ya hospitali hiyo katika kuhudumia wagonjwa.
Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Profesa Lawrence Museru akimkabidhi cheti chake Daktari wa Kitengo cha Wagonjwa wa Nje, Upendo Jeremia
Furaha isiyo kifani, goti mpaka chini.
Hongera sana mama
Mmefanya kazi nzuri mno

  Washiriki wakifuatilia jambo kwa makini

DEREVA WA UDA AJALI YA TRENI AELEZA ILIVYOKUWA

Na Mwandishi Maalumu, Dar es Salaam DEREVA wa basi la UDA lenye namba za usajili T. 696 CVB ambalo liligonga treni juzi na kusababisha kifo cha mtu mmoja papo hapo na majeruhi zaidi ya 20, Majuto Hamis (PICHANI) amefunguka na kuzungumzia tukio hilo. Akizungumza na matukionamaisha katika wodi 2B iliyoko kwenye jengo jipya la Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) ambako amelazwa kwa ajili ya kupata matibabu, alisema ilikuwa ajali mbaya mno. “Sikutegemea…ilikuwa ni usiku wa saa tatu nilikuwa nimepakia abiria wangu wapatao 40 tulikuwa tunatoka Kariakoo kunaelekea Mbagala lakini safari yetu iliishia pale eneo la Kamata na sasa nipo MOI nikiwa nimevunjika miguu yangu yote miwili. “Jambo ambalo nakumbuka, katika eneo lile, hakuna kielelezo chochote kinachomtaarifu dereva kuwa mbele yake kuna reli inakatisha kwenye barabara hivyo aendeshe kwa uangalifu. “Sasa mchana huwa ni rahisi kujua kama kuna treni inakatisha maana kunakuwa na nuru tofauti na usiku kwani huwa kuna giza,” alisema…

U17 MADAGASCAR KUIJARIBU SERENGETI BOYS KESHO

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Madagascar kesho Jumamosi Julai 30, 2016 itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Serengeti Boys ya Tanzania kwenye Uwanja wa Taifa wa Madagascar.
Serengeti Boys imepiga kambi jijini Antananarivo, Madagascar kujiandaa kucheza na Afrika Kusini katika mchezo wa awali kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6, 2016. Mchezo wa marudiano utafanyika Agosti 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam, ulioko Chamazi-Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Taarifa kutoka kwa mkuu wa msafara Ayoub Shaibu Nyenzi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Vijana, zinasema mchezo huo ni muhimu na Kocha Kocha Mkuu, Bakari Nyundo Shime au Mchawi Mweusi, amesema kwamba amefurahi kupata nafasi hiyo huku Daktari wa timu hiyo, Shecky Francis Mngazija akithibitisha kwmaba vijana hao wako salama.
Nyota walioko kambini ni pamoja na makipa, Ramadhani Awm Kabwili, …

MAZOEZI MAKALI YANAENDELEA KATIKA KAMBI YA SUPER D COACH

Mabondia Faraji Sayuni kushoto na Hassani Kiwale wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM Kariakoo mabondia wote hawo watapanda uringoni agost 8 katika ukumbi wa kobelo pub manzese Dar Es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Hassani Kiwale kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Faraji Sayuni wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika katika kambi ya Super DCoach Uhuru GYM Kariakoo Dar es salaam mabonda hawo watapanda uringoni Agost 8 kuwakabili wapinzani wao katika ukumbi wa kobelo pub manzese Dar Es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS Mabondia Faraji Sayuni kushoto na Hassani Kiwale wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM Kariakoo mabondia wote hawo watapanda uringoni agost 8 katika ukumbi wa kobelo pub manzese Dar Es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Hassani Kiwale kushoto akioneshana umwamba wa kutu…

MAKONDA, MALINZI KUPAMBA UZINDUZI AIRTEL RISING STARS KESHO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kesho Jumamosi Julai 30, 2016 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mashindano ya kuibua na kukuza vipaji vya mpira wa miguu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya Barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.
Sambamba na Makonda, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi naye amethibitisha kuwako kwenye hafla hiyo ambayo mchezo wa kwanza utazikutanisha timu za Ilala Boys dhidi ya Bombom Ilala, Dar es Salaam. Inawakilishwa na mikoa yote mitatu kisoka ambayo ni Ilala, Kinondoni na Temeke kwa pande zote mbili za wavulana na wasichana.

Kadhalika, wakuu wa mikoa mingine ambayo mashindano hayo yatafanyika nao watakuwa wageni rasmi katika mikoa yao ambayo ni Mbeya, Mwanza na Morogoro kwa upande wa wavulana pia Arusha, Lindi na Zanzibar kwa upande wa wasichana.

PROPERTY INTERNATIONAL WADHAMINI TAMASHA LA UZINDUZI WA KITABU CHA SAFARI YA SOKA NCHINI, WATANI WA JADI YANGA, SIMBA, MABALOZI KUUMANA

 Mkurugenzi wa Fedha wa Property International Hashim Thabiti (wa pili kushoto) akimkabidhi Jezi zitakazotumika katika Tamasha hilo Naohodha wa timu ya Wachezaji wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein 'Machinga', wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu Tamasha hilo litakalofanyika Jumamosi hii Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed (kushoto) ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obada na (kulia) ni Mratibu wa Tamasha hilo, Bahari Camari.  Mkurugenzi wa Fedha wa Property International Hashim Thabiti (wa pili kushoto) akimkabidhi Jezi zitakazotumika katika Tamasha hilo Naohodha wa timu ya Wachezaji wa zamani wa Simba, Moses Mkandawile, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu Tamasha hilo litakalofanyika Jumamosi hii Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed (kushoto) ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obad…

PHOTO OF AFRICAN LEADERSHIP FORUM 2016 IN DAR ES TANZANIA

FORMER PRESIDENT OF SOUTH AFRIKA THABO MBEKIFORMER PRESIDENT OF MOSAMBIQUE JOACHIM CHISSANO
CCM YATAMBA KUVUNJA UKUTA YA UKAWA

Japanese Teachers visit Tanzania for Development Education Study