Skip to main content

Posts

Showing posts from July 31, 2016

WAPAKISTANI WA DAWA ZA KULEVYA WAENDELEA KUSOTA RUMANDE

KASEJA AIBUKIA SERENGETI BOYS

JOKATE AJENGA UWANJA JANGWANI

Na Mwandishi wetu Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake yake ya kuchangia jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” amejenga uwanja utakaotumika kwa ajili ya michezo ya mpira wa kikapu na Pete (netiboli) kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani. Uwanja huo ulizinduliwa jijini jana katika hafla fupi iliyofanyika kwenye shule hiyo na kuhudhuriwa na wanafunzi, walimu na viongozi mbalimbali wa serikali. Ujenzi wa uwanja huo umemgharimu Jokate kiasi cha Sh 50 milioni. Akizungumza katika uzinduzi huo, Jokate alisema kuwa ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya michezo nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini. Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ya Tanzania imeadhimia kuondoa changamoto nyingi katika elimu na yeye kuamua kuanzia katika masuala ya michezo ambayo uchangia ufaulu darasani na kuibua…

TAZARA WACHANGIA DAMU WAKIADHIMISHA MIAKA 40 YA UWEPO WAO

 Wakati Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia TAZARA wakiadhimisha miaka 40 ya uwepo wake nchini Tanzania maadhimisho hayo yameenda sambamba na zoezi maalum la kuchangia damu zoezi ambalo limefanyika makao makuu ya TAZARA Dar es salaam Tanzania ambapo wafanyakazi wake wameitumia siku ya leo kuchangia damu zoezi ambalo liliongozwa na mpango wa Taifa wa damu salama Tanzania.
Akizungumza na wanahabari wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU amesema kutokana na uhitaji mkubwa wa Damu uliopo Tanzania wao kama TAZARA wameamua kusitisha shughuli za leo kwa ajili ya kufanya zoezi moja la kuchagia damu zoezi ambalo linaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 40  ya kuanzishwa kwake.
Amesema kuwa zoezi hilo linaonyesha ni jinsi gani wafanyakazi wa TAZARA wamekuwa wakiguswa na maswala mbalimbali ya kijamii hususani swala la ukosefu wa Damu mahospitalini huku akiyataka mashirika mengine na watu mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachangia damu mara kwa mara wawezavyo kwa …

PLIJM AFUKUZA WAANDISHI KATIKA MAZOEZI YA YANGA

KOCHA wa Yanga, Hans van der Pluijm, ameonekana kuchukizwa na tabia ya waandishi wa habari kufika katika mazoezi ya timu hiyo mara baada ya kuamuru Polisi kuwazui wapiga picha wasufanye kazi yao wakati wa timu hiyo ilipokuwa ikifanya mazoezi katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam .

hali hiyo imemkuta kocha huyo mara baada ya kupata  matokeo mabaya  katika michezo mitatu ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo  alitumia zaidi ya saa moja kuwaweka kitimoto wachezaji wake kabla ya kuanza mazoezi.
Pluijm na msaidizi wake, Juma Mwambusi, waliwasili katika Uwanja wa Gymkhana uliopo Posta jijini saa mbili asubuhi kwa ajili ya kuendelea na programu ya mazoezi kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.Wadau wa Sanaa nchini wahamasishwa kudhamini na kufadhili Mashindano ya Urembo

JOSEPH SENGWA AZIKWA KIJIJINI KWAO SHISHI WILAYANI KWIMBA

Ilala yawataka wafanyabiashara kuzingatia muda wa usafi

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaaamimewataka wafanyabiashara kuzingatia muda uliopangwa na Serikali kwa ajili ya usafi wa mazingira katika maeneo yao ya kazi unaofanywa kila ifikapo siku ya jumamosi. Muda uliowekwa kwa ajili ya zoezi hilo ni kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 3:30 asubuhi, ambapo wafanyabiashara wote watapaswa kufungua maduka na masoko yao mara baada ya zoezi hilo kukamilika. Hayo yamesemwa leo na Afisa wa Manispaa hiyo, David Langa wakati alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii kuhusu mwitikio wa wananchi juu ya zoezi la usafi wa mazingira unaofanyika kila jumamosi na kila mwisho wa mwezi. “Nawaomba Wafanyabiashara wenye tabia ya kujichelewesha ili wafike baada ya muda wa usafi pamoja na wale wanaofungua biashara kabla ya muda uliopangwa na Serikali kuacha mara moja kwanilengo la kubadili muda wa kufungua biashara ni kwa ajili ya kufanya usafi” alisema Langa. Akifafanua zaidi Langa aliwatahadharisha wananchi wanaopen…

Wanamichezo waaswa kutotumia dawa za kuongea nguvu katika michezo.