Skip to main content

Posts

Showing posts from August 14, 2016

Watoto waingizwa kwenye jeshi Sudan Kusini

Serikali ya Sudan Kusini imewaajiri watoto wavulana kama wanajeshi wakati huu inapojiandaa kwa mzozo mpya, kwa mujibu wa shirika la Associated Press. Mwanasiasa mmoja mwenye ushawishi anaripotiwa kuongoza shughuli ya kuwaajiri watoto hao, wengine wakitajwa kuwa na umri wa hadi miaka 12 kutoka kijiji kimoja nchini humo.
Nyaraka zinaonyesha kuwa shughuli ya kuwaajiri watoto hao, ilifanyika muda mfupi baada ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuidhinisha azimio wiki moja iliyopita la kutuma wanajeshi 4000 kwenda Sudan Kusini, kuwalinda raia baada ya kuzuka mapigano mapya katika mji mkuu Juba mwezi uliopita.
Mapigano hayo yamekuwa kati ya vikosi watiifu kwa rais Salva Kiir na vile vya makamu wake aliyefutwa kazi Riek Machar ambaye tayari ameikimbia nchi hiyo.
Shirika la kuwahudumia watoto la umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa zaidi ya watoto 650 wameajiriwa na makundi yaliyojihami nchini Sudan Kusini tangu mwanzo wa mwaka huu.
UNICEF sasa ina hofu kuwa mzozo huo mp…

MTWARA GIRLS VINARA WA SAYANSI 2016

Wanafunzi, Nadhara Mresa na Diana Sosoka kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtwara (Mtwara Girls), jana waliibuka mabingwa wa taifa katika Mashindano ya Tano ya Sayansi ya wanafunzi wakati wa maonyesho ya siku mbili yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wanafunzi hao ambao wazo la utafiti wao lilikuwa ‘Umaskini Siyo Suala la Msingi kwa Wanawake Mkoani Mtwara’ (Poverty Is No Longer An Issue For Women In Mtwara Region) waliwashinda wenzao 298 kutoka shule mbalimbali nchini Tanzania ambapo mbali ya kupewa nishani, tuzo kubwa na hundi ya Shs. 1.8 milioni, pia watadhaminiwa safari kwenda jijini Dublin, Ireland kuhudhuria maonyesho ya sayansi kwa wanafunzi wa huko (BTYSTE) yatakayofanyika Januari 2017.
Wanafunzi hao pia watapata udhamini wa shahada ya kwanza katika sayansi kutoka taasisi ya Karimjee Jivanjee Education Scholarships ya jijini Dar es Salaam.Washindi wa pili kwenye mashindano ya mwaka huu ni Bennedict Msangi na William…

MALINZI AMLILIA KELVIN HAULE

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Klabu ya Majimaji ya Songea, mkoani Ruvuma, Humphrey Millanzi kutokana na kifo cha mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Kelvin Haule kilichotokea jana Agosti 18, 2016 kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.

Rais Malinzi amesema, amepokea taarifa za kifo cha Haule kwa masikitiko makubwa.
Rais Malinzi amemuelezea Haule kuwa alikuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya timku ya Majimaji ya Songea na Lipuli ya Iringa hivyo ameacha alama ya ucheshi, kujituma na uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake katika timu ambazo alichezea.
Salamu za rambirambi za Rais wa TFF Malinzi pia zimekwenda kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati huu mgumu wa msiba wa Kelvin Haule.
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu Kelvin Haule mahala pema peponi.
Bwana alitoa, Bwana alitoa, jina la Bwana lihimidiwe.

KUIONA SERENGETI BOYS BUKU 2,000

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kiingilio cha Sh 2,000 kwa mzunguko na Sh 5,000 kwa jukwaa kuu wakati timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 itakapocheza na Amajimbos ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika  zitakazofanyika Madagascar, mwakani.
Mchezo huo utaoanza saa 9.00 alasiri Jumapili Agosti 21, 2016 kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi – Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam utachezeshwa na Mwamuzi Noiret Jim Bacari wa Comoro akisaidiwa na Mmadi Faissoil na Said Omar Chebli wakati mezani atakuwa Ali Mohamed Adelaid huku Kamishna wa mchezo huo atatoka Somalia ambaye anaitwa Amir Abdi Hassan. Jumamosi Agosti 6, 2016, Serengeti ilitoka sare ya 1-1 na Afrika Kusini katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Mji ulioko Kusini – Magharibi mwa jiji la Johannesburg, mabao yote yalipatikana kipindi cha pili yakiwa ni ya penalti kwa kila upande. Afrika Ku…

KESI RASMI KUCHEZEA YANGA

Kamati ya Sheria na Haki za wachezaji imepisha usajili wa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara huku ikiwa imepitisha jina la Hassan Ramadhani ‘Kesi’ kuitumikia Young Africans kuanzia msimu huu 2016/17 baada ya kuona kuwa hana tatizo katika usajili badala yake madai ambayo pande husika zinaweza kudaiana wakati mchezaji anaendeleza kipaji chake.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Richard Sinamtwa imepitia usajili wa timu zote na kujiridhisha kwamba suala la mchezaji Hassan Kessy limeegemea kwenye madai na si usajili ambako Simba ndiye mdai kwa kumtuhumu mchezaji huyo kuwa alianza kuitumikia Young Africans kabla ya kumaliza mkataba wake Simba SC. Mkataba wake ulifika mwisho, Juni 15, 2016. Kama ni madai Simba inaweza kuendelea kumdai Kessy au Young Africans wakati mchezaji huyo anatumika uwanjani kwa mwajiri mpya. TFF inafuatilia na kuangalia haki ya Simba namna ya kupata haki yake baada ya kuwasilisha madai kuhusu kuvunja mkataba na mwajiri wake wa zamani.
Kanuni hazimzuii mch…

LIGI KUU YA VODACOM YAANZA, TFF YATOA ANGALIZO

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17 inatarajiwa kuanza kesho Jumamosi Agosti 20, 2016 kwa michezo mitano huku Bingwa Mtetezi wa Kombe hilo 2015/16, Young Africans ya Dar es Salaam ikisubiri hadi Agosti 31, 2016 kuanza kutetea taji lake.
Young Africans inatarajiwa kusafiri kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kucheza na TP Mazembe kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kufanyika Agosti 23, mwaka huu.  Michezo itakayochezwa kesho ni pamoja na Simba SC itakayoikaribisha Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Taifa, ulioko Chang’ombe Dar es Salaam, katika mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni wakati Azam itakuwa mwenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa Azam FC ulioko Chamazi-Mbagala, nje kidogo ya jiji.
Kadhalika Stand United ya Shinyanga itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga sawa na Mtibwa Sugar itakayoikaribisha Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Manungu uliuoko Turiani, Mvomero mkoani Morogoro wakati Priso…

Makonda abainisha vipaumbele vya mkoa wake

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amewataka watendaji wa mkoa huo kuhakikisha kuwa wanasimamia ubora wa madawati yanayotengenezwa na vyumba vya madarasa vinavyojengwa maeneo mbalimbali ya mkoa huo. Aidha, amezitaka manispaa za mkoa huo kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga madarasa mapya na kuwahamasisha wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo kujitolea kufanikisha mpango huo na kutoa wito kwa madiwani kujiwekea mkakati wa kujenga walau madarasa mawili kwenye Kata zao.

Akifungua kikao chake cha kwanza cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC), Mhe Makonda amesema kuwa licha jiji hilo kukabiliwa na changamoto za kimaendeleo za muda mrefu kwenye sekta ya elimu, miundombinu ya Afya, maji na barabara mafanikio yameanza kuonekana kutokana na juhudi za pamoja za viongozi wa mkoa huo. UPATIKANAJI WA MADAWATI Kuhusu upatikanaji wa madawati amesema kuwa toka Mhe. Rais wa Jamhuri ya Tanzania atangaze kampeni ya upatikanaji wa madawati kwa ajili ya s…