Sunday, August 28, 2016

MUFTI MKUU WA TANZANIA AWANANGA WANAOMSEMA MTANDAONI

>SHEHE Mkuu wa Tanzania , Mufti Aboubakar Zuberi amesema kamwe hawababaishwi wala kuongozwa na Maneno ya kashfa yanayoandikwa mitandaoni dhidi yao.
>
>Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Baraza la Kiislam Tanzania ( BAKWATA), shehe Zuberi alisema ujenzi wa jengo hill umezua maneno ya kashfa dhidi yao lakini wao wanachosimamia ni kuhakikisha baraza hilo linajengeka katika misingi ya amani.
>
>Alisema wapo wanaohoji ujenzi wa jengo hilo kusimamiwa na Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda wakidai ni mkristo jambo ambalo kimsingi halikubaliki na linatakiwa lipuuzwe kwakuwa watanzania hatujafikia kubaguana kidini wala kikabila.
>
>"Yapo maneno mengi yanasambazwa katika mitandao kutukashfu sisi kwa sababu ya ujenzi wa jengo la Bakwata tunaomba waumini jambo hili mlipuuze kwani halina maslahi kwetu...tunachohitaji ni Maendeleo yetu ya kiimani na kijamii," alisema Zuberi.
>
>Aliongeza kuwa anahitaji Jamii ya kitanzania sote kwa pamoja washirikiane katika shida mbalimbali.
>
>Kwa upande wake, Makonda alisema imefika wakati Jamii ikaona umuhimu wa viongozi wa dini katika kuilinda amani iliyopo hapa nchini.
>
>Alisema kwa kutambua umuhimu wa viongozi hao kuanzia sasa ametoa agizo Kwa watumishi wa umma kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa viongozi wa dini kuwapa huduma pindi wanapofika katika ofisi zao.
>
>Makonda alisema viongozi wa dini ndiyo nguzo ya amani na maadili yaliyopo hivi sasa Kwa sababu ya kazi kubwa waifanyao.
>
>"Binafsi naona umuhimu wa watu hawa kwa sababu ya kazi yao kubwa kwa sababu hoi kuanzia leo naomba viongozi mliopo hapa ninawaagiza kuhakikisha katika Mkoa wangu watu hawa wanavyokuja katika. Ofisi zenu wapeni huduma hataka," alisema.
>
>Alisema ujenzi wa jengo hilo utagharimu Sh.Bilioni 5 ambapo mfadhili ambaye ni Taasisi ya GSM ndiyo wamejitolea kujenga jengo hilo.
>
>Makonda alisema ana imani maombi ya viongozi wa dini yatasaidia kuwajenga kiimani na kuwafikisha katika pepo.
>

MBUNGE WA ILEJE JANET MBENE AKABIDHI VIFAA VYA KAZI KWA JESHI A POLISW WILAYA YA ILEJE

 Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbeneakipokea Risala kutoka kwa Ocd Wilaya Ileje
 Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene, akikabidhi Laptop kwa OCD wa Wilaya ya Ileje kw ajaili ya kusaidia kazi katika Wilaya hiyo
 Mbunge wa Ieje , Mh Janet Mbene, akikabidhi Matairi kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi  Wilaya ya Ileje Hamida Mbogo
 Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akipokea mkono wa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje  Joseph Mkude mara baada ya kukabidhi laptop, Photocopy Mashine, Matairi na lim tano

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...