Wednesday, September 21, 2016

RSM YACHANGIA MADAWATI 50 KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM


RSM, Mtandao wa Kimataifa katika ukaguzi wa mahesabu na tathmini za kodi,  umesherehekea madhimisho  tano ya kila mwaka ya Siku Maalumu Duniani ya RSM—kwa kuchangia madawati kwa shule mbalimbali za Dar es Salaam.
Mchango wa RSM, Mtendaji Mkuu wa RSM Afrika Mashariki, Bi. Lina Rantasi alisema kuwa timu ya RSM imedhamiria kusaidia jitihada za Serikali za kuokoa maisha na kuendeleza elimu.
Bi. Ratansi aliendelea kusema,”Kumekuwa na wito mwingi wa kuchangia madawati, Na sisi hatutaki kubaki nyuma, ndo maana tumetoa madawati 50 (3, 750, 000) ili kusaidia watoto wasika chini tena.”
Amesema madawati utasaidia kuongeza uwezo na akili za watoto katika masomo, hivyo kuongeza ufaulu, kwa sababu “motto akikaa chini hata ufahamu wake unakuwa mdogo.
Akipokea madawati hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Madawati-Mkoa wa Dar es Salaam, Hamid Abdul Rahaman, amesema mchango wa RSM utasaidi kukuza sekta ya elimu, na kuwapongeza Mtandao wa RSM kwa kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya kuziwezesha shule kuwa na madawati ya kutosha.

Background:
hadamu kwani benki ya damu imepungua kiasi cha kutokuwa na damu kabisa. Sisi hapa RSM tumeamua kuchukua hatua na kuwahamasisha wengine kufanya kama hivi. Shime tuungane pamoja kuokoa maisha ya Mtanzania.”

 na sherehe kubwa zaidi za dira na malengo ya pamoja ambayo mtandao huu huru wa sita kwa ukubwa wa ukaguzi, kodi na ushauri wa kitaalamu haujawahi kufanya. Kupitia shughuli za aina mbalimbali duniani kote, wafanyakazi katika mashirika ya RSM zaidi ya nchi 120 zilizounganishwa kwa njia ya mshiriki, mteja na matukio ya hisani katika kusherehekea maadili ya msingi ya RSM ya utendaji kazi wa pamoja, uelewa wa kina wa watu, kuchangia wazo na utambuzi kwa manufaa ya mteja.
RSM jijini Dar es Salaam imesherehekea siku hii kwa shughuli  mbali mbali za kijamii kama sehemu ya wajibu wake kwa jamii. Timu imeianza siku kwa kuchangia damu katika Damu Salama. Wakati akihojiwa, Vile vile timu ya RSM, itajumuika na wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Mchanganyiko. “Watoto hawa wanahitaji mapenzi na misaada ya hali na mali. Sisi hapa RSM tunafurahia kuwaonyesha kuwa wao ni sehemu muhimu ya jamii yetu na wanathaminiwa katika ulimwengu huu.” Alisema Mtendaji Mkuu wa RSM. Shirika na wafanyakazi pia limeichangia shule vyakula mbalimbali na vifaa vingine kwa kwa ajili ya wanafunzi.
Kama sehemu ya kuendelea kusaidia sekta ya Elimu, RSM pia imechangia madawati katika jiji la Dar es Salaam kupitia  Kamati ya Madawati Mkoa wa Dar es salaam. Hii ni kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya kuziwezesha shule kuwa na madawati ya kutosha.
Chapa ya RSM inaiwezesha kuelezea vizuri uimara  na uwezo wake wa kutoa huduma duniani kote kama mshauri wa chaguo kwa soko la kati. Mtandao una mashirika katika zaidi ya nchi 120 na unajumuisha wat


Tuesday, September 20, 2016

PIKIPIKI YA WIZI YAGEUKA KIVUTIO KWA WATU DAR

Na Mpekenyuzi wetu, Dar es Salaam
 
UKWELI juu ya pikipiki iliyoko eneo la Veterinary, Temeke, inayodaiwa kuwa na maajabu umejulikana.
  Juzi katika mitandao mbalimbali ya kijamii zilisambaa picha zinazoionesha pikipiki hiyo ikiwa na maelezo kuwa iliibiwa mkoani Tanga na mtu ambaye baada ya kuifikisha kituoni hapo kwa ajili ya kutafuta abiria alianguka na kufa papo hapo.

Zaidi ilidaiwa kuwa pikipiki hiyo haihamishiki wala haisogezeki.

Mpekenyuzi wetu alifika katika eneo hilo na kuzungumza na viongozi mbalimbali kuhusiana na pikipiki hiyo yenye namba za usajili T 684 CJZ.

Akizungumza, mmoja wa madereva wa bodaboda wa kituo hicho ambacho pikipiki hiyo imeegeshwa hapo kwa takribani miaka mitatu sasa pasipo kuibiwa, Shukuru Kiyomola, alisema kile kilichoandikwa mtandaoni hakina ukweli wowote.

“Hii pikipiki ilikuwa ikiendeshwa na mwenzetu anaitwa Frank William, hajafariki kama inavyosambazwa mtandaoni, yupo hai, mara nyingi huwa anabeba abiria usiku, lakini kwa kutumia pikipiki nyingine.

Pikipiki hii ipo hapa takribani miaka mitatu kwa sababu kuna mgogoro kati ya Frank na bosi wake,” alisema.

Alisema si kweli kwamba pikipiki hiyo haihamishiki, lakini alikiri kuwa wanaogopa kuihamisha au hata kuisogeza kwa kuhofia kudhurika kwa kupata mabaya.
 
“Ukiisogeza, inasogezeka, lakini tunaogopa kufanya hivyo hata mwenyewe (Frank) akiwepo, akikuona unaisogeza au hata kuikalia anakufokea uondoke, sasa hatujui ina nini na pengine ndiyo maana haijaibiwa na ipo hapa muda wote huo,” alisema.

Waandishi wa habari hii waliikagua pikipiki hiyo ambayo inaonekana kuwa kuu kuu hivi sasa na kubaini kuwa tayari imenyofolewa sehemu ya kuwekwa funguo ili kuiwasha.
Si hivyo tu, pia walijaribu kuisogeza kujiridhisha na kubaini inahamishika.

Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Bodaboda wa Mtaa huo (WAMAPIME), Godliving Bahati, alisema ni kweli pikipiki hiyo ipo katika eneo hilo kwa muda mrefu.

Alisema Frank ambaye ndiye aliyekuwa dereva wake amekuwa akiwagombeza wenzake na kuacha kuisogelea au kuigusa pikipiki hiyo bila kuwaeleza sababu za msingi.

“Kwa kweli siri ya hii pikipiki anaijua Frank mwenyewe na bosi wake, hata ukimlazimisha aongee akueleze, hasemi, hilo ndilo linalosababisha hofu na mnaweza kugombana kabisa tena ugomvi mkubwa hadi watu wakaja kuwaamulia,” alisema.

Bahati alisema tayari wametoa taarifa juu ya pikipiki hiyo katika Kituo Kidogo cha Polisi- Maganga na katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Veterinary na kwamba wanasubiri viongozi waende kuiondoa.

“Kwa sababu tulishamueleza Frank afanye utaratibu wa kuiondoa, lakini hakuna chochote alichofanya na bado imeendelea kuwepo, hataki kuitoa na hana sababu za msingi anazotueleza,” alisema.

YAGEUKA MAONESHO
Waandishi wa habari hii walishuhudia pikipiki hiyo ikiwa imefunikwa pande zote, licha ya awali kuelezwa kuwa ilikuwa ikiachwa wazi.

Aidha, mbele yake kulikuwa na ubao uliokuwa unasomeka ‘Kuangalia 1,000, Kupiga picha 2,000. Hatari’.
 
Akizungumzia hilo, Mwenyekiti huyo alisema wamechukua uamuzi wa kuifunika pikipiki hiyo kwani tangu taarifa zake zisambae zimesababisha kero katika eneo hilo.

“Unajua tangu iliposambazwa ile picha juzi eneo hili naweza kusema kumekuwa hakuna utulivu, watu wanajaa mno, leo (jana) umekuta wachache kwa sababu tumeifunika.

“Hatujafanya hivi kwa lengo la kupata fedha, bali kurejesha utulivu kama ilivyokuwa awali, watu wamekuwa wakimiminika kuja kuishangaa,” alisema.

Alisema hata usiku imekuwa ikibaki yenyewe katika eneo hilo na hakuna mtu anayethubutu kuisogelea au hata kuiiba, licha ya wizi wa vyombo kama hivyo kushamiri katika jiji la Dar es Salaam.

Alisema wananchi ambao wamekuwa wakifika  kuishangaa pikipiki hiyo wamekuwa wakiogopa kuisogelea na hata kuigusa kwa kuhofia kudhurika.
 
“Wanaogopa eti watanasa au watakufa, hivyo tumeona bora tuifunike iwe kama mwali eneo hili kuwe na utulivu,” alisema.

Wakati mahojiano hayo yakiendelea, watu walianza kujaa katika eneo hilo kuishangaa pikipiki hiyo.

Mpigapicha wa gazeti hili alimuomba mwenyekiti huyo aifunue pikipiki hiyo ili aweze kuipiga picha, hali iliyozusha hofu kwa baadhi ya wananchi.

“Mungu wangu wanaifunua, waiache hivyo hivyo bwana… bora niondoke zangu, kwa kweli haya mambo yanatisha, yaani pikipiki haisogei sijawahi kuona,” alisikika mmoja wa wananchi waliofika katika eneo.

KWELI INASOGEA

Wakati hatua hiyo ya upigaji picha ikiendelea, mwandishi wa habari hii alijaribu kuisogeza ili kuthibitisha kile kilichoelezwa na ilisogezeka.

OFISI YA MTAA
Mwenyekiti wa Mtaa wa Veterinary, Ally Mwamba, alisema alipata taarifa za pikipiki hiyo tangu alipoanza kusimamia usafishaji wa mazingira kwenye mtaa huo.

“Binafsi nilianza kuiona pikipiki ile tangu wakati wa kampeni, nilikuwa nakuta vijana wameweka bendera ya Chama cha Wananchi (CUF), sasa mimi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nikawaomba na yetu iwe inawekwa na zote mbili zikawa zinapepea pale.

“Sasa uchaguzi ukamalizika, tukaanza kutekeleza amri ya Rais John Magufuli ya kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, ndipo wale vijana wakanieleza ukweli juu ya ile pikipiki na kunitaka niwasaidie kuiondoa,” alisema.
 
Alisema vijana hao walimweleza kuwa imekuwapo kwa muda mrefu katika eneo hilo kutokana na mgogoro wa maslahi uliopo baina ya mmiliki wa pikipiki hiyo na dereva wake.

“Kabla ya haya yote kutokea, Frank ambaye ni miongoni mwa waanzilishi wa kituo kile alikamatwa na polisi pamoja na viongozi wenzake na wakavuliwa uongozi kwa ubadhirifu wa fedha za chama.

“Sasa tangu alipotoka ndani hakukuwa na maelewano na mmiliki wa pikipiki hiyo ambaye wamenieleza kuwa anaishi mkoani Mbeya. 

Walisema kulikuwa na mkataba kati ya mmiliki na dereva huyo uliomtaka aiendeshe kwa muda wa kati ya miezi sita hadi mwaka mmoja kabla ya kukabidhiwa kuwa mali yake,” alisema.

Mwenyekiti huyo aliongeza “Frank aliendesha pikipiki hiyo na kumjulisha mmiliki kuwa muda waliokubaliana ulikuwa umekwisha, hivyo amkabidhi kadi ya pikipiki hiyo, lakini mmiliki huyo aligoma na ndipo mgogoro ulipoanzia.”

Alisema alitaka kuchukua hatua ya kuiondoa pikipiki hiyo lakini ameshindwa, kutokana na kuwapo kwa mgogoro huo.

“Naogopa kuiondoa maana baadaye nisije nikajikuta na mimi najumuishwa katika mgogoro huo, nimewaeleza waje mezani wajieleze ili nichukue hatua zaidi ya kuripoti kituo cha polisi, lakini bado sijawaona,” alisema.

Mwamba alisema hata hivyo, hajawahi kusikia wala kuthibitisha iwapo pikipiki hiyo ina miujiza kama wengi wanavyoeleza.

“Ni uzushi tu, pikipiki inasogezeka toka eneo moja hadi lingine kama kawaida,” alisema.

Juhudi za gazeti hili kumpata Frank hazikuzaa matunda, lakini lilimpata aliyekuwa Katibu wa umoja huo ambaye aliondolewa pamoja naye katika uongozi.

“Frank si rahisi kumpata, sina hata namba yake siku hizi, kwani amekuwa akibadilisha kila mara, ninachojua ni kweli ana mgogoro na bosi wake na ndiyo kisa cha kila mmoja kuisusa pikipiki hiyo,” alisema.

KAMANDA WA POLISI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto, alipoulizwa alisema hafahamu lolote juu ya pikipiki hiyo na kuahidi kulifuatilia suala hilo.

“Sijui ndugu mwandishi wewe ndiye wa kwanza kunieleza, nitafuatilia kwa kina ukweli wa suala hili,” alisema.

DK. LWAKATARE: SADAKA ZA JUMAPILI HII KUWALIPIA WAFUNGWA

Na Mwandishi Makini, Dar es Salaam


MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto, Mikocheni B Assemblise of God, Dk. Getrude Rwakatale amesema sadaka zitakazokusanywa kanisani hapo jumapili ya wiki hii zitakwenda kuwalipia faini wafungwa walioko gerezani waliotimiza vigezo lakini wameshindwa kulipa kwa kukosa fedha na hivyo kutupwa magerezani.

Mchungaji Rwakatale ametamka ahadi hiyo juzi mbele ya Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustino Mrema saa chache baada ya kumpongeza na kumteua kuwa msimamizi wa harambee ya kukusanya fedha za kuwalipia wafungwa waliokidhi masharti ya Parole.

Awali akizungumza Mrema alisema kukosekana kwa fedha ya kukamilisha mchakato wa sheria ya Parole kwa wafungwa mbalimbali nchini waliomaliza nusu ya kifungo chao gerezani ni miongoni mwa sababu yakuwepo mrundakano wa wafungwa katika magereza Tanzania.
 https://3.bp.blogspot.com/-hPk0ph6KYxg/V9KIeQmSbpI/AAAAAAAA5RA/RtjhNQYgzoQ2MlIUpZp1Cbnhnyp0NdHkwCEw/s640/IMG_1955.JPG

“Ni lazima maofisa wa parole wafuatilie nakala ya hukumu kwenye mahakama iliyomukuhumu na waende kuonana na uongozi wa kijiji au mtaa ambapo mfungwa atenda kuishi anapotoka gerezani ikiwa ni pamoja na kuonana na familia yake na pia kuonana na watu waliowakosea ili jamii ya eneo hilo itambue kuwa ataachiwa huru” amesema

Aidha, Mrema amewataka maofisa wa parole kote nchini kuwatembelea wafungwa waliopata Parole ili wafungwa wengi wenye sifa za kutolewa kwa sheria ya Parole wasiendelee kuteseka magerezani bali waende kuungana na familia zao sambamba na kuongeza nguvu kazi.

Kutokana na kutotengwa fedha kwa ajili ya kushugulikia suala hilo, Mwenyekiti huyo wa Parole Taifa, amemteua Mama Getrude Lwakatare kuwa mratibu wa kuchangisha fedha kwa kushirikisha viongozi wote wa dini nchini kushiriki harambee kwaajili ya kuchangisha fedha za kuwatoa wafungwa magerezani na kupunguza msongamano katika magereza nchini.

“Napendekeza kufanyike harambee kwenye makanisa yote nchini, siku ya Jumapili moja ili sadaka zote zikatumike kuwalipia faini wafungwa waliopo magerezani” amesema
Mrema amesisitiza kuwa wanaolengwa na Parole siyo wanye makosa ya ubakaji, mauaji, wizi kwa kutumia silaha na makosa mengine.

Naye Mchungaji Lakatare amewataka watanzania kuangalia taifa kwanza kwani kina baba wengi wenye nguvu watarudi katika jamii na kusaidia katika uzalishaji mali sambamba na kutatua matatizo ya kiuchumi na kimaendeleo katika familia zao.

“Tutaunganisha familia zilizo sambaratika na kutaabika baada ya mzazi mmoja kufungwa miaka 6 pengine kwa kukosa faini ya milioni moja tuu, tutaondoa msongamano wa wafungwa na kulinda afya zao kutokana na magonjwa wanayopata wakiwa gerezani” amesema

Mchungaji Lwakatare amesema anaunga mkono jitihada za bodi ya Parole Taifa na siyo kuwalinda waalifu kama ambavyo wengine watatafsiri kwani kurejesha familia ni miongoni mwa kustawisha jamii huku akinukuu maneno ya kidini yanayolenga kuwakomboa walioko kwenye vifungo na taabu mbalimbali ndani ya jamii.

WANAUME WENGI WAJAZANA MOI KWA AJALI ZA BODABODAhttp://www.jamiiforums.com/attachments/bodaboda1-jpg.132439/WANAUME wenye umri wa kati ya miaka 25 hadi 35 ndiyo wanaoongoza kupata ulemavu kutokana na ajali za bodaboda, Takwimu za Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) zimebainisha.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dk. Othuman Kiloloma alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea miguu 600 ya bandia yenye thamani ya Sh milioni 60.

Miguu hiyo imetolewa na  Taasisi ya Legs 4 Afrika ya nchini Uingereza kwa lengo la kuwasaidia wagonjwa wenye mahitaji ya viungo hivyo.


"Kuna ongezeko kubwa la walemavu, takwimu zetu zinaonesha mwaka 2013 tulikuwa tukipokea wagonjwa 15 wa dharura watokanao na ajali, idadi hiyo imeongezeka na sasa tunapokea wagonjwa kati ya 50 - 60 kwa siku,” alisema.
 http://dailynews.co.tz/images/kiloloma.JPG
Dk. Kiloloma (pichani) alisema takwimu hizo zinaonesha robo tatu ya majeruhi hao ni wale wanaotokana na ajali za pikipiki maarufu bodaboda.

Alisema wapo wanaokatika mikono na miguu hali iliyofanya kuongezeka kwa uhitaji wa viungo bandia.

“Gharama za utengenezaji wa viungo hivi inategemea vipuri ambavyo hununuliwa nje ya nchi, baada ya utengenezaji mguu  mmoja hugharimu kati ya Sh milioni 3.5 hadi Sh milioni sita kutegemeana na uzuri wake, chuma na aina ya joint iliyopo pale.

“Hakukuwa na uwiano kati ya vifaa tulivyonavyo na vile vinavyohitajika, gharama yake ni kubwa mno na vifaa tulikuwa tunavichukua toka nchini Ujerumani kuna gharama ya usafiri kuvitoa kule viliko na hata kuvitoa bandarini vinapofika nchini,” alisema Dk Kiloloma.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Watoto Kwanza, Janet Kiwia alisema msaada huo utaiwezesha MOI kutoa huduma kwa gharama nafuu.

Monday, September 19, 2016

ROBO TATU YA WATU WALIOPO GEREZANI NCHINI TANZANIA SIO WAFUNGWAMkurugenzi  wa Legal Services Facility ,Scholastica Julu, akizungumza na wadau waliofika katika hafla ya miaka mitano ya LSf
 Wajumbe wa Bodi wa Legal Services Facility katika picha ya pamoja
 Mwenyekiti wa bodi ya Lsf , Joaquine De Mello akiakabidhi hundi kwa mmoja wa wanufaika.
 Mnufaika wa Ruzuku kutoka tasisi ya  TEWORECakinyoosha hundi yake juu yenye thamani ya shilingi bilioni moja
 Wanufaika wa Ruzuku wakiwa katika picha ya Pamoja na Wajumbe wa bodi
Mkurugenzi  wa Legal Services Facility ,Scholastica Julu, akizungumza na wadau waliofika katika hafla ya miaka mitano ya LSf
 Mkurugenzi  wa Legal Services Facility ,Scholastica Julu, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa  LSf


Na  Humphrey   Shao, Dar es Salaam
WITO umetolewa kwa wadau wa sheria  kusaidia kupunguza mahabusu Magerezani kutokana na wingi wao ambao aikuwa lazima kuweka humo .

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la kisheria lisilo la kiserikali la Legal Services Facility (LSF),Joaquine De Mello,  wakati wa Hafla ya miaka mitano ya shirika hilo na kukabidhi fedha kwa mashirika mapya ya wanaufaika.

“nimeweza kuzunguka magereza yote nchini na kujionea namna gani wafungwa walivyojazana kwa wingi lakini robo tatu ya wafungwa waliopo humo ni mahabusu ambao awaja hukumiwa” alisema Jaji Joaquine De Mello
Aliongeza kuwa imefika wakati wa wasaidizi wa kisheria kuanza kuwasaidia watu kwa nagazi ya vituo vya Polisi ambapo huko wanaweza kupata dhamana kabla ya kufika magarezani.

Kwa upande wake, Scholastica Julu, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo alisema kuwa shirika hilo limeweza kutoa fedha zaidi ya Bilioni ishirini kwa mashirika mbalimbali nab ado litaendelea kutoa hili kuweza kusaidia wasaidzi wa kisheria na Mashirika yanayowasimamia .

Alisema kuwa wameweza kupokea changamoto ya usafiri kwenye baadhi ya mikoa na kama shirika wanalifanyia kazi hilo swala hili waweze kutatua tatizo hilo kwa wasaidizi wanaofanya kazi hiyo kwa mazingira hayo magumu. 

ENDDDDD

RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KUWEZESHA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO DHIDI YA WATENDAJI WASIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI.

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 09 amezindua Mfumo wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo ...