Sunday, September 25, 2016

Unaambiwa hii ndiyo Darubini kubwa zaidi duniani

China imeanza kutumia darubini kubwa kabisa ya redio duniani ambayo imesha anza kupata habari kutoka nyota iliyoko masafa yatayochukua zaidi ya miaka elfu moja kwa mwangaza kufika.Darubini hiyo itawasaidia wanasayansi kuuelewa zaidi ulimwengu
Darubini hiyo itawasaidia wanasayansi kuuelewa zaidi ulimwengu na kutafuta viumbe katika sayari nyengine.
Mamia ya wajuzi wa elimu ya nyota na washabiki, wamehudhuria uzinduzi wa darubini hiyo.
Sinia kubwa ya darubini imewekwa kati ya milima kadha katika jimbo la Guizhou, baada ya watu elfu nane kuhamishwa kujenga mtambo huo.- BBC

CUF wajibu ushauri wa Msajili

Kamati tendaji ya CUF imekataa ushauri wa msajili wa vyama vya siasa juu ya malalamiko yaliyotolewa na Ibrahim Lipumba.
http://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/Waziri-mazrui.jpg
NASSOR AHMED MAZRUI,
NAIBU KATIBU MKUU CUF.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Imetolewa leo Tarehe -25/9/2016

Na NASSOR MAZRUI

KAMATI YA UTENDAJI YA TAIFA IMEKATAA MAONI NA USHAURI ULIOTOLEWA NA MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI

Jana tarehe 24/9/2016 KAMATI YA UTENDAJI YA TAIFA YA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-Chama cha wananchi) imekutana katika kikao chake cha dharura kilichofanyika kwenye Makao Makuu ya Chama, Zanzibar. Kamati ya Utendaji Taifa imejadili taarifa kuhusiana na MAONI NA USHAURI WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI pamoja na KITENDO CHA UVAMIZI WA OFISI KUU YA CHAMA BUGURUNI, DAR ES SALAAM kilichofanywa na Ibrahim Lipumba na kundi lake la wahuni na kusababisha uharibifu wa mali za Chama. Kutokana na matukio hayo Kamati ya Utendaji ya Taifa imefikia maamuzi yafuatayo;

1. Baada ya kupitia Maoni na Ushauri wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini juu ya malalamiko yaliyowasilishwa katika ofisi yake na Ibrahim Lipumba na wanachama wenzake waliochukuliwa hatua za kinidhamu na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, Kamati ya Utendaji ya Taifa inakataa na kupinga kwa hoja thabiti ushauri na maoni yaliyopendekezwa na Msajili na badala yake inaendelea kusimamia maamuzi ya Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa wa tarehe 21/8/2016 uliokubali kujiuzulu kwa Ibrahim Lipumba kama Mwenyekiti wa Chama na maamuzi ya Baraza Kuu la Uongozi Taifa yaliyofikiwa katika kikao chake cha tarehe 28/8/2016 juu ya kuwasimamisha uanachama Ibrahim Lipumba, Magdalena Sakaya, Maftaha Nachuma, Abdul Kambaya, Masoudi Mhina, Thomas Malima, Ashura Mustafa, Kapasha H. Kapasha, Musa Haji Kombo, Habibu Mnyaa, Haroub Shamis na kumfukuza uanachama Shashu Lugeye.

Katiba ya Chama haina kifungu chochote kinachompa mamlaka Msajili wa Vyama vya Siasa kupokea rufaa kuhusiana na maamuzi ya vikao vya Chama na kubatilisha maamuzi ya vikao hivyo.

2. Kutokana na kitendo cha kuvamia Ofisi Kuu ya Chama, Buguruni na kusababisha uharibifu wa mali za Chama, Kamati ya Utendaji ya Taifa kwa mujibu wa ibara ya 85(5) na ibara ya 108 ya Katiba ya CUF ya mwaka 1992 Toleo la mwaka 2014 imeitisha kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa kitakachofanyika tarehe 27/9/2016 siku ya Jumanne, kuanzia saa 4 asubuhi kwenye Makao Makuu ya Chama, Zanzibar.4

Kwa mujibu wa Ibara ya 12 (6), (7) na (16) ya Katiba ya CUF ya mwaka 1992 Toleo la mwaka 2014, Kamati ya Utendaji ya Taifa imeandaa ajenda na kumfikisha Ibrahim Lipumba mbele ya Baraza Kuu la Uongozi Taifa na kutakiwa kujieleza na kujitetea kwa nini Baraza Kuu la Uongozi Taifa lisimchukulie hatua za kinidhamu kwa matendo yake aliyoyafanya jana.
Ibara tulizozitaja hapa zinazungumzia;

“Kulinda heshima ya Chama kwa kuwa na tabia njema, kutekeleza masharti ya katiba ya Chama, kutii kanuni za Chama, kutii sheria na sheria ndogondogo za serikali iliyoundwa kihalali na pia, kwa busara, kukosoa utekelezaji mbaya wa serikali kwa hoja za msingi ili kuendeleza maslahi ya Chama, maslahi yake mwenyewe, maslahi ya wanachama wenzake, maslahi ya nchi na maslahi ya raia wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.” Ibara 12(6)

“Kuwa mwaminifu kwa Chama na serikali zilizoundwa kihalali na kwa ridhaa ya wananchi na kuwa tayari kuwatumikia watu kwa juhudi, maarifa na vipaji vyake vyote.” Ibara 12(7).

“Kukilinda kutokana na maadui wa ndani au wa nje wanaokusudia kukihujumu, kukiua, kukigawa au kukidhoofisha.” Ibara 12(16).

HAKI SAWA KWA WOTE
____________________________________

NASSOR AHMED MAZRUI,
NAIBU KATIBU MKUU CUF.
 

Rais Erdogan aweka rekodi ya wafuasi kwenye Twitter

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameweka rekodi kwenye mtandao wa jamii wa Twitter kwa idadi kubwa ya wafuasi.
https://pbs.twimg.com/profile_images/660430083753136128/dzWitvi2_400x400.jpg
Rais Erdogan
Baadhi ya maelezo yaliyonukuliwa kutoka kwenye hotuba ya Erdogan ya mkutano wa baraza kuu la UN nchini Marekani yalisambazwa kwenye mtandao wa jamii wa Twitter kwa lugha 4 tofauti.
Maelezo hayo yanayojumuisha suala la wakimbizi wa Syria alilozungumzia kwenye mkutano wa 71 wa baraza kuu la UN yalifikia mamilioni ya watumiaji wa Twitter.
Rais Erdogan alivutia wafuasi wengi kwa ujumbe wake uliosambazwa kwa kutumia hashtag ya #ErdoganSautiYaWanyonge.
Kwa majibu wa takwimu zilizotolewa na mhusika kuu wa akaunti ya Twitter ya Erdogan , Ismail Cesur, maelezo hayo yaliyosambazwa kwa lugha za Kituruki, Kiingereza, Kifaransa na Kiarabu yalisomwa na watumiaji milioni 13,360,000.
Jumbe 12 zilizosambazwa kwa lugha ya Kituruki zilifikia watumiaji 4,780,000.
Ujumbe mmoja pekee wa uliosambazwa pia umeweza kufikia watumiaji zaidi ya milioni.

Emoji mpya za WhatsApp kwa watumiaji wa Android

Programu ya mawasiliano ya WhatsApp inayohudumia watumiaji wengi wa simu za Android imeleta maboresho. Kufuatia maboresho hayo, WhatsApp sasa itawezesha wateja wake kutumia emoji kubwa kwenye vifaa vyao vya Android. http://thenextweb.com/wp-content/blogs.dir/1/files/2016/02/Old-New-Emoji-WhatsApp-1200x600.jpg
 Hapo awali WhatsApp iliweza kuleta maboresho hayo kwa watumiaji wa vifaa vya Apple vinavyoendeshwa na mfumo wa iOS 10. Maboresho hayo pia yatawezesha wateja kutumia emoji za mfumo wa 3D na LGBT. Miongoni mwa emoji hizo mpya ni kama vile bastola za watoto za kutoa maji badala ya picha za bunduki.

Pambano la Tyson v/s Klitschko laahirishwa

Bingwa wa masumbwi uzani mzito kutoka Uingereza Tyson Fury ameahirisha maregeo ya pambano lake na Wladimir Klitschko kwa mara ya pili kwasababu ''afya yake hairidhishi''.
http://www.boxingnewsonline.net/wordpress/wp-content/uploads/2015/12/Tyson-Fury.jpg
Tyson Fury
Mapromota wake hawakufichua taarifa zaidi lakini wamesema " hali yake ni mbaya mno na haimruhusu kushiriki pambano hilo".
Fury, mwenye umri wa miaka 28, alimshinda Klitschko kutoka Ukraine kwa pointi katika pambano la kwanza mnamo Novemba mwaka jana.
Regeleo la pambano la awali lilipangwa Julai 9 katika uwanja wa Manchester Arena, na liliahirishwa hadi Juni baada ya Fury kuvunja fupa la kisigino chake.
Pambano jipya la maregeo kati ya mabondia hayo wawili liliangwa kufanyika Octoba 29.
"Tyson sasa inabidi fanayiwe matibabu anayohitaji ili aweze kupona kikamilifu," Hennessey Sports iliongeza.
"Tunaomba radhi kwa wote wanaohusika katika pambano hili na mashabiki wote wa masumbwi waliotazamia maregeo hayo. Ni wazi kuwa Tyson pia amehuzunishwa na hali ilivyo.
"Tutatoa taarifa zaidi katika muda unaofaa."

Balaa lazidi kuiandama Samsung

Kampuni ya utengenezaji vifaa vya electronic ya Samsung yenye makao yake makuu, Korea Kusini imezidi kuandamwa na balaa baada ya simu nyingine ya Note 2 ya kampuni hiyo kudaiwa kufuka moshi.
Ndege ya kampuni ya IndiGo
Taarifa zinasema kuwa wafanyikazi wa kampuni moja ya ndege nchini India walilazimika kutumia kifaa cha kuzima moto ili kuizima simu aina ya Samsung iliokuwa ikifuka moshi.
https://cnet3.cbsistatic.com/img/mEmWXxd4RLjukVv_D5uGEVLNjKw=/770x433/2012/10/23/7f2da670-8ae8-11e2-9400-029118418759/-2.jpg
Samsung Note 2
Simu hiyo ya Note 2 ilikuwa ikitoka miale ya moto kulingana na taarifa kutoka kwa kampuni ya ndege ya Airline Indigo.
Hatua hiyo ya haraka iliochukuliwa na wafanyikazi hao ilisaidia ndege hiyo kutua salama katika uwanja wa ndege wa Chennai,ikiwa ndio lengo la safari hiyo.
https://cdn2.pcadvisor.co.uk/cmsdata/features/3644465/note7_colours.jpg
Simu za Note 7 zilizorejeshwa kiwandani kutokana na matatizo ya betri
Kisa hicho kimetokea wakati ambapo Samsung inazirudisha simu aina ya Note 7 kutokana na matatizo ya betri.
IndiGo imesema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa wakati wa kisa hicho katika ndege ya 6E-054 iliokuwa ikitoka Singapore kuelekea Chennai.

Soma hapa kama unatumia Yahoo!

MTANDAO uliojizolea umaarufu kwenye nyanja ya utoaji huduma za barua pepe miaka ya nyuma wa Yahoo! ulionunuliwa Julai mwaka huu na kampuni ya Verizon umedukuliwa na kusababisha kuvuja kwa taarifa mbalimbali za watumiaji wa mtandao huo. Taarifa zinasema kuwa zaidi ya akaunti milioni 500 za watumiaji wa Yahoo! zimedukuliwa.http://www.brecorder.com/images/2016/04/yahoo0.jpg
Mapema wiki hii Yahoo! walisema kuwa mwishoni mwa mwaka juzi wadukuzi walifanikiwa kudukuwa database za kampuni hiyo na kuiba baadhi ya taarifa za watumiaji wa mtandao huo.
Msemaji wa Yahoo! amesema kuwa udukuzi huo ulifanywa na watu waliolipwa na serikali, ambapo taarifa zilizodukuliwa na kuibwa ni, Password ywira, barua pepe, namba za simu, majina na tarehe za kuzaliwa za watu mashuhuri.http://i2.cdn.turner.com/money/dam/assets/160922095225-yahoo-hack-780x439.jpg
Umhimu wa kubadili pasword
Ili kujiweka katika mazingira salama zaidi ni vyema kama wewe ni mtumiaji wa mtandao huu ukajenga utaratibu wa kubadili paswedi mara kwa mara.
Kwani itakufanya ujilinde kwa kiasi fulani na wadukuzi ambao wanazidi kuongezeka kila kukicha tena kwa kutumia mbinu za kisasa hali ambayo inaweza kupelekea taarifa zako kutumiwa kwenye kufanya uhalifu.

Snapchat yazindua miwani yenye kamera

Kampuni ya Snapchat ambayo ni mshindani mkubwa wa Facebook imezindua miwani ya aina yake yanayomuezesha mtu kupiga video na kuisambaza katika mtandao huo wa kijamii.
Snapchat wamesema kuwa miwani hiyo iliyopewa jina 'Spectacles', ina nasa kumbukumbu za watu kupitia kamera ndogo.https://assets.bwbx.io/images/users/iqjWHBFdfxIU/ixxv6jnFUSe4/v0/1200x-1.jpg
mtandao huo wa Snapchat umekuwa ukijiongezea umaarufu kila kukicha kwenye mitandao ya kijamii inayotumiwa kutuma ujumbe, zikiwemo picha na video ambazo hufutwa baada ya kuonekana mara moja.
Lakini kifaa hicho kipya na kampuni hiyo kubadilisha jina kutoka Snapchat na kujiita Snap, zinadhihirisha azma ya kampuni hiyo kupita kiwango cha kuwa mtandao wa ku chati.
https://static.independent.co.uk/s3fs-public/styles/article_large/public/thumbnails/image/2016/09/24/11/spectacles.jpg
Miwani ya Snap kwenye tangazo la biashara
Katika tangazo lake la biashara, Snap inasema miwano hiyo ya kutuma video ina lensi ya ukubwa wa digri 115, iliyo na upana zaidi kuliko kamera za kwenye simu za kisasa.
Snapcht wameongeza kuwa miwani hiyo pia ina uwezo wa kurekodi video kwa hadi sekundi 10 kwa mara moja.
huku picha zake hizo zikitumwa moja kwa moja kwenye mtandao huo wa kijamii ili mtu aweze kuzisambaza kwa wafuasi wengine wa mtandao huo.
Mkurugenzi mkuu wa Snap,Evan Spiegel(26), ametaja miwani hiyo kama chombo kinachomuezesha mtu kuona kumbukumbuku nzuri kama walivyoiptia kwa mara ya kwanza

Shekau: Bado sijafa niko hai

Kiongozi anayekabiliwa na upinzani wa kundi la Nigeria Boko Haram Abubakar Shekau, ametoa ujumbe wa sauti akikanusha madai ya jeshi kuwa aliuawa au amepata majeraha mabaya wakati wa mashambulizi ya angania mwezi uliopita.
https://www.360nobs.com/wp-content/uploads/2015/05/Abubakar-Shekau.jpg1_-640x431.jpg
Abubakar Shekau
Shekau alionekana mwenye afya kwenye kanda hiyo ambayo alizungumza kwa lugha za kiarabu,Hausa na Kanuri.
Shirika la Habari la BBC limeripoti kuwa, haijabainika sauti hiyo ilirekodiwa lini. Bado jeshi la Nigeria halijazungumza chochote.
Mapema mwezi huu kundi la Islamic State ambalo Boko Haram limetangza kulitii, lilitangaza kuwa wadhifa wa Shekau ulikuwa umechukuliwa na kiongozi asiye maarufu Abu Mus'ab Albarnawi. Bado Shekau anasema kuwa ndiye kiongozi. 
"Ieleweke kwamba taarifa zote zilizowahi kuripotiwa kuwa nimeuawa niza upotoshaji na uongo mkubwa kwani bado nipo hai kama mnavyonisikia kwenye ujumbe huu wa sauti," amesikika Shekau kwenye sauti hiyo.

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...