Thursday, October 6, 2016

FAST JET YAANZISHA SAFARI ZA NDEGE MPYA NCHINI, KUANZA RASM KESHO WANANCHI WAOMBWA KUCHANGAMKIA

 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kuanza kutumia ndege mpya aina ya Embraer 190 kusafirisha abiria. Kulia ni Ofisa Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Lucy Mbogoro.
 Ofisa Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Lucy Mbogoro (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse (katikati), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Huduma kwa Wateja, Christina Kausan.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Dotto Mwaibale

WANANCHI wametakiwa kuchangamkia usafiri wa ndege wa Kampuni ya Fast jet baada ya kampuni hiyo kuanza kutumia ndege mpya aina ya Embraer 190 ambayo ni nafuu zaidi kwa matumizi.

Mwito huo umetolewa na Dar es Salaam leo na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse wakati akizungumza na waandishi wa habari jana kuwa ndege hizo ni rahisi kwa matumizi ya usafiri hapa nchini. 

Alisema kuwa ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 108  aliongeza kuwa zitahudumia kwa miezi 6 huku ikitoa nafasi kwa mafunzo wa marubani wa Fast jet hapa nchini.

Aliongeza kuwa kwa kuwa Fast jet hapa nchini imepata hasara kiuendeshaji hivyo ndege hizo kwa kuwa hazitumii matufa mengi itasaidia kuiimarisha biashara.

" Hii imetokea tu kuwa wakati serikali imeleta aina ya ndege zisizotumia mafuta mengi na sisi tulikuwa pia tumeshaanza mchakato huo na hivyo kwa sasa binafsi naona kuwa watanzania watanufaika zaidi" alisema Corse.

Pia aliipongeza serikali kwa kuleta ndege mpya aina ya Bombardier 8, Q400 ambazo zinaenda mikoa ya Rukwa, Mara, Kagera na Dodoma ambapo ndege za Fast jet hazifiki.

Alisema kwa kuwa lengo la Fast jet ni kuwapatia watanzania huduma nafuu za usafiri wa anga hivyo inafurahia pale ambapo inaona kuwa ndege za serikali zinafika mikoa ambayo Fast jet haifiki. 

Alisema kuwa kwa kupeleka ndege kwenye mikoa hiyo ni hatua ambayo inatimiza lengo la Fast jet la kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za anga kwa bei rahisi na kwa wakati.

SERIKALI YARUHUSU WIMBO WA CHURA WA MSANII SNURA KUPIGWA

 Snura Mushi
 Msemaji wa Msanii Snura Baraka Nyagenda. akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salamm leo.
 Msanii Snura Mushi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu kupigwa kwa wimbo wa chura ya kuufunga kwa kuwa haukuwa na maudhui mazuri ya kitanzania. Kushoto ni Msemaji wake, Baraka Nyagenda.
Mkutano na wanahabari ukiendelea. N a Dotto Mwaibale

SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu kupigwa kwa wimbo wa chura wa msanii Snura Mushi baada ya kuufunga kwa kuwa haukuwa na maudhui mazuri ya kitanzania.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Snura Mushi alisema wimbo wake na video umeruhusiwa kupigwa baada ya audio ya chura kufanyiwa marekebisho na kuifanya kuwa katika maudhui ya kitanzania.

Alisema ruhusa hiyo imetolewa kwa barua iliyoaandikiwa Septemba 26, 2016 yenye kumbukumbu HA.26/375/01'B'/137 ambayo gazeti hili lina nakala yake.

Kupitia mkutano huo msanii Snura Mushi kwa mara nyingine aliomba radhi kwa watanzania na Serikali kwa ujumla kwa usumbufu walioupata kwa video yake ya kwanza na kuwaomba waendelee kuiona video mpya iliyorekebishwa baada ya kuifuta ya kwanza.

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI-Afya Dkt.Zainabu Chaula atembelea Wizara ya Afya

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI-Afya Dkt. Zainabu Chaula ametembelea   Wizara  ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kukutana na Waziri Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Makatibu wa Wizara hiyo.

Dk. Zainabu Chaula ametembelea Wizara hiyo hii ni baada ya kuapishwa rasmi na Ikulu Jijini Dar e Salaam na Rais Dk. John Pombe Magufuli, Septemba 26.2016. Akiwa Wizarani hapo amepata kufanya mazungumzo ya kiutendaji kwa pamoja akiwemo Waziri Afya na Makatibu wake.
Mwisho.
dsc_2166Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI-Afya Dkt. Zainabu Chaula akisalimiana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea Wizarani hapo mapema jana Oktoba 4.2016

dsc_2157Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI-Afya Dkt. Zainabu Chaula akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya alipomtembelea ofisini kwake Wizarani jana Oktoba 4.2016.
dsc_2169Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI-Afya Dkt. Zainabu Chaula akifuatiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya
dsc_2175Picha ya pamoja: Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI-Afya Dkt. Zainabu Chaula akifuatiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya na Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Mh. Siaba Nkinga.

MD UBUNGO AWATAKA WATUMISHI WA MANISPAA YA UBUNGO KUZINGATIA NIDHAMU NA UADILIFU KATIKA KAZI

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo (Katikati) akisikiliza kwa makini maoni ya watumishi wa Manispaa hiyo wakati wa kikao cha pamoja na watumishi wa Manispaa hiyo

 Waratibu wa elimu wakisikiliza kwa makini maelekezo ya utendaji kazi kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na waratibu wa elimu Kata wakati wa kikao cha Kazi


Watumishi wa Manispaa ya Ubungo wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo wakati wa kikao cha kazi

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Watumishi wote wanaofanya kazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wametakiwa kufanya kazi katika hali ya ukweli, Uwazi, Ufanisi, Uadilifu, Kujituma na kuwa na nidhamu katika utendaji ili kukuza ufanisi wa Changamoto zinazowakabili wananchi mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John L. Kayombo wakati wa kikao cha kazi na waratibu wa elimu kutoka kata 14 na wakuu wa shule za msingi zilizopo katika Manispaa hiyo mara baada ya ukaguzi wa shule za msingi Temboni Msigani.

Kayombo amezuru katika maeneo tofauti tofauti katika Halmashauri hiyo ikiwemo Shule ya Msingi Temboni ambapo alikutana na kamati ya shule sambamba na kufanya ukaguzi wa vyumba 8 vya madarasa utakaogharimu kiasi cha Shilingi milioni mia moja sitini (Mil 160) na matundu kumi ya choo ambayo yanataraji kugharimu kiasi cha shilingi milioni thelathini na mbili (Mil 32) ambapo pia ukarabati wa shule wenyewe utagharimu kiasi cha shilingi milioni kumi (Mil 10).

Kayombo alisema kuwa fedha hizo zimetolewa na serikali kuu kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu na kuhakikisha watoto wa masikini wanapata elimu bora katika mazingira rafiki.

Ziara ya kazi ya Mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Ubungo John L. Kayombo kwa kukutana na waratibu wa elimu kutoka kata 14 za Halmashauri hiyo pamoja na wakuu wa shule za msingi imejikita zaidi katika kuamsha ari na ufanisi katika utendaji na kuwakumbusha watendaji wote majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.

Ziara hiyo inatazamiwa kuwa kila mtumishi sasa atakumbuka majukumu yake katika utendaji na kuyafanya ipasavyo kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria za muongozo wa watumishi wa umma.
Akizungumza na www.wazo-huru.blogspot.com DED Kayombo alisema kuwa watumishi wa serikali wanapaswa kutambua kuwa hawatakiwi kujiingiza na kufanya siasa zisizo na tija badala yake wanapaswa kuwajibika zaidi katika kuwatumikia watanzania na kuakisi kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya Hapa Kazi Tu chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Kuzuru katika maeneo mbalimbali kukagua miradi na kujionea shughuli za maendeleo ni utaratibu ambao amejiwekea Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo John L. Kayombo ili kufahamu maeneo yake ya kiutendaji na kuamsha ari katika uwajibikaji na ufanisi wa kazi.

Baada ya ziara hiyo ya kukutana na waratibu Kata katika Manispaa ya Ubungo DED Kayombo hii leo amekutana tena na watumishi wote wa Manispaa kikiwa ni kikao chake cha kwanza kukutana na Watumishi wote kwa lengo la kutoa miongozi na maelekezo mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya ubungo Mkurugenzi huyo amesisitiza ufanyaji kazi kwa bidii, ushirikiano mahali pa kazi, upendo na uaminifu ili kuiwezesha ubungo kusonga mbele katika maendeleo na kuwafanya wananchi wa Ubungo kuimarika katika sekta ya uchumi.

DED Kayombo amewataka watumishi hao kuwa wabunifu katika utendaji kazi wao ili kuongeza mapato ya ya manispaa ya kurahisisha Manispaa hiyo katika ufanisi wa kazi na kuwahudumia wananchi kirahisi.

DC MTATURU AWAAGIZA VIONGOZI WA VIJIJI VYOTE KUSOMA MAPATO NA MATUMIZI NDANI YA WIKI MOJA

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakazi wa Kata ya Ntuntu wakati kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake Wilayani Ikungi
Wananchi wa Kata ya Ntuntu wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka akisisitiza jambo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kuwahutubia wananchi wa kata ya Ntuntu


Kaimu katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Dandala Mzunguor akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa hadhara kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turukaili naye amkaribishe Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kuwahutubia wananchi wa kata ya Ntuntu
Wananchi wakimsikiliza kwa Makini Mkuu wa Wilaya akitoa maagizo ya mpango wa maendeleo ya Wilaya
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza maelekezo yaliyopelekea kukwama kwa ujenzi wa maabara katika shule ya Sekondari Ntuntu
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Ntuntu
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Taru kuwa na nidhamu na kusoma kwa bidii
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza sababu zilizochangia kukwama kwa ujenzi wa maabara ya shule ya Sekondari Lighwa
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua ulipoishia ujenzi wa maabara ya shule ya Sekondari Lighwa
Wakazi wa Kijiji cha Mwisi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizitaja siasa taka kuwa ndizo zilizokwamisha kupatikana kwa maendeleo katika Wilaya ya Ikungi

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wake wa kazi katika kata ya Lihgwa


Na Mathias Canal, Singida

Viongozi wa Vijiji vyote Wilayani Ikungi Mkoani Singida wameagizwa kusoma mapato na matumizi ili kuwarahisishia wananchi kufahu jinsi fedha zao zinavyotumika katika ukweli na uwazi na kutoa fursa kwa wananchi kupata nafasi ya kuhoji ili kujiridhisha pale wanapokuwa na mashaka.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa mikutano yake ya kazi katika Wilaya hiyo iliyoanza jana kwa kutembelea kila kata kukagua miradi ya maendeleo na kufanya mikutano ya hadhara yenye lengo la kujua maeneo ya utendaji na kuwakumbusha wenyeviti na watendaji wa Vijiji na Kata kutambua majukumu yao na kuyapatia majibu sawia na kubadili changamoto kuwa fursa.

Dc Mtaturu ameagiza kufanyanyika uchunguzi ili kubaini kama kuna watendaji wamehamishwa kazi na wanatuhumiwa kuhujumu mapato ya serikali na michango ya wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo kurudishwa haraka iwezekanavyo ili kutoa majibu ya tuhuma hizo na kuchukuliwa hatua endapo watabainika kujihusisha na kadhia hiyo.

Katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Ntuntu na Kata ya Lighwa Dc Mtaturu amesema kuwa wazazi wote ambao watoto wao wanajihusisha na utoro watachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo ili kubaini chanzo cha utoro huo kama unasababishwa na wazazi wenyewe ama wanafunzi kujihusisha na makundi ovu ikiwemo kufanywa vijakazi katika maeneo ya mijini.

Dc Mtaturu amewakemea wanasiasa ambao wamezuia wananchi kuchangia ujenzi wa nyumba za walimu, Ujenzi wa Shule na maabara huku wakiwaahidi kuwa serikali itajenga kila kitu na kuongeza kuwa serikali kuu haiwezi kufanya kila jambo badala yake wananchi kwa umoja wao wanapaswa kushiriki katika uchangiaji wa huduma za kijamii.

Mkuu huyo wa Wilaya amewaagiza watumishi wote wa serikali ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Kata kufanya kazi kwa haki, Usawa na uwazi na kiwashirikisha wananchi katika kila jambo linalohusu vipaombele vya maeneo yao.

Pia amevitaka vijiji 39 ambavyo havijapimwa kupimwa na kurahisisha upangaji wa matumizi bora ya ardhi ili kuepuka migogoro mbalimbali ya ardhi ambayo imekuwa ni changamoto kubwa katika maeneo mengi nchini.

Akizungumzia kadhia ya maji safi na salama kati kata hizo mbili Dc Mtaturu alisema kuwa serikali inatambua kuwa hakuna maji safi na salama hivyo imejipanga kuzikabili changamoto hizo katika kipindi cha muda mfupi.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wamempongeza mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kwa kufanya ziara katika Kata hizo kwani wana miaka zaidi ya 10 hawajawahi kutembelewa na Mkuu wa Wilaya wala Mkurugenzi.

Wananchi hao wametoa mifano ya Wakuu wa Wilaya waliowahi kufika wakati huo Wilaya ikiwa haijagawanywa kitoka Wilaya ya Singida kuwa ni pamoja na aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Hawa Ngurume (Marehemu) sawia na Mhe Abas Kandoro ambaye hivi karibuni alistaafu akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ameivunja kamati ya maji katika Kijiji cha Ntewa B iliyopewa mamlaka ya kuendeleza upatikanaji wa huduma ya maji na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka kufatilia ili kujua chanzo cha kukosekana kwa maji katika kijiji hicho ilihali miundombinu ya kupatikana maji kijijini hapo imekamilika vyema.

Dc Mtaturu alisema kuwa Demokrasia inayohubiriwa na baadhi ya wanasiasa nchini inapaswa kuwa Demokrasia ya kweli kwa kuwa na nidhamu na mamlaka pia kutoitukana serikali na kupinga kila jambo linalofanywa na serikali.

Sambamba na hayo pia Dc Mtaturu amemuagiza Mkuu wa Polisi Wiliya ya Ikungi kuwakamata haraka iwezekanavyo wazazi wa watoto watatu ambao ni wanafunzi wa katika Shule ya Sekondari Lighwa waliopatiwa mimba ili kutoa taarifa ya watu waliowapa ujauzito huo na kuchukuliwa hatua.

Tigo yadhamini mbio za Tigo Igombe Charity Marathon

Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza na wanariadha wa Tigo Igombe Charity Marathon, kabla ya kuzindua mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni wa wiki iliyopita mjini Tabora.
Mtoa huduma Mwl Mwajuma Mwamba akiwasajili wanariadha mara baada ya kumaliza mbio za Tigo Igombe Marathon zilizofanyika mjni hapa.
Mkurugrnzi wa Tigo kanda ya Ziwa Ally Maswanya akizungumza na wanariadha wa mbio za baiskeli kabla ya kuzindua shindano hilo.
Wanaridha wakiwa tayari kusubiria kipyenga cha Tigo Igombe Charity Marathon
Vijana wa mkoa wa Tabora wakishindana kukimbia wakati wa mashindano ya Tigo Igombe Charity Marathon yaliyofanyika leo mjini hapa.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza na mwakilishi wa Tanzania Breweries Ltd ambao ni wadhamini wenza wa mbio za Tigo Igombe Marathon, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa, Ally Maswanya, mbio hizo zimefanyika leo mjini hapa.

UHAKIKI NA UBORESHAJI WA TAARIFA ZA TIN KWA MKOA WA DAR ES SALAAM KUMALIZIKA OKTOBA 15/2016

2
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo akifafanua jambo kwa waandshi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika Makao Mkuu ya TRA. Kulia ni Gabriel Mwangosi Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA.
Zikiwa zimebaki siku tisa kumaliza zoezi la uhakiki na uboreshaji wa taarifa za Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa mikoa ya kodi ya Dar es salaam na Zanzibar, tayari Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imehakiki na kutoa vyeti vipya vya TIN 15,467.
Zoezi la ukakiki na uboreshaji wa taarifa za TIN linaendelea hadi tarehe 15 Oktoba 2016 katika ofisi zilizoanishwa hivyo wananchi wenye TIN wanashauriwa kuhakiki TIN zao kabla muda uliowekwa haujaisha kwani baada ya muda huo kuisha TIN ambayo itakuwa haijahakikiwa itaondolewa katika mfumo wa TIN wa TRA.
1
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo katikati akizungumza na waandishi wa habari  wakati alipokuwa akitangaza makusanyo ya kodi ya mwezi wa tisa pamoja na uhakiki wa TIN za wafanyabiashara ambapo amesema siku ya mwisho kwa Dar es salaam itakuwa Oktoba 15 2016, kulia ni Gabriel Mwangosi Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA na kushoto ni Julius Ciza Afisa Mkuu wa Huduma na Elimu ya Mlipa KodiTRA Makao Mkuu.
Vituo vya uhakiki:  • Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays (Kariakoo-Gerezani)
  • Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo Complex (Tegeta) na ofisi za TRA Kimara
  • Mkoa wa Kodi Temeke: Uwanja wa Taifa na Ofisi za TRA Mbagala- Zakhemu
  • Wilaya ya Kigamboni – Ofisi za TRA Kigamboni
Pamoja na kuwakumbusha wananchi kuendelea kuhakiki na kuboresha taarifa za TIN, tungependa pia kuwakumbusha na kuwahimiza wafanyabiashara na wananchi mambo yafuatayo:-
Wasafirishaji wa mizigo kwenda mikoani wanahimizwa kudai risiti za EFDs pindi wanaponunua bidhaa na kuwa nazo wakati wanasafirisha mizigo ili kuepuka usumbufu pale wanapohitajika kuonyesha risiti hizo.
Aidha wafanyabiashara nao wanahimizwa kutoa risiti kwa wateja wao ili kuhakikisha makusanyo ya kodi yanakusanywa kwa usahihi
Waagizaji wa mizigo nje ya nchi kwa upande wao wanatakiwa kutumia mfumo wa forodha wa TANCIS kila mara kufuatilia taarifa za upakuaji wa bidhaa zao ili kuepuka udanganyifu wa aina yoyote.
Kwa kutumia TANCIS mzigo unaweza kufualiwa kwa: kuandika namba ya TANSAD sehemu ya meseji/ujumbe bila kuacha nafasi. Mfano TZDL15XXXXXX kisha tuma kwenda namba 15111. Utapata ujumbe kuhusu hatua iliyofikiwa katika kuondosha mzigo.
Kwa wale wanaoagiza magari wanashauriwa kupata taarifa za kodi wanayostahili kulipa kabla magari hayajafika ili kuepuka malalamiko ya aina yoyote pale matarajio yao yanapotofautiana na makadirio ya kodi wanayostahili kulipa. Taarifa za kodi ya magari zinapatikana katika kikokotozi kilichopo katika tovuti ya TRA
Wale Walipakodi ambao wana madeni mbalimbali ya kodi tunawashauri waonane na mameneja wa Wilaya au Mikoa ya Kodi ili kuona jinsi ya kulipa madeni hayo kuliko kukaa kimya na hivyo deni kuendelea kuongezeka.
Katika hatua nyingine TRA imekusanya jumla shilingi trilioni 3.59 katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka wa fedha 2016/17 kati ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi trililioni 15.1 mwaka 2016/17. Makusanyo hayo yanajumuisha mwezi Julai shilingi Trilioni 1.05, mwezi Agosti Trilioni 1.13 na Septemba 2016 shilingi Trilioni 1.37.
Ukusanyaji wa mapato ya serikali unaenda sambamba na kuelimisha wananchi kuhusu wajibu wao wa kulipa kodi sahihi na kwa wakati hivyo tunawaomba waandishi wa habari kuendelea kutoa elimu hiyo kupitia vyombo vyao vya habari.
Mwisho napenda kuwasisitiza waandishi wa habari kuwania tuzo ya ‘Uandishi wa Kodi na Makusanyo ya Mapato ya Serikali’ katika tuzo za Umahiri katika Uandishi wa Habari 2016, ambazo hutolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), pale MCT itakapozindua uwasilishwaji wa kazi za waandishi. ili kuendelea kuelimisha masuala mbalimbali yahusuyo kodi na kujishindia zawadi mbalimbali zitakazotolewa.
‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’
Richard M. Kayombo
Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipakodi

Wednesday, October 5, 2016

SERIKALI YAKANUSHA JUU YA TUHUMA ZA WATANZANIA KUTESWA OMAN


 Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imekanusha Taharifa zilizochapishwa na Gazeti la Tanzania Mpya yenye kichwa cha Habari kilichosema watanzania wateswa Oman na wengine na kunyofolewa figo zao na kupewa ndugu wa waajiri

akikanusha taharifa hiyo jijini Dar es Salaam leo Abdalah Kilima amesema kitendo hicho cha kuchapisha habari hiyo na kutumia picha ya Waziri Augistine Mahiga  hali iliyowanya watu wengi kuamini kuwa taharifa hiyo imetolewa na Wizara.
 "wizara inapenda kuwatangazia umma kwa ujumla kwamba mheshimiwa Dr Ausgustine Mahiga hausiki na taharifa hiyo na wala akuwahi kuzungumza na Mwandishi wa habari wa Makala husika na wala yaliyomo kwenye taharifa hiyo ni maoni binafsi ya mwandishi wa gazeti"alisema Balozi.

NECTA WANZISHA MFUMO MPYA WA UANDIKISHWAJI WANAFUNZI

Afisa Habari wa Baraza la Mitihani nchini ,John Nchimbi akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Mafanikio


Na Humphrey Shao, Dar es Salaam

Baraza la mitahani nchini limeanzisha mfumo mpya wa Kutunza Kumbukumbu za Wanafunzi wa shule za Msingi (PREM), Utakaosadia uandikishwaji wa wanafunzi wote.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema jijini Dar es Salaam leo Afisa Habari wa Baraza la Mitihani nchini John Nchimbia, alisema kuwa mfumo huo utatoa namba Maalum ambayo itamtambulisha mwanafunzi katika ngazi zote za mitihani.

“Mfumo huu utakuwa na faida nyingi sana pamoja na kusaidia katika uhamisho wa mwanafunzi kutoka shule moja kwenda nyingine ndani ya mkoa au nje ya mkoa hivyo kuondoa tatizo la wanafunzi hewa”alisema Nchimbi.

Aliongeza kuwa mfumo huu utasaidia katika uandaaji na utoaji wa Takwimu za Wanafunzi katika ngazi ya shule Wilaya ,Mkoa mpaka Taifa.

Alimaliza kw akusema kuwa Baraza limeanza kufanya majaribio ya Mfumo huu katika mikoa miwili ya Mwanza na Ruvuma na Ifikapo Disemba mfumo utaimarishwa ili Januari hadi Mei 2017 utumiwe nchi nzima kwa shule za msingi.
mwisho


++++

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...