Wednesday, October 12, 2016

MKUU WA WILAYA YA ILALA AENDELEA NA ZIARA YAKE KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI, LEO ATINGA VINGUNGUTI


 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (Kushoto) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihoji mambo kadhaa kuelewa maendeleo ya mpango wa kampuni ya PMM kuhusu mradi wa kuhamisha wanannchi kwa fidia, ili kupata eneo la shughuli za kampuni hiyo, alipokagua eneo hilo lililopo eneo la Vingunguti, akiwa katika ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika eneo la Kata ya Vingunguti, Dar es Salaam, leo. Mkuu huyo wa wilaya ameitaka PMM kuharakisha kulipa fidia wananchi wanaohusika ili waweze kujua hatma yao mapema. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa PMM Deogratius Donard
 Mkurugenzi wa Masoko wa PMM, Deogratius Donard, akimpa maelezo kwa kina, Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema kuhusu eneo ambalo kampuni hiyo inakusudia kufanya uwekezaji katika shughuli zake, Mkuu huyo wa wilaya alipotembelea eneo hilo la Uwekezaji lililopo Vingunguti, Dar es Salaam leo
 Mkurugenzi wa Masoko wa PMM Deogratius Donard akiendelea kumpa maelezo mkuu wa Wilaya
 Sehemu ya eneo ambalo Kampuni ya PMM inataka kufanya uwekezaji ambalo PMM inataka kufanya uwekezaji kwa kuwahamisha kwa malipo wananchi katika eneo la Vingunguti, Dar es Salaam.
 Mkuu wa wilaya ya Ujumbe wake wakiwa na Viongozi wa kampuni ya PMM baada ya kumaliza ziara katika kampuni hiyo leo
 Picha ya Muasisi wa Kampuni ya PMM ikiwa imewekwa pamoja na Muasisi wa Taifa la Tanzania, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, kumuezi


ZAHANATI YA VINGUNGUTI 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akipata maelezo kuhusu utendaji kazi wa Zahanati ya Vingunguti, alipokagua Zahanati hiyo leo. Kulia ni Mganga Mkuu wa Zahanati hiyo Chiku Simba. Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo
 Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema akizungumza na baadhi wa wagonjwa waliokuwa wakisubiri kupatiwa huduma katika zahanati ya Vingunguti alipotembelea Zahanati hiyo leo
  Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema akizungumza na baadhi wa wagonjwa waliokuwa wakisubiri kupatiwa huduma katika zahanati ya Vingunguti alipotembelea Zahanati hiyo leo
  Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema akizungumza na baadhi wa wagonjwa waliokuwa wakisubiri kupatiwa huduma katika zahanati ya Vingunguti alipotembelea Zahanati hiyo leo
  Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema akizungumza na baadhi wa wagonjwa waliokuwa wakisubiri kupatiwa huduma katika zahanati ya Vingunguti alipotembelea Zahanati hiyo leo
  Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema akizungumza na mfanyakazi katika chumba cha maabara katika zahanati ya Vingunguti alipotembelea Zahanati hiyo leo
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akienda kukagua wodi ya Wazazi katika Zahanati hiyo
 Mkuu wa wialaya ya Ilala Sophia Mjema akimpa maelekezo Mganga Mkuu wa Zahanati hiyo
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akitazama mtoto wa kike aliyezaliwajana katika Zahanati ya Vingunguti alipokagua Zahanati hiyo leo
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimpa pole mama aliyelezwa katika wodi ya Wazazi katika Zahanati ya Vingunguti alipokagua Zahanati hiyo leo
 Mkuu wa Wilaya akiagana na Mganga Mkuu wa hospitali hiyo baada ya ziara yake
 Watendaji katika Wilaya ya Ilala wakimuaga Mganaga Mkuu wa Zahanati ya Vingunguti.


OK PLAST LIMITED...
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya OK Plast Limited, Vingunguti, Dar es Salaam, Fadl Gadal, alipotembelea kiwanda cha Kampuni hiyo leo, akiwa katika ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya OK Plast Limited, Vingunguti, Dar es Salaam, Fadl Gadal, alipotembelea kiwanda cha Kampuni hiyo leo, akiwa katika ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi

Monday, October 10, 2016

SHINYANGA YAONGOZA NDOA ZA UTOTONI


Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Magreth Mussai 

NA VERONICA ROMWALD, DAR ES SALAAM

MKOA wa Shinyanga unaongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni kwa asilimia 59.

Vilevile, asilimia 42 ya wasichana   barani Afrika huolewa wakiwa na umri wa chini ya miaka 18.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA) linakadiria kuwa miaka 10 ijayo wasichana wapatao milioni moja wanatarajiwa kuolewa katika umri huo.

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Magreth Mussai (pichani juu) alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike.

Alitaja mikoa mingine yenye ndoa za utotoni na asilimia zake kuwa ni Tabora asilimia 58, Mara 55, Dodoma 51, Lindi 48, Mbeya 45, Morogoro 42, Singida 42, Rukwa 40 na Ruvuma 39.

Nyingine ni Mwanza 37, Kagera 36, Mtwara 35, Manyara 34, Pwani 33, Tanga 29, Arusha 27, Kilimanjaro 27, Kigoma 29, Dar es Salaam 19 na Iringa asilimia nane.

“Kwa kuwa Shinyanga inaongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni, serikali na wadau wameona vema maadhimisho hayo yafanyike mkoani humo Oktoba 11, mwaka huu kuelimisha jamii.

“Kiwango cha ndoa za utotoni nchini kipo kwa kiwango kikubwa na wasichana wengi wanaoolewa wanatoka kwenye familia maskini na wale wanaoishi   vijijini.

“Takwimu zinaonyesha asilimia 61 ya wanawake wenye umri kati ya miaka 20 hadi 24 ambao hawakusoma na asilimia 39 ya wanawake wenye umri huo wenye elimu ya msingi ndiyo walioolewa wakiwa chini ya umri wa miaka 18,” alisema.

Alisema hali hiyo inafanya ndoa za utotoni kuwa ni sehemu ya unyanyasaji wa watoto wa kike.

ASILIMIA 75 YA WANAUME HUKATAA WATOTO WAO DAR ES SALAAM


http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2510226/medRes/867304/-/7g12b7z/-/JINA.jpgPatricia Kimelemeta – Dar es Salaam
 
ZAIDI ya asilimia 75 ya wanaume wamewakataa watoto wao, hali inayosabababisha ongezeko la watoto wa mitaani jijini Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa na Mkaguzi wa Polisi Dawati la Jinsia la Kituo cha Polisi Oysterbay, Prisca Komba katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya mkakati wa ‘tunaweza kupinga vitendo vya ukatili’ uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Alisema taarifa zilizotolewa kwenye dawati hilo zinaonesha wanaume hao wamekuwa na tabia ya kuwapa mimba wanawake na kuwakimbia ili kwenda kuwapa tena mimba wanawake wengine bila kuwasaidia kulea mimba hizo au mtoto.
 http://i0.wp.com/www.multiculturalfamilia.com/wp-content/uploads/2015/08/biracial-hair-care_multicultural-familia_stock.jpg?resize=1600%2C1220
“Zaidi ya asilimia 75 ya kesi zilizofika kwenye dawati letu zimesababishwa na wanaume kukataa watoto wao, jambo ambalo limechangia kuongezeka kwa watoto wa mitaani.

“Hivyo Jeshi la Polisi litashirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wanatoa elimu ya kujitambua ili kuepuka mimba zisizotarajiwa ambazo zimechangia kuongezeka kwa watoto wasiokua na matunzo bora ya wazazi wao.

“Kuna kila sababu ya kuanzisha mkakati wa kitaifa ambao utashirikisha wanaume na wanawake kwa ajili ya kutoa elimu juu ya madhara yatokanayo na kuwakataa watoto, jambo ambalo linaweza kupunguza ukubwa wa tatizo,” alisema.

Alisema, licha ya kujitokeza kwa tatizo hilo, lakini pia kumekuwepo na vitendo vya ukatili vinavyofanywa na wazazi hao huku jamii ikifumbua macho.

Prisca alisema hali hiyo imesababisha kuongezeka kwa vitendo vya rushwa ili kuficha ukweli kwenye taarifa za ukatili zinazowasilishwa kwenye mamlaka husika ikiwamo polisi au mahakamani.
 http://dar24.com/wp-content/uploads/2016/07/ummy-mwalimu.jpg
“Jamii imekuwa ikishindwa kutoa ushirikiano kwenye taarifa za matukio ya ukatili yanayotokea kwenye jamii yao, jambo ambalo limechangia kuongezeka kwa vitendo hivyo,”alisema.

Hata hivyo, Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Grace Mbwillo, alisema Serikali inatarajia kuzindua mpango maalumu wa kufuatilia vitendo vya ukatili vinavyoendelea nchini.

Alisema, mpango huo utashirikisha wadau mbalimbali ili kupata taarifa za vitendo hivyo ili wahusika watakaobainika kufanya ukatili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Serikali haitawavumilia watu wanaoendelea kufanya ukatili nchini, hivyo basi tutazindua mpango maalumu ambao utashirikisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kupata taarifa kuhusu vitendo vinazofanywa na baadhi ya watu ili waweze kuchukuliwa hatua,

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA UMEPUNGUA KWA ASILIMIA 4.5


 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar eas Salaam leo, kuhusu mfumuko wa bei ya taifa kwa mwezi Septemba 2016. 
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo

Na Dotto Mwaibale

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba, 2016 umepungua hadi asilimia 4.5 kutoka asilimia 4.9 ilivyokuwa mwezi Agosti 2016.

Hayo yabebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar eas Salaam leo. 

" Hii inamanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Septemba, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2016 " alisema Kwesigabo.

Alisema  Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.05 mwezi Septemba 2016 kutoka 98.64 
mwezi Septemba 2015.Kwesigabo aliongeza kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi mwezi Septemba 2016 umepungua hadi asilimia 6.0 kutoka asilimia 7.0 ilivyokuwa 
mwezi Agosti 2016.

Alisema  kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 kumechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Septemba 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Septemba 2015.

Alisema mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua ni pamoja na bei za dagaa kwa asilimia 11.6 na viazi vitamu kwa asilimia 3.2.

"Kwa upande mwingine mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilionesha kupungua ni pamoja na bei za gesi kwa asilimia 10.4, dizeli kwa asilimia 2.9 na petrol kwa asilimia 2.8.

Akizungumzia mabadiliko ya bei kati ya mwezi Agosti na Septemba 2016 fahirisi za bei zimepungua hadi 103.o5 mwezi Septemba 2016 kutoka 103.28 mwezi Agosti 2016.

Alisema kupungua kwa fahirisi za bei kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.

Alitaja baadhi ya bidhaa zilizochangia kupungua kwa fahirisi ni pamoja na mchele kwa asilimia 2.6, unga wa mahindi kwa asilimia 1.0, dagaa kwa asilimia 3.0 na mbogamboga kwa asilimia 4.3.

Alisema kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na dizeli kwa asilimia 2.9, petroli kwa asilimia 2.8 na mafuta ya taa kwa asilimia 2.9

Akizungumzia thamani ya shilingi ya Tanzania kwa mwezi Septemba 2016 kutoka mwezi Desemba 2015 alisema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia sh.97 na senti 04 mwezi Septemba 2016 kutoka mwezi Desemba 2015 ikilinganishwa na shilingi 96 na senti 83 ilivyokuwa mwezi Agosti 2016.

Kwesigabo akizungumzia mfumuko wa bei kwa bidhaa ya nchi za Afrika Mashariki nchini Kenya mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 umeongezeka kidogo hadi asilimia 6.34 kutoka asilimia 6.26 mwezi Agosti 2016.

Alisema nchini Uganda mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 umepungua hadi asilimia 4.2 kutoka asilimia 4.8 mwezi Agosti 2016.

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WA NCHI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 10 Oktoba, 2016 amepokea hati za utambulisho za mabalozi wanne wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Balozi wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi, Balozi wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Mhe. Frantisek Dlhopolcek, Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk na Balozi wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Kwame Asamoah Tenkorang.

Rais Magufuli amezungumza na Mabalozi hao kwa nyakati tofauti baada ya kupokea hati zao za utambulisho, ambapo wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hizo kwa kujikita zaidi katika biashara na uwekezaji.

"Mhe. Balozi najua nchi yenu ya Sudan ina utajiri wa mafuta na imefanikiwa kujenga uchumi wake kupitia mafuta, sisi pia hapa nchini tumebaini uwepo wa mafuta na gesi asilia katika maadhi ya maeneo, ningependa uhusiano na ushirikiano wetu sasa ujielekeza katika kubadilishana uzoefu na ujuzi wa namna tunavyoweza kunufaika na mafuta na gesi"  amesema Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Sudani hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi.

Dkt. Magufuli pia ametoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi za Sudan, Slovakia, Ukraine na Ghana kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo Mafuta na gesi, Kilimo, Uvuvi, Mbuga za wanyama, Madini na ufugaji.

"Hivi sasa Tanzania ipo katika mpango wa ujenzi wa viwanda na pia tunatekeleza mpango wa pili wa maendeleo, hivyo nakuomba Mhe. Balozi uwahamasishe wafanyabiashara na wawekezaji wa Ukraine waje wawekeze katika viwanda kwani soko la uhakika la bidhaa lipo" amesisitiza Dkt. Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk.

Aidha, Rais Magufuli amewasihi Mabalozi wa Slovakia, Ukraine na Ghana ambao makazi yao ya Ubalozi yapo Mjini Nairobi nchini Kenya kuanzisha Ubalozi wao hapa nchini ili kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Oktoba, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang mara baada ya kupokea Hati yake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya utambilisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya utambilisho Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini Yevhemsi Tsymbalik Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini Yevhemsi Tsymbalik mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini Yevhemsi Tsymbalik mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia Frantisek Dlhopolcek Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Frantisek Dlhopolcek mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Frantisek Dlhopolcek mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Picha na Ikulu.

STEVE NYERERE KUHAMISHISHIA STAND UP COMEDY YAKE SERENA HOTEL

STEVE NYERERE STANDS UP COMEDY YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

Mchekeshaji Steve Nyerere akitoa burudani katika usiku wa Steve Nyerere Stand Up Comedy iliyofanyika Jumamosi Oktoba 8, 2016 ukumbi wa Little Theatre jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbali mbali waliweza kuhudhuria. Steve Nyerere amepanga kufanya onyesho la kuchekesha mara moja kwa kila mwezi ambapo mwezi ujao anatarajia kufanya onyesho hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Happi aalikuwa ni mmoja ya wageni waalikwa.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alikuwa ni miongoni mwa wageni waliofika katika usiku wa Steve Nyerere Stand Up Comedy iliyofanyika Jumamosi Oktoba 8, 2016 ukumbi wa Little Theatre jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbali mbali waliweza kuhudhuria.
Mchekeshaji Steve Nyerere akicheza muziki na msanii Dokii katika usiku wa Steve Nyerere Stand Up Comedy iliyofanyika Jumamosi Oktoba 8, 2016 ukumbi wa Little Theatre jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbali mbali waliweza kuhudhuria.
Wageni waalikwa walioweza kufika katika usiku wa Steve Nyerere Stand Up Comedy iliyofanyika Jumamosi Oktoba 8, 2016 ukumbi wa Little Theatre jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbali mbali waliweza kuhudhuria.
Vijana wakitoa burudani.
Bendi ya ngoma za asili ijulikanayo kwa jina la 'Mango Star' ikitumbuzia katika usiku wa Steve Nyerere Stand Up Comedy iliyofanyika Jumamosi Oktoba 8, 2016 ukumbi wa Little Theatre jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbali mbali waliweza kuhudhuria.
Wanenguaji Super Nyamwela, Mandela sura mbaya na Lilian Intanet wakionyesha umahili wao wa kucheza.
Mchekeshaji Steve Nyerere (katikati) akionyesha umahili wame wa kuimba katika usiku wa Steve Nyerere Stand Up Comedy iliyofanyika Jumamosi Oktoba 8, 2016 ukumbi wa Little Theatre jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbali mbali waliweza kuhudhuria. Steve Nyerere amepanga kufanya onyesho la kuchekesha mara moja kwa kila mwezi ambapo mwezi ujao anatarajia kufanya onyesho hilo.
Wageni waalikwa wakifuatilia burudani.
Muonekano wa ukumbi.
Mchekeshaji Steve Nyerere akimtambulisha mchekeshaji mwenzake Michelle.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Happi akisalimiana na wageni waliofika katika katika usiku wa Steve Nyerere Stand Up Comedy iliyofanyika Jumamosi Oktoba 8, 2016 ukumbi wa Little Theatre jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbali mbali waliweza kuhudhuria.
Wasanii nao walibadilishana mawili matatu.

TASISI YA HUMANITY ACTION FOR CHILDREN FOUNDATION YATOA VIFAA KWA WALEMAVU

 Mwanzilishi wa Tasisi ya Humanity  Action For Children Foundation , Rahma Mohamed Abdalah akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa ...