Thursday, December 15, 2016

MKURUGENZI MALINYI AHAMISHIA OFISI CHINI YA MTI

Marceline Ndimbwa


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ,  Marceline Ndimbwa amelazimika kufanyia kazi nje ya ofsi kutokana kukumbwa na majukumu ya kusimamia ujenzi wa madarasa hili kuweza kuenenda na kasi ya rais John Pombe Magufuli aliyemuagiza kumaliza ujenzi huo ndani ya mwezi huu.
Katika hali isiyo ya kawaida mkurugenzi huyo ambaye ameonekana katika eneo la ujenzi akiendelea na kazi zingine za kiofsi huku akiwa na lundo la mafaili ambayo alikuwa akiyasaini hili kuweza kuruhusu shughuli zingine za kiofisi zikiendelea.
Kwa upande wake mkurugenzi huyo alipo ulizwa juu ya swala hilo amesema kuwa jambo ni la kawaida katika mazingira ya kazi kwani jambo moja aliwezi kukwamisha shughuli nyingine zisiendelee wakati wananchi wana mahitaji ya haraka.
Amesema kuwa Rais alimuagiza kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika kwa wakati hivyo yeye kama mteule anahakikisha kuwa anatekeleza agizo hilo kwa wakati hili watu wa Malinyi waweze kunufaika na ahadi za Rais Magufuli.
Amemaliza kwa kutoa wito kwa wakazi wa malinyi kuwa na imani na serikali yao ambayo kipaumbele chake ni kutumikia wanyonge kwa kurekebishe miundombinu ya elimu kwa kipindi kifupi.

MAJALIWA AWASILI LOLIONDO KUENDELEA NA ZIARA YA MKOA WA ARUSHA Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakati alipowasili kwenye  uwanja wa ndege wa Kiltaro katika tararafa ya Loliondo kuendelea na ziara yake wilayani Ngorongoro Desemba, 15, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanawake wa Kimasai wakati alipotembelea Kituo mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni kilichojengwa na UNICEF katika kijiji cha Ololosokwan kilichopo Loliondo wilayani  Ngorongoro Desemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kazi mbalimbali za mikono hasa mapambo yanayotengenezwa na wanawake wa kimasai katika kijiji cha Ololosokwan katika tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro wakati alipotembelea Kituo cha Mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni  kijijini  hapo Desemba 15, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa ndani ya nyumba ya asili ya wamasai maarufu kwa jina la Emanyatta katika kijiji cha Ololosokwan  kwenye tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Desemba 15, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka ndani ya nyumba ya asili ya wamasai maarufu kwa jina la emanyatta katika kijiji cha Ololosokwan kwenye tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Desemba 15, 2016. 
 Wananchi wa kijiji cha Ololosokwan  kwenye tarafa ya  Loliondo wilayani Ngorongoro  wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipowasalimia akiwa ktika ziara ya wilaya ya Ngorongoro Desemba 15, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanchi wa kijiji cha Ololosokwan katika tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro akiwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MABALOZI WA NNE KWA WAKATI TOFAUTI NA KUFANYA NAO MAZUNGUMZO


Mabalozi wa Nchi Mbili za Brazil na Kenya wameipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa mipango na mikakati yake ya madhubuti ya kulifufua Shirika la Ndege Tanzania -ATCL – kwa kununua ndege mpya kama hatua ya kuhakikisha shirika hilo linakuwa bora katika utoaji wa huduma za usafiri wa anga ndani na nje ya nchini.
Mabalozi hao wamesema hatua hiyo ya kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania itasaidia kukuza shughuli za utalii na pato la taifa kwa ujumla.Balozi wa Brazil nchini Carlos Alfonso Puente na Balozi wa Kenya hapa nchini Chirau Ali Makwere wametoa pongezi hizo mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikulu jijini Dar es salaama.
Kwa upande wake, Balozi wa Brazil nchini Carlos Alfonso Puente amesema kutokana na nchi hiyo kuwa ni miongoni mwa nchi kadhaa Dunia zenye viwanda wa kutengeneza ndege hivyo serikali ya Tanzania ina nafasi nzuri ya kununua ndege nchini Brazil hasa kulingana na mahusiano mazuri na ya muda mrefu yaliyopo kati ya nchi hizo mbili.
Kufutia wito huo wa Balozi wa Brazil Nchini, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wa nchi ya Brazil kuja nchini kutangaza bidhaa wanazotengeneza hasa ndege kama hatua ya kuimarisha mahusiano ya biashara kati ya Brazil na Tanzania.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kutokana na nchi ya Brazil kupiga hatua kubwa katika uzalishaji wa sukari na Tanzania ni moja ya nchi yenye maeneo mazuri kwa ajili ya uwekezaji huo hivyo ni muhimu kwa wafanyabiasha wa Brazil kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta hiyo.
Kuhusu kilimo cha Pamba nchini, Balozi wa Brazil Carlos Alfonso Puente amesema serikali ya nchi hiyo imeanzisha mradi kabambe unaolenga kusaidia uzalishaji bora wa pamba katika mikoa ya kanda ya ziwa mradi ambao utagharimu dola za Kimarekani milioni Sita kwa miaka minne nchini.
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika mazungumzo yake na Balozi wa Kenya hapa nchini Chirau Ali Makwere amesisitiza kudumishwa na kuendelezwa kwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Kenya hasa katika uimarishaji wa biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo Mbili.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito maalum kwa Watanzania kuchangamkia fursa ya kufanya biashara na nchi ya Kenya kutokana na nchi mbili kuwa na mahusiano mazuri ya kibiashara.
Wakati huo huo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini Hebogand Jensen ambaye amemweleza Makamu wa Rais nia ya nchi hiyo kwa ushirikiano na nchi nyingine ya kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea wilayani Kilwa.
Balozi huyo wa Denmark nchini amesema anaimani kiwanda hicho kitakachojengwa nchini kitafanya uzalishaji mkubwa na kutoa ajira kwa mamia ya wananchi wa Tanzania.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali katika kuelekea kwenye uchumi wa viwanda imeweka mazingira mazuri kwa ajili ya wawekezaji wanaotaka kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini kama hatua ya kukuza uchumi wa nchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Kenya Nchi Mhe. Ali Makwere, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Brazil Nchi Mhe. Carlos Alfonso Puente, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Denmark Nchi Mhe. E. Hebogand Jensen, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), Mhe. Maniza Zaman, mara baada ya kumaliza mazungumzo,Ikulu jijini Dar es Salaam.

MAKONDA AKUTANA NA MACHINGA WA KARIAKOO


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza nawafanyabiashara ndogo ndogo marufu kama Machinga mtaa wa Kongo na kusikiliza kero zao leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza wafanyabiashara wa soko kuu la Kariakoo nakusikiliza kero zao leo jijiji Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa na viongozi mbalimbli akikagua soko la Kariakoo.
Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akifafanua jambo katika mkutano wawafanyabiashara ndogo ndogo Machinga mtaa wa Kongo leo jijiji Dar es Salaam.
Wafanyabiashara na wananchi wakimsikiliza mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

WAFANYABIASHARA ndogo ndogo wa Kariakoo wametakiwa kuuza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani ili kukuza uchumi wa viwanda. Hayo ameyasema leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokutana na wafanyabiashara wandogo wandogo wa Kariakoo, amesema bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vya ndani zikipata soko nchi itapata mapato pamoja na kukuza uchumi wa nchi yetu.

Amesema serikali iko pamoja na wamachinga kuhakikisha wanafanya biashara kwa mujibu wa sheria kwa kuuza vitu vyenye ubora na wakibaini kuwepo kwa vitu ambavyo vinahatarisha maisha ya watanzania watachukuliwa hatua mara moja.

Makonda amesema ni marufuku wageni kutoka nje ya nchi kufanyabiashara ya umachinga katika jiji la Dar es Salaam wao wanatakiwa kuleta utaalam tu. Aidha amewaasa wamachinga kuwafichua wale ambao wanaweka rebo katika bidhaa wakati hawazalishi wenyewe.

Makonda amesema katika maeneo ambayo wanafanyia kazi wamachinga kufuata sheria na kanuni zilizowekwa bila kuharibu utaratibu.

UNICEF YAADHIMINISHA MIAKA 70 TANGU KUANZISHWA, SERIKALI YAIPONGEZA KWA KUSAIDIA WATOTO


Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) limeadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa (1946-2016) likiwa na kauli mbiu ya Kwa Kila Mtoto, Tumaini. Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bi. Maniza Zaman alisema shirila lao kwa kipindi cha miaka 70 limekuwa likifanya kazi za kuwasaidia watoto ambapo malengo yao ni kuhakikisha watoto wanaishi maisha bora na kuwawezesha kufikia malengo ambayo wanatamani kuyafikia. 
Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman akielezea kazi ambazo UNICEF imekuwa ikizifanya kwa miaka 70 tangu kuanzishwa na mafanikio ambayo wameyapata.

"Hii ni siku muhimu kwetu kufikisha miaka 70, ni muhimu kwa sababu ya malengo ambayo yamewekwa ya kujenga dunia ambayo kila mtoto atapata haki zake za kimsingi bila kumuacha hata mmoja nyuma ni muhimu sababu ya uwepo wenu kujadili umuhimu wa watoto ambao utatoa matumaini mapya kwa kila mtoto Tanzania, "Kwa miaka 70 UNICEF imekuwa ikiwatetea watoto, kwa pamoja tukishirikiana na wadau wetu kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha tunaboresha maisha ya kila mtoto duniani kote. Mpango wetu upo wazi kuwa kuhakikisha kila mtoto anapata nafasi ya kufikia malengo yake," alisema Zaman. Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema UNICEF ni washirika wazuri wa serikali kutokana na programu ambazo wamekuwa wakitoa kwa watoto na kuwaomba kuendelea kushirikiana na serikali ili kuboresha maisha ya watoto nchini. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza faida ambazo Tanzania imepata kutokana na uwepo wa UNICEF nchini pamoja na kumshukuru Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kwa kusaini mkataba ambao uliwaruhusu UNICEF kuingia nchini kwa ajili ya kuwasaidia watoto.

"Serikali ya Tanzania itaendelea kulinda na kutetea haki za watoto na katika utekelezaji wa hili tunawashukuru sana UNICEF kwa programu ambazo wamekuwa wakizifanya, watoto wa Tanzania wamefaidika sana na programu ambazo UNICEF mnazitoa na serikali itaendelea kushirikiana na UNICEF kuwasaidia watoto nchini," alisema Mwalimu. Kwa upande wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN), Alvaro Rodriguez alisema UNICEF imesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha ya watoto duniani kote tangu ilipoanzishwa na kupitia mpango wa SDGs ni matumaini ya UN kuwa serikali ya Tanzania kwa kushirikiana nanyi zitaendelea kushirikiana ili kuwasaidia watoto. 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN), Alvaro Rodriguez akielezea jinsi UNICEF ambavyo natekeleza mipango ya Umoja wa mataifa kwa kuanza na mpango wa kwanza wa Millenium Development Goals (MDGs) ambao ulimalizika mwaka 2015 na mpango wa sasa wa maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals - SDGs).

"Mchango wa shirika hili la watoto ni mkubwa, muhimu na wenye thamani kubwa sana katika dunia ya leo na kesho, kwa miaka 15 iliyopita tulikuwa na mpango wa MSDs ambao ulishughulikia changamoto ambazo zinawakabili watoto na sasa kuna mpango wa SDGs ambao tumekusudia ufanye mageuzi makubwa kwa maendeleo ya baadae ya binadamu wakiwepo watoto, na Tanzania kama mwanachama wa UN ina wajibu wa kuhakikisha inafanikisha hilo," alisema Rodriguez. 
Rais wa pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi akitoa pongezi kwa UNICEF kwa kazi ambazo wanafanya za kuwasaidia watoto ili waishi katika mazingira bora.

Nae mgeni wa heshima katika maadhimisho hayo, Rais wa pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi aliipongeza UNICEF kwa kufikisha miaka 70 na kusema kuwa "Nilihusika kukubali UNICEF kufanya kazi nchini na leo sijuitii hilo kwa kazi ambayo mnaifanya, niwatie moyo muendelee na kufanya kazi kwa kuwasaidia watoto." 
Baadhi ya watu waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa shirika la UNICEF.

MAKONDA AKUTANA NA MACHINGA WA KARIAKOO


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza nawafanyabiashara ndogo ndogo marufu kama Machinga mtaa wa Kongo na kusikiliza kero zao leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza wafanyabiashara wa soko kuu la Kariakoo nakusikiliza kero zao leo jijiji Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa na viongozi mbalimbli akikagua soko la Kariakoo.
Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akifafanua jambo katika mkutano wawafanyabiashara ndogo ndogo Machinga mtaa wa Kongo leo jijiji Dar es Salaam.
Wafanyabiashara na wananchi wakimsikiliza mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAFANYABIASHARA ndogo ndogo wa Kariakoo wametakiwa kuuza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani ili kukuza uchumi wa viwanda. Hayo ameyasema leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokutana na wafanyabiashara wandogo wandogo wa Kariakoo, amesema bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vya ndani zikipata soko nchi itapata mapato pamoja na kukuza uchumi wa nchi yetu.

Amesema serikali iko pamoja na wamachinga kuhakikisha wanafanya biashara kwa mujibu wa sheria kwa kuuza vitu vyenye ubora na wakibaini kuwepo kwa vitu ambavyo vinahatarisha maisha ya watanzania watachukuliwa hatua mara moja.

Makonda amesema ni marufuku wageni kutoka nje ya nchi kufanyabiashara ya umachinga katika jiji la Dar es Salaam wao wanatakiwa kuleta utaalam tu. Aidha amewaasa wamachinga kuwafichua wale ambao wanaweka rebo katika bidhaa wakati hawazalishi wenyewe.

Makonda amesema katika maeneo ambayo wanafanyia kazi wamachinga kufuata sheria na kanuni zilizowekwa bila kuharibu utaratibu.

KINANA AZINDUA JENGO LA KITEGAUCHUMI LA CCM, UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO
Jengo la kisasa la Kitegauchumi la Chama Cha Mapinduzi (CCM), lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, lililozinduliwa leo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Anna Abdallah, ujenzi wa jengo umegharimu sh. Bilioni saba.Mama Anna Abdallah, amesema, jengo hilo limejengwa kwa hali ya juu na limewekwa kila kitu ikiwemo zamani.

"Mpangaji anapotaka kuingia katika nyumba hii, yeye anachopaswa kufanya ni kuja na chakula na nguo tu, halazimiki kuingia na samani yoyote hata TV anaikuta ipo sebuleni", Alisema, Mama Anna. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua jengo la kisasa la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mama Zakia Megji na Mama Anna Abdallah. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua rasmi jengo hilo. Kushoto kwake ni Mama Anna Abdallah na kulia kwake ni Mama Zakia Meghji. Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la Kisasa la Kitegauchumi la CCM, lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Baadhi ya waalikwa wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la kisasa la kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo.

Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa mali za CCM, Mama Anna Abdallah, akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la Kisasa la Kitegauchumi la CCM, lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza kabla ya kuzindua jengo la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia baadhi ya wanachama wa CCM wakati akienda kuzindua jengo la Kitegauchumi la CCM, lililopo Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mama Zakia Meghji
Katibu Mkuu wa CCM, Andulrahman Kinana akienda kukagua ndani ya jengo Kinana akitazama ukumbi wa mikutano katika jengo hilo Kinana akisalimiana na mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa mali za CCM wakati akikagua jengo.Samani ndani ya jengo
🔻


jikoni

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na baadhi ya viongozi kabla ya kuondoka baada ya kuzindua rasmi jengo la kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-theNkoromo Blog

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...