MWAMBUSI AKIRI UKABAJI UMEIGHARIMU YANGA



Kocha msaidizi  wa yanga Juma Mwambusi akiwa na kocha mkuu wa timu hiyo George Rwandamina wakipanga jambo katika mchezo wa dhidi ya Simba.

 Na Humphrey Shao, Globu Ya Jamii
Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amekiri kuwa timu yake ilikuwa na tatizo katika eneo la ukabaji na kupelekea kuchapwa bao 2-1.

Mwambusi amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo na kutaja ubovu wa timu yake.
“tulianza mchezo huu vizuri lakini tatizo la ukabaji katika timu yetu ndio limetugharimu na kuwapa wapinzani wetu ushindi wa wazi ambao kila mtu ameuona” amesema Mwambusi.

Mwambusi ametaja kuwa kulikuwa hakuna sababu ya timu yao kupoteza mchezo huo kwani tayari walikuwa washatangulia kwa bao moja hivyo walikuwa na nafasi nzuri ya kupata ushndi lakini uzembe wa wachezaji wachache umeigharimu timu.
Ametaja kuwa tatizo lililowakuwa wapinzani wao la kupewa kadi Nyekundu lilikuwa zawadi tosha ya kuondoka na ushindi lakini bado wachazaji walishindwa kukaba.

Post a Comment

Previous Post Next Post