Wednesday, February 8, 2017

SIMU NA MANGE KIMAMBI KUMSOTESHA WEMA SEPETU RUMANDE
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Matumizi ya simu ya mkononi huku akiwa ameshikiliwa na jeshi la Polisi ni moja ya mambo yalitojwa kumfanya mtuhumiwa wa kesi ya Dawa za kulevya Wema Sepetu kuendelea kusota rumande.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa moja ya makosa katika nchii hii ni mtu akiwa yupo chini ya ulinzi alafu kuendelea kutumia simu ya mkononi.
Amesema kuwa mrembo huyo ambaye alikuwa akituma Video na sauti mbalimbali kuhusu hali ya maisha akiwa mahabusu ya kituo cha kati huku akimkejeli mkuu wa mkoa uenda akaendelea kuwa katika wakati mgumu zaidi kutokana na kitendo hicho cha kutumia simu akiwa mahabusu.

Makonda ametaja kuwa amezungumza na wakuu wa magereza yote yaliyopo Dar es Salaam na wakuu wa mikoa juu ya vitendo vya watu kuingia na simu katika vituo vya Polisi.
Pia amesema kuwa matumizi ya simu hizo watu wakiwa gerezani yamekuwa yakitumika kuendeleza biashara zao za dawa za kulevya kwa njia ya mawasiliano hata kama wakiwa ndani.


No comments:

Post a Comment

JK AWATAKA WASANII WA BONGO MOVIE KUJIONGEZA NA KUACHA KULALAMIKIA SERIKALI

 Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza wakati wa uzinduzi Televisheni  inayoshughulika na masuala ya filamu...