STARTIMES YASHEHEREKEA VALENTINE NA WATEJA

 Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania ,Felix Awino akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao
 Bwana na Bibi Alex wakifurahi mara baada ya kukabidhiwa zawadi kampuni ya Star Times Tanzania
 Meneja uhusiano wa kampuni ya Sar Times Tanzania Juma Suluhu akikabidhi zawadi kwa Bwana na Bibi Nuezy Fredrick
 Wafanyakazi wa Star Times Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja  wakiwa wameshika maua
 Meneja uhusiano wa kampuni ya Sar Times Tanzania Juma Suluhu na Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania ,Felix Awinowakikabidhi zawadi kwa washindi wa Ni Valentine's na Star Times






Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

KAMPUNI ya Star Times imesheherekea siku ya wapendanao na wateja wake kwa kutoa zawadi kadhaa katika promosheni yake ya "Ni Valentine na Startimes".

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi zawadi hizo Meneja Masoko wa kampuni hiyo Tanzania, Felix Awino amesema Star Time inasheherekea siku hii kwa kuwazawadia wapenzi kupata chakula cha jioni na malazi ya Hotel ya kisasa.

“tunafurahi kusheherekea siku ya wapendanao na wateja kwa kuwa karibu nao kama sehemu ya upendo wetu kwao kwa kuwapa promotion na maudhui yanayoendana na wakati hivyo kwa wateja wetu wa Dar es Salaam watapata malazi SeaScape,  Mwanza watalala katika hoteli ya Malaika , Meya wataenda Usungilo , Arusha Palece Hotel na kwa mkoa wa Dodoma watapata kupumzika katika Hotel ya Morena”amesema Awino.

Kwa upande wake mmoja wa washindi wa promotion hiyo ya ni Valentine na Startimes, Nuezy Fredrick amesema kuwa ni furaha kubwa kwao kama wateja wa Star Times kupata nafasi hiyo ya kupelekwa sehemu ya kifahari kama hiyo hili waweze kufurahi na wapenzi wao kutokana na kutumia king’amuzi cha Star Times.

Amesema kuwa star Times imemuheshimu na yeye ataendelea kutumia bidhaa za kampuni hiyo na kufurahia vipindi bomba vya kila siku.

Post a Comment

Previous Post Next Post